Msanii Sifa Bujune ambaye aliswekwa rumande kwa maelezo kwamba, wimbo wake umejaa Uchochezi , na kwamba angeburuzwa mahakamani kwa uchochezi wake huo, leo amefikishwa mahakamani, baada ya shinikizo la Wanasheria kutaka aachiliwe ama afunguliwe mashtaka.
Bali kinyume na madai ya RPC wa Mbeya ambaye alimpa Bujune kesi ya Uchochezi, Msanii huyo ameshitakiwa kwa makosa ya
kusambaza taarifa za uongo, Ajabu!
Hii maana yake ni kwamba RPC wa Mbeya ni Muongo na hafai kuendelea kuwa mtumishi wa jeshi la polisi, Napendekeza Afukuzwe kazi haraka na akamatwe.