Mbeya: Kikundi cha kihalifu maarufu kama vibeberu com chabaka wananchi mchana kweupe

Mbeya kuna ushirikina sanaa…ukute mashart ya waganga
 
Kikundi cha ubakaji maarufu kama 'Vibeberu.com' kilichopo Kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kimezua taharuki baada ya kudaiwa kufanya vitendo vya ubakaji kwa watoto.

Inadaiwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya vitendo hivyo vya ubakaji mchana kweupe hali inayowatia hofu wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Ipinda (jina limehifadhiwa) amesema kitendo cha walimu kuwaagiza wanafunzi kuwahi saa 12 asubuhi kushika namba shuleni, kimechochea hatari ya watoto kubakwa, hivyo ameomba wanafunzi waongezewe muda walau saa moja asubuhi.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Erick Komba amesema idadi ya watoto walioripotiwa kubakwa ni zaidi ya watoto 8 ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Chanzo: Swahili times
Shida iko wapi wakubwa? Si wanafanya vitendo hivyo vya uhalifu mchana kweupe? Kwa hiyo wanaonekana mnawaona au mnashuhudia wakitenda uvunjifu wa sheria. Kwa nini msimalizane nao mnasubiri upelelezi wa Polisi? Mbona hawatendi wakiwa na bisibisi, kisu wala panga au rungu na nondo? Kha, eti mtoto wa1, mtoto wa 2,mtoto wa 3... hadi mtoto wa 8 nyie bado mmekalia kutunza tu mahesabu. Amkeni, jipangeni ifike mahali na hao vibeberu mzazi wa "kibeberu" aelekezwe kwenda kumtambua kibeberu wake hospitali(Mortuary) au Kituo cha Polisi. Msiogope kwani walianza bila sheria na wanatakiwa waishe bila sheria. Kwani panyarodi walifanywa nini? Unawasikia tena? OK. Kazi kwenu - Kazi iendelee.
 
Hawa vibeberu inabidi wahenyeshwe wakidakwa
 
Kikundi cha ubakaji maarufu kama 'Vibeberu.com' kilichopo Kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kimezua taharuki baada ya kudaiwa kufanya vitendo vya ubakaji kwa watoto.

Inadaiwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya vitendo hivyo vya ubakaji mchana kweupe hali inayowatia hofu wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Ipinda (jina limehifadhiwa) amesema kitendo cha walimu kuwaagiza wanafunzi kuwahi saa 12 asubuhi kushika namba shuleni, kimechochea hatari ya watoto kubakwa, hivyo ameomba wanafunzi waongezewe muda walau saa moja asubuhi.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Erick Komba amesema idadi ya watoto walioripotiwa kubakwa ni zaidi ya watoto 8 ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Chanzo: Swahili times
Kwa ukomavu wa tendo hili la ubakaji, Serikali sasa inastahili iongeze adhabu stahiki yaani pamoja na kifungo pia wahasiwe (waondolewe kiume - castration).
Adhabu hiyo nina hakika itapunguza au kuondosha kabisa tendo hilo la kinýama.
 
Kamatani nanyi wainamisheni hao makima.
Samahani Chifu, hii pp yako haijakaa kiuchangamfu kama ile inayoonesha Ke akiwa anapelekewa moto kwenye PC na Me huku pakiwa na picha ya Mama

Ni mtizamo wangu tu ikikupendeza urudishe ile pp ya awali maana sisi wadau wa JF tulishawahi kuwaeleza hivyo Espy na Extrovert hatimaye walirudisha pp zao za awali... [emoji2960]
 
Saa kumi na mbili kuripoti, saa moja kuhesabu Namba, baada ya hapo usafi wa mazingira, vyoo nk, baada ya hapo saa 1:30 ukaguzi kwa wanafunzi pamoja na matangazo, saa mbili kamili darasani.

Kama unaona watoto wako wanaonewa peleka Toto lako international school, mnajifanya wajuvi kumbe bure tu, hamjui hata mtaala wa Elimu unasemaje, unadhani sisi walimu tunapenda kuamka saa kumi na mbili?? Au Ni kwasabu mtaala na kanuni zinatutaka tufanye hivyo!!
Mwambie mwalimu mwambie vizuri akuelewe, kasoma English Medium, Saint Kayumba anazisikiaga tu

Beesmom upitie na huku
 
Na baridi ya mbeya unamuwahisha mtoto saa 12 kisa kushika namba ...
Hao walimu ni wapuuuzi kabisa.
Walimu wa Kyela wameshakupa jibu mkuu Kyela hakuna baridi, baridi lipo Nzovwe, Ivumwe, Teku hadi Mama Jon, Soko Matola hadi Uyole kabla hujakatiza Mafiati km unaelekea Mbalali
 
Back
Top Bottom