Mwalimu ajulikanaye kwa jina la Sabina Haule amewapa adhabu wanafunzi wake wa shule ya msingi kwa kuwafungia darasani usiku kucha wakipigwa na baridi huku yeye akienda kulala nyumbani na mume wake. Adhabu hii imedumu kwa muda sasa hadi pale wazazi walipoenda kulalamika kwa mkuu wa mkoa, ndugu Homela.
Baaada ya wazazi kumpa taarifa RC alifanya ziara ya kushtuka shuleni hapo usiku wa manane ambapo aliwakuta wanafunzi hao wakipigwa baridi huku wakiwa hawana blanketi za kujifunika wala nguo za kuwakinga na baridi. Ndipo mkuu wa mkoa alipochukua jukumu la kuvunja mlango na kuwakoa wanafunzi waliokuwa wakitetemeka kwa baridi kali ya usiku.
Kufuatia tukio hili, RC amewaomba wanafunzi kuwa na nidhamu kwa walimu huku akiahidi kumshughulikia mwalimu aliyehusika na tukio hili hasa ukizingatia wanafunzi waliolazwa darasani bado ni watoto wadogo. Aidha, aliwashauri walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni. Ikumbukwe wiki iliyopita mwalimu mmoja alitiwa mbaroni mkoani humo kwa kuwachomeka mimba wanafunzi wawili huku akimchomoa mimba mmoja wao.
Chanzo: RFA; habari na matukio 13/07/2023
MAONI YANGU
Hili liwe fundisho kwa wanafunzi wenye tabia mbaya na wasiowaheshimu walimu. Wanafunzi wa kizazi hiki wana vichwa vigumu sana. Hawasikii. Hii inatokana na malezi mabovu kutoka kwa wazazi na jamii inayowazunguka. Wazazi tuongeze juhudi za kuwalea watoto wetu kuwa na nidhamu ya kuwaheshimu walimu na watu wengine katika jamii.
Nawasilisha.