Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

Uko sahihi kabisa Mkuu Wangu
Isipokua Huyo Matron( Mwalimu na Mlezi wa kike) katoa Adhabu Kali sana Kwa hao wanafunzi.
Kuna Adhabu nyingi Sana ukizingatia na kosa , mazingira ya husika.
Matron kavuka kiwango ( Scale) kaingia kwenye Body and mental torture.
..... Walimu stop being Saddist.
Nakubaliana kabisa na wewe. Adhabu zinazotolewa na Walimu ktk shule hii haziendani na kosa.
Jumamosi iliyopita kuna wanafunzi walikutwa bwenini; muda ambao walitakiwa kuwa darasani kujisomea (saa 10 alfajiri hadi saa 5 asubuhi). Adhabu waliyopewa ni kufukuzwa shule. Mbaya zaidi wamefukuzwa bila hata taarifa kwa wazazi. Watoto wakajikuta wanazagaa Mbeya mjini kutafuta msaada.
 
Mwalimu ajulikanaye kwa jina la Sabina Haule amewapa adhabu wanafunzi wake wa shule ya msingi kwa kuwafungia darasani usiku kucha wakipigwa na baridi huku yeye akienda kulala nyumbani na mume wake. Adhabu hii imedumu kwa muda sasa hadi pale wazazi walipoenda kulalamika kwa mkuu wa mkoa, ndugu Homela.

Baaada ya wazazi kumpa taarifa RC alifanya ziara ya kushtuka shuleni hapo usiku wa manane ambapo aliwakuta wanafunzi hao wakipigwa baridi huku wakiwa hawana blanketi za kujifunika wala nguo za kuwakinga na baridi. Ndipo mkuu wa mkoa alipochukua jukumu la kuvunja mlango na kuwakoa wanafunzi waliokuwa wakitetemeka kwa baridi kali ya usiku.

Kufuatia tukio hili, RC amewaomba wanafunzi kuwa na nidhamu kwa walimu huku akiahidi kumshughulikia mwalimu aliyehusika na tukio hili hasa ukizingatia wanafunzi waliolazwa darasani bado ni watoto wadogo. Aidha, aliwashauri walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni. Ikumbukwe wiki iliyopita mwalimu mmoja alitiwa mbaroni mkoani humo kwa kuwachomeka mimba wanafunzi wawili huku akimchomoa mimba mmoja wao.

Chanzo: RFA; habari na matukio 13/07/2023

MAONI YANGU
Hili liwe fundisho kwa wanafunzi wenye tabia mbaya na wasiowaheshimu walimu. Wanafunzi wa kizazi hiki wana vichwa vigumu sana. Hawasikii. Hii inatokana na malezi mabovu kutoka kwa wazazi na jamii inayowazunguka. Wazazi tuongeze juhudi za kuwalea watoto wetu kuwa na nidhamu ya kuwaheshimu walimu na watu wengine katika jamii.

Nawasilisha.
Tatizo lipo Kwa walimu,umepelekwa kufundisha Sasa iweje ujiongezee majukumu meeeeengi badalabya kwenda kufanya issues zako ujiongezee kipato, serikali hainaga shukurani unaweza jitoa sana ukafaurisha sana but one mistake inakuwa mfano
 
Ndio maana nilikataa kazi ya ualimu tangu nasoma maana ni kazi ya kitumwa.

Just imagine huyo mwalimu saiv anavyohaha kwa kitendo alichodhani ni sahihi kukifanya.

Ualimu ni wito, mlioitwa nendeni mkaihudumie jamii kwa utumishi uliotukuka.

Mimi ningeua watoto wa watu.
Mi ni mwalim,huwezi nikuta nafanya ujinga kama huo zangu pindi tu mda wa KAZI ukiisha sitaki kujuana na mwanafunzi naenda zangu kutafuta mia mbili miambili kitaa,Over!
 
Tatizo lipo Kwa walimu,umepelekwa kufundisha Sasa iweje ujiongezee majukumu meeeeengi badalabya kwenda kufanya issues zako ujiongezee kipato, serikali hainaga shukurani unaweza jitoa sana ukafaurisha sana but one mistake inakuwa mfano
Kweli kabisa kiongozi. Suala la nidhamu tuwaachie wazazi; walimu wajikite kwenye ufundishaji tu.
 
Naona RC wa amekuwa kama mwalimy mkuu wa shule za Mbeya...
 
Nakubaliana kabisa na wewe. Adhabu zinazotolewa na Walimu ktk shule hii haziendani na kosa.
Jumamosi iliyopita kuna wanafunzi walikutwa bwenini; muda ambao walitakiwa kuwa darasani kujisomea (saa 10 alfajiri hadi saa 5 asubuhi). Adhabu waliyopewa ni kufukuzwa shule. Mbaya zaidi wamefukuzwa bila hata taarifa kwa wazazi. Watoto wakajikuta wanazagaa Mbeya mjini kutafuta msaada.
Balaa yani Tit for tat.
 
A
Loleza girls ina manyanyaso sana toka miaka hiyo,
HayajaAnza leo.
Kuna muda mwalimu anamkalisha mtoto nje asbh mpaka jioni kwenye mvua aiseee ni unyama.

Naongea nikiwa na uhakika wa kutosha,, I've been there for yrs.
U na wewe mkorofi?
 
"Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal. Mkuu Betiseba Nsemwa".

Huyu Maza ndo aliletwa huku daah tulimkimbiza Kiwanja High School,Chunya ana ubaya wa hatari.
 
Aisee pole kwake.
Hizi shule za seminary huwa wako serious kusimamia basi itakuwa ilitokea bahati mbaya tu.
Ahsante Wee nilimuia sana Mimi bwana sipendi uonevu kabisaa, mbayaa si unajua Ile pre form 1 Sasa hv wamepunguza na anajua pia kujitetea kashakua mkubwa
 
Kuna mwanafunzi kamaliza miaka 3 iloyopita ananiambia mwl alikuwa anawa amsha sa 11 asubuhi wafanye usafi, wakimaliza anarudia kukagua alikuwa anawapiga kama sio watu.

Sasa hapo alikuwa bado hajaolewa, akaolewa akaachika na hana mtoto itakuwa stress zimeongezeka mara mbili, wamtafutie msaada asije tuulia watoto.

Kuna madam alikuwa mkali sanaa na roho mbaya juu, wanafunz walicho mfanyia hawezi sahau.
Na walimwambia, akabeba mimba alikaa bed rest miez karibu yote hospital na bado akakosa mtoto. Alirud mpole mbona ukali wote uliisha.

Loleza kama katabia hiv cha roho mbaya wana ambukizana, akiondoka hiyu anarithi mwingine
Na sijui kama adhabu ya matofali waliacha ,matofal elf 1 mtu mmoja adhabu gani hiyo
Aseehh....ndo maana kumbe ana shidaa
Ila walimu hizi stress zetu kutolea Kwa Wanafunzi ni shidaa...
Hyo shule iangaliwe Kwa jicho la tatu watakuja kuua Wanafunzi au siku Wanafunzi wataua mwl
 
Walimu hawa wanafunzi watawapa tabu sana, mind your business fundisha sepa achana nao watajijua.
Wakati nasoma Kuna ticha alikuwa hajishughulishi na mwanafunzi yoyote, alikuwa anasema kazi yake ni kufundisha na kusahihisha kazi za somo analofundisha tu. Hawa wanafunzi unatakiwa kuwaacha kama walivyo ili yasijekutokea usiyoyadhania. Siku hizi ndio nimeanza kumuelewa yule ticha .
 
Ahsante Wee nilimuia sana Mimi bwana sipendi uonevu kabisaa, mbayaa si unajua Ile pre form 1 Sasa hv wamepunguza na anajua pia kujitetea kashakua mkubwa
Kwa kweli haipendezi kumuonea mtoto kupita kiasi.
Hata akikosea basi mpe adhabu ambayo ungempa mwanao wa kumzaa.

Siyo ndio unakomesha Mtoto aisee kama vita [emoji1787][emoji1787]
 
Kwa kweli haipendezi kumuonea mtoto kupita kiasi.
Hata akikosea basi mpe adhabu ambayo ungempa mwanao wa kumzaa.

Siyo ndio unakomesha Mtoto aisee kama vita [emoji1787][emoji1787]
Yaani walimu Baadhi Wana act kama wanajeshi wa quantanamo bay,ukatili tu au km hawajazaaa ,utadhani wako na wake wenzao au waume wenzao...it is scary kwa kweli
 
Back
Top Bottom