Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi

efb19a95-bc49-4f88-8e47-d3944f8e6633.jpg

Wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na funguo za bwenini kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kupitia vyanzo vyake vya taarifa anasema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.
cdfb1c4e-90b0-499f-9d8a-f908fee6afc2.jpg

Homera ameeleza kukerwa na tukio hilo kwenye shule ya Loleza anayosema ni ya mfano ikikusanya watoto kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo hata kama watoto walifanya kosa ilifaa kupewa adhabu walizojiwekea shuleni hapo na si kuwalaza darasani ikizingatiwa na musimu huu wa baridi.

Mwalimu anayedaiwa kuondoka na funguo za bweni ambaye ni msimamizi wa watoto hao bwenini Sabina Haule anasema chanzo ni ukorofi wa watoto hao lakini hakuwaamuru kwenda kulala darasani kwakuwa baada ya kufunga bweni alirudi baadaye majira ya saa nne usiku na kuwaelekeza kwenda kulala mabweni mengine ambayo hayana wanafunzi lakini watoto hao walikaidi na kwenda kulala darasani kimyakimya hivyo kuomba msamaha kwa mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal.mkuu Betiseba Nsemwa alipoulizwa juu ya suala hilo amesema.
2671df1f-6e32-4121-a19d-61c27a3ced4d.jpg

Hata hivyo Mkuu wa mkoa, alipata nafasi ya kutembelea hadi darasa ambalo wanafunzi wanadaiwa kulala usiku kisha kuzungumza na wanafunzi hao akiwaasa kuzingatia nidhamu wawapo masomoni na kumuagiza Afisa Elimu Mkoa Mwl. Ernest Hinjo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwalimu husika.
 
Kuna siku nilimsikia binti yangu wa Standard Two akisema mwalimu wake hana akili. Aisee, nilimwambia atubu na akamwombe msamaha mwalimu wake. Kama mwalimu hana akili, maana yake na mwanafunzi hana akili. Akaleta mambo ya "Why, why, dad?" Nikasema, "Mkubwa akikosea, unamwambia kwa heshima. Huwezi pwayuka kuwa mwalimu hana akili. Jifunze kupuuzia wajinga na kujifunza kuacha kufanya ujinga kimya-kimya, and not shouting 'mwalimu hana akili.' Tabia mbaya za kijeuri nyingine zinaendelezwa na wazazi."
Wewe ni mzazi bora sana
 
Kama hawatak adhabu kali waache kufanya makosa
Tena wangetundika miguu juu ukutan kichwa chini matako nje

Tatizo wanawake mnajiona special sana na huu upumbavu wenu mnaleta hadi kwenye ndoa na jamii kiujumla

Ukiwa na adabu huwez kupata adhabu za kihun

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mwanamke ni kiumbe dhaifu[emoji1787]
We are special Mkuu. Mungu alituumba baada ya kuwa amekamilisha kila kitu.,sisi ni malastborn wa Mungu.
Kutundika miguu juu watoto wa mjini hawawezi elewa.
Hii haina mbabe.
 
"Mwl wa mase hapa ni wapi..." huu msemo tu unatosha kuachana na wanafunzi kazuge shule saa nne nenda chini ya mti vuta fegi yako mwisho wa mwezi kapokee salary kale na familia yako
 
Ni kweli wanafunzi wengine ni wake za watu kwani walishaingia kwenye mahusiano ya kingono.
Hivyo kuwafuga hakuna tofauti na kufuga kunguru.
Kidato cha 6 ni watu wazima tena mikoani wanachelewa kuanza shule unakuta form 6 ana miaka hadi 24 kumfuga kama mfungwa ni upuuzi.
 
View attachment 2686526
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na dhamu dhidi ya mwalimu husika.

JAMBO TV
Kwa nini wanafunzi wa form 6 wanaitwa WATOTO!! watu wako above 18 years siyo watoto hata kidogo wanatakiwa waheshimiwe.
 
View attachment 2686526
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na funguo za bwenini kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kupitia vyanzo vyake vya taarifa anasema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.

Homera ameeleza kukerwa na tukio hilo kwenye shule ya Loleza anayosema ni ya mfano ikikusanya watoto kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo hata kama watoto walifanya kosa ilifaa kupewa adhabu walizojiwekea shuleni hapo na si kuwalaza darasani ikizingatiwa na musimu huu wa baridi.

Mwalimu anayedaiwa kuondoka na funguo za bweni ambaye ni msimamizi wa watoto hao bwenini Sabina Haule anasema chanzo ni ukorofi wa watoto hao lakini hakuwaamuru kwenda kulala darasani kwakuwa baada ya kufunga bweni alirudi baadaye majira ya saa nne usiku na kuwaelekeza kwenda kulala mabweni mengine ambayo hayana wanafunzi lakini watoto hao walikaidi na kwenda kulala darasani kimyakimya hivyo kuomba msamaha kwa mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal. Mkuu Betiseba Nsemwa alipoulizwa juu ya suala hilo amesema alikuwa akiendelea kushughulikia suala hilo kwa kuwakutanisha mwalimu wa nidhamu na msimamizi huyo wa bweni.

Baadaye mkuu wa mkoa Juma Zubery Homera akapata nafasi ya kutembelea hadi darasa ambalo wanafunzi wanadaiwa kulala usiku mzima kisha kuzungumza na wanafunzi hao akiwaasa kuzingatia nidhamu wawapo masomoni na kumuagiza afisa elimu mkoa Mwalimu Ernest Hinjo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwalimu husika.

JAMBO TV
Homera nae hana dogo anaacha kuhangaika na mambo makubwa ya msingi anahangaika na mambo ya kipuuzi puuzi ambayo mengine yanaishia kumfedhehesha kama lile la PANDAHILL

matokeo yake ili kuficha aibu wanaamua kutengeneza kosa ili kosa liwepo mambo mengine ni yakumaliza tu wala hakuna haja ya kuhangaika na waandishi wa habari kila kukicha kufuatilia walimu na wanafunzi
 
Maadili yameporomoka sana. Hawa wanasiasa mara nyingi hawana ku balance changamoto wao huegemea upande wa wanafunzi hata kama wenyewe ndio wakorofi.
 
Maadili yameporomoka sana. Hawa wanasiasa mara nyingi hawana ku balance changamoto wao huegemea upande wa wanafunzi hata kama wenyewe ndio wakorofi.
Homera nimemdharau sana reasoning yake ndogo sana kwenye maswala ya kijamii
 
Huyo homela inaonekana ni mtu wa totoz sana jamaa kila siku misala yake ya mademu tu kama ana uchungu sana awasemee na wavulana hebu deal na mambo ya msingi braza hizi kiki nyngn muwe mnaziangalia kwa makini
 
Kwa hiyo wanafunzi kulala darasani nyie mnaona ni sawa?Siku nzima mtu yupo darasani,baadae jioni ale,kisha usiku preparation time,baada ya preparation time mtu kaondoka na funguo ili iweje?Kesho tena huyu huyu mwanafunzi aamke mapema kujiandaa,usafi nk.Adhabu zipo nyingi ila sio ya kuondoka na funguo,Wewe mtu mzima na akili zako upo nyumbani umerelax watoto wa watu umewafungia wasilale kama sio ujinga ni nini hiki.Mimi nimesoma shule za bweni nikisikia mtu anafanya hivyo nashangaa
 
Back
Top Bottom