Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

Ni kweli wanafunzi ni watukutu ila adhabu ziangalie utu wa wanafunzi,
Adhabu nyingi zinazotolewa zinakiuka hadi za binadamu.
Ndio nakwambia kuna baadhi ya walimu wamevamia fani sio wote kwa hio waangaliwe kwa jicho la ndani, mwingine hata hana passion na ualimu ilibidi awe magereza huko akajikuta yupo shuleni kwa hio kinachofuata mtamuelewa
 
Hakuna mwalimu mnyanyasaji bali wanafunzi ndio changamoto.
Ifikie hatua walimu wafundishe ya darasani wakimaliza haoooo.
Nashukuru nilisoma shule ambayo ni gvnt,walimu wanakuja kufundisha darasani,ukitaka uingie ukitaka baki bwenini,fanya kila unaloweza uhuru kama wote mwisho wa siku kila mtu alivuna alichokipilanda na kila mbuzi alikula kwa urefu wa kamba yake.
 
Kuna shule tuliendaga group ki kazi,mkuu wa shule akatuambia kuwa hawa wanafunzi ni majeuri hivyo msibishaneni nao,wanajifanya watoto wa mjini na nyie ni watoto wa mjini wakileta ujeuri achaneni nao watajijua wao na wazazi wao.


Toto likiwa jeuri achana nalo, fundisha pita hivi[emoji125],. Hakuna haha ya kushindana na majeuri coz watajuana wenyewe na mtihani wa mwisho.
 
Wamuache tu
Ni vile yeye tu kibao kimemuangukia
Ila kuna walimu wenzie wengi tu wanaotoa adhabu kali sana kuliko hata yeye.
Wamuache Ila apewe onyo matoto ya watu akae nayo mbali fundisha maliza sepa usianze kuleta malezi unawafanya watoto wa kwako yatakutokea puani siku hizi mtoto wa mtu sio wako we mpe elimu akachukua sawa asipochukua basi atafundishwa kwao
 
Kweli kabisa,unawaacha wafanye watakavyo.
 
Azaboy Mambo vp?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Wamuache Ila apewe onyo matoto ya watu akae nayo mbali fundisha maliza sepa usianze kuleta malezi unawafanya watoto wa kwako yatakutokea puani siku hizi mtoto wa mtu sio wako we mpe elimu akachukua sawa asipochukua basi atafundishwa kwao
Yah
Anatakiwa akae nao mbali maana wanafunzi huwa wanakera
Ukiutumia hasira unajikuta unaishiq pabaya.

Yeye atekeleze jukumu lake la kuwafundisha,Mtoto asipotaka kusikiza shauri yake.
 
Hapo wamefanya Makusudi wamkomoe mwalimu hiki kizazi sio kabisa
 
Kabisaa yaan
 
Sahihi kabisa mkuu,mambo mengine ni level ya kamati ya nidhamu ya shule...eti mkuu wa mkoa. Surely hizi siasa zimetuletea viongozi wajinga sana. Kwamba mkoani katatua shida zote imebaki hiyo ya wanafunzi? Upuuzi mtupu
 
Sema kesi za wanawake ngumu sana kuziamua... Usikute hapo mwalimu na wanafunzi walianza kusutana baada ya wote kuwa emotional. Mwanamke akiamua kuwa katili huwa ni hatari ya kifo. Ninamshauri huyo mwalimu apunguze unoko kufuatilia fuatilia wanafunzi. Hata sisi tukiwa O-level kuna mwalimu alikuwa akija kila siku saa 11 alfajiri na kiboko kutuamsha.. Akifungua tu mlango anakimbilia kuwasha taa huku kashika kiboko na kukimbilia kutucharaza viboko. Yaani kwenye kuwasha taa na kuanza kutuchapa ni kitendo cha kufumba na kufumbua. Mkono mmoja umeshika swichi mwingine umeshaanza kuchapa... Baada ya kutafakari kwa kina tukaona tuifungue swichi na kuacha zile nyaya wazi. Kesho yake mwalimu kaja kama kawaida na spidi zake kilichomkuta hatakaa asahau hata kwenye maisha baada ya kifo. Na sisi pia kilichotukuta kwa wiki nzima hatutakaa tusahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…