Mbeya: Askari Polisi afariki kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi

Mbeya: Askari Polisi afariki kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi

View attachment 2770839
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ametoa taarifa za tukio la Askari kujiua kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi.

Amesema tukio la kujiua kwa kujipiga risasi kwa aliyekuwa Askari J.2596 Konstebo wa Polisi Samwel Feston Kaziyote [24] wa kituo kikuu cha Polisi Mbeya.

Ni kwamba, Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku huko maeneo ya Mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani, Jijini Mbeya Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kisha kuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Kaziyote amemaliza kaziyote. Ukiiangalia sura yake macho yanaonesha kama mzee wa visungura.
 
Huyo dogo ukute alienda home kwa pisi yake hakuikuta aisee...yaani kakitafuta kifo mwenyewe shida ya wadogo wengi wakishakamatwa wanadhani huko nje hakuna pisi kali kama hiyo tena...
 
itoshe kusema marehemu ni bwege , minyapu ilivyojaa dunia hii Duh hawa madogo wa umri wake Jau sana
 
Kama 2001 ni mashangaz,kuanziaa 90 ni kina nani?
 
Ni mapenz jamani au ni stress?? mm Hawa jamaa nikiambiwa Wana ugumu wa maisha siamin kwa kwel kwa sabab form 4 baada ya stahiki zote anapat lak 7 makato tayar apo na form 6 usisem ukitoa hapo Wana pesa za nje za Malindo escort nk halaf mtu anasem Wana stress za maish Kun watu hawaipat Kam hio na mbon wapo vizur au wao tatzo nn au hawan muda wa kujiekeza
 
vijana wa kiume wanapaswa kuanza kushauriwa kuhusu mioyo ya wanawake mara wanapobalehe.....mioyo ya wanawake ni vichaka vina kila aina ya hatari ndnai yake. Hata ndoa kwa sasa ni shida. Wanawake wengi wako ktk ndoa kwa sababu hana kwa kukamata. Akishapata tu anamwanzishia mume vurugu.
Anaanzisha vurugu ili iweje?
 
Alafu alikuwa anakaa na bunduki huyu

Ova
 
Mbona mapenzi yanatutesa sana wanaume kijana mdgo anakatisha future yake kisa mapenzi
 
Hii pisi dogo aliona bora aiche wahuni wairukie...
 

Attachments

  • IMG-20231005-WA0004.jpg
    IMG-20231005-WA0004.jpg
    116.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom