Uchaguzi 2020 Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi wakati akichukua fomu ya Uteuzi

Nani kafanya kutoka CCM kipindi hiki cha uchaguzi amekusanya watu (kwanza washatoa hata hiyo list yao ya wagombea ubunge) sio CCM tu chama gani kingine kimefanya mkusanyiko?

Ata mapokezi ya Lipumba yalipata kibali cha polisi.
Wewe hujaona shughuli mbalimbali za CCM??? Kwani wale vijana wa uvccm waliokusanyika daraja la flyover ubungo kumpokea magufili wakati anatoka Dodoma walikuwa na kibali??
 
Mbona siku wamempokea Lissu waliandamana na hakuna tatizo lililotokea hii nchi kama vurugu zitakuja kutokea zitasababishwa na jeshi la polisi na IGP afahamu hilo ili siku yakitokea asiseme yeye hahusiki.
Unamawazo mgando sana kwahiyo ulitaka na siku hiyo akamatwe?
 
Hili ndio tatizo lenu ni juzi tu IGP kawafafanulia ni kosa kufanya ivyo bila ya kibali ni hekima tu inawaongoza wanapokaa kimya.
Muda mwingine polisi nao wanachokozwa, watu wanafanya mambo yaliyokatazwa kwa makusudi ili wapate sababu tu.
 
Naomba hamasisha vijana wa Mbeya mbona wamekaa kisengesenge bwana wanamuangusha Sugu police ni wachache vijana mkiamua mnaweza bwana acheni uoga wa ki senge BAVICHA amkeni bwana.
Watapata majibu hao polisi. Uonevu sasa basi. Imetosha kwa kweli
 
Haya yana mwisho kura yangu kwa upinzani
 
Balaa hii. Yote haya ni mkuu wa mkoa aliyeapa kumuangusha Sugu.
Ni kweli Chalamila anahusika na njama zote kuhakikisha Tulia anashinda Jimbo la Mbeya. Hata kwenye kura za maoni ndani ya CCM tuliona Ndele Mwaselela akitishiwa asichukue fomu ya kutia nia. Na Cosmas Mwaifwani naye alidhibitiwa na TAKUKURU mara alipoonekana Mbeya kabla ya kura za maoni.

MC Charles Mwakipesile aliandikiwa onyo asijihusishe na siasa. Wote hao watatu ni wazawa tofauti na Tulia Ackson anyetokea Rungwe.
 
Duhhhhh. Kweli hakuna mbabe wa njaa
 
Uvunjivu wa amani nchini unasababishwa na ccm kupitia kwa vyombo vya usalama! Ni mambo ya aibu kabisa haya! wao wakifanya hakuna noma ila wengine ni vita tupu!
 
Hayo ni maagizo ya chalamila kwa ujinga huu wanazidi kuupa upinzani nguvu siasa sio uadui jamani
Mwenyekiti wangu Mh raisi magufuli hawa wateule wako wanakuangusha na ndio maana unakuta mbeya mjini wanaichukia ccm kwa sababu ya mambo kama haya
hebu tujalibu kuangalia kwa jicho LA pili huu uchanguzi utatuchafua sana tusipo kuwa makini
moyo wa upendo
Moyo usio na hila
Siasa zitapita
Tanzania itabaki
 
Police munawapa watu kiki za bure kabisa. Haikua na haja kumkamata. Mungemuacha achukue fomu harafu kama kuna tatizo mungemuita ofisini kwenu. Katika hili mumeniangusha sana police. Hii kiki mumeitoa kirahisi sana.
 
Vijana wa Mbeya Embu leo pelekeni salamu kwa hao watu wajue Uchaguzi huu hatutaki uonevu. Wala msiukalie kimya huu uonevu wa mchana kweupe. Najua hamuwezi kuniangusha
 
Wewe kwa akili yako timamu ni kweli hasa unaamini kama hao polisi wana sababu ya kweli ya kumchukuwa Sugu akiwa ndani ya jengo la tume akichukuwa fomu ya kugombea? Huo ustaarabu ulizaliwa Tanzania?
 
14 August 2020
Mbeya, Tanzania

Hali Halisi Ilivyokuwa Katika ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Ofisa wa Polisi : Naomba Twende kuna mahojiano
Sugu :Mahojiano ya nini?
Ofisa wa Polisi : kuhusu maandamano !
Sugu: Maandamano ?


7 August 2020
MZEE BUTIKU AFUNGUKA, AWAKUMBUSHA POLISI, USALAMA WA TAIFA, TPDF / JWTZ NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAJIBU WAO
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku amesema ili uchaguzi wa Oktoba uwe huru na haki vyombo vya dola vinatakiwa kuhakikisha vinavilinda vyama vyote kwa usawa, huku akieleza kuwa lengo la uchaguzi ni kupata viongozi watakao tetea maslahi ya taifa ikiwa ni pamoja kupambana na Rushwa.
Source: mwananchi digital
https://fikrapevu.com › kumbuk...
KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE: Wasomi wahoji uhuru ...

13 Apr 2018 · ... Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema baba wa taifa alituachia msingi mzuri wa
 
Lakini polisi walivyokuwa wamewapa nafasi tangu Tundu Lissu amerudi, mliwasifu sana sasa mnawachokoza tena?
Kwahiyo wakifanya kosa isisemwe kisa waliwahi kufuata utaratibu? au wewe ndo jamii ya wale wanaokula kodi ya wananchi bure kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…