Mbeya: Kikundi cha kihalifu maarufu kama vibeberu com chabaka wananchi mchana kweupe

Mbeya: Kikundi cha kihalifu maarufu kama vibeberu com chabaka wananchi mchana kweupe

Kikundi cha ubakaji maarufu kama 'Vibeberu.com' kilichopo Kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kimezua taharuki baada ya kudaiwa kufanya vitendo vya ubakaji kwa watoto.

Inadaiwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya vitendo hivyo vya ubakaji mchana kweupe hali inayowatia hofu wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Ipinda (jina limehifadhiwa) amesema kitendo cha walimu kuwaagiza wanafunzi kuwahi saa 12 asubuhi kushika namba shuleni, kimechochea hatari ya watoto kubakwa, hivyo ameomba wanafunzi waongezewe muda walau saa moja asubuhi.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Erick Komba amesema idadi ya watoto walioripotiwa kubakwa ni zaidi ya watoto 8 ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Chanzo: Swahili times
Vipi hawajamfikia Betina Bado??
 
Hali ya hewa ya kyela ni kama Dar, ule ni ukanda wa ziwa nyasa
Screenshot_20221018-081631.png
Screenshot_20221018-081638.png
 
Dar Kuna Panyaroad
Mbeya Kuna vibeberu dot com
Mwanza vipi?
Arusha vipi?
 
Aiseee
Ipinda kuna mashamba mengi hivyo rahisi mtu kubakwa
 
Akizungumza mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Ipinda (jina limehifadhiwa) amesema kitendo cha walimu kuwaagiza wanafunzi kuwahi saa 12 asubuhi kushika namba shuleni, kimechochea hatari ya watoto kubakwa, hivyo ameomba wanafunzi waongezewe muda walau saa moja asubuhi.
Kuna mtandao wa simu wenye nembo fulani mbaya ndiyo umechangia haya kwa kauli yao ya "cha asubuhi"
 
Back
Top Bottom