Mbeya na Kanda ya Ziwa ziwe semi-autonomous kama Zanzibar!


Weka na taja basi pia na Wilaya na Halmashauri za Mikoa mingine iliyotajiri kwa maana umetaja Kanda ya Ziwa na kusema ni masikini wa kutupwa weka tulinganishe usisahahu Kahama (ni KZ pia) ni moja kati ya Wilaya inayoongoza kwa mapato Tanzania na imezidi Mikoa mingi sana Tanzania!
 
Mnajua lkn mnachoongea? Mikoa ambayo haofikishi hata 2% ya mchango wa kodi katika Taifa ndjo ijitenge? Kwani wafanyakazi wanaotoa huduma katika hiyo mikoa mnalipa ninyi?
Suala la kulipa wafanyakazi..sidhani kama litakuwa tatizo rasilmali zipo za kutosha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nilijua utataja Kahama, nitajie na nyingine yenye mapato makubwa. Mmeanza mambo haya ya hovyo baada ya Magu kuwa Rais. Watanzania wanajua mwendazake akiwaharibu sana akili zenu na mlivyo washamba mkamwamini.
 
Ukutaka kujua wilaya yenye mapato makubwa ushahidi wa kwanza itakuwa na halmashauri zaidi ya moja. kwa hyo kanda yenu nu Kahama, Tarime na Bunda tu. Tena 2 ziko Mara ambao hawana sifa za kishamba km wasukuma. Hata wilaya za mkoa Kilimanjaro bado zina mapato madogo hakuna hata wilaya moja ina halamashauri 2 lakini ukija kwenye sifa za kijinga watakuambia Kilimanjaro tumeendelea sana. Nchi hii sasa hivi kuna makabila mawili kwenye mitandao sijui wamelogwa na nani. Ni sifa za uwongo na za kijinga.
 
Nilijua utataja Kahama, nitajie na nyingine yenye mapato makubwa. Mmeanza mambo haya ya hovyo baada ya Magu kuwa Rais. Watanzania wanajua mwendazake akiwaharibu sana akili zenu na mlivyo washamba mkamwamini.

Mimi ningependa sehemu yoyote kwenye rasimali basi asilimia fulani ibakie hapo hapo na siyo kuchukuwa yote na kwenda kufanyia anasa Dubai au USA, mara sijui kucheza cinema na ujinga kama huo, kama ni Gesi inatoka MT basi asilimia ibakie hapo Mtwara kama ni Ml.Kili unaleta Watalii basi asilimia fulani ibakie kwa watu wa eneo hilo kama ni Makaa ya Mawe huko Ziwa Nyasa basi pia asilimia ibakie huko, …
 

Mimi siko huko unakodhania wewe, ningependelea rasilimali zisaidie eneo ambalo zinapatikana, kama ni Tanzanite isaidie watu wa huko iliko na siyo kuchukuwa fedha yote kupeleka sehemu moja na kuifuja!
 
Tuanzishe serikali za majimbo kila sehemu ifaidi rasilimali zake, huku kanda ya ziwa tuna kila kitu lakini cha kushangaza ata maji tu wananchi hawapati na ziwa lipo mlangoni, pia miundombinu ndio ovyo kabisa, kila kitu kinapelekwa mikoa ya pwani na dar. TUNAITAJI SERIKALI ZA MAJIMBO KILA KANDA IFAIDI RASILIMALI ZAKE.
 
Atakuja kwa vile kuna uchaguzi mbele kama sio hivyo sidhani
 
Mimi siko huko unakodhania wewe, ningependelea rasilimali zisaidie eneo ambalo zinapatikana, kama ni Tanzanite isaidie watu wa huko iliko na siyo kuchukuwa fedha yote kupeleka sehemu moja na kuifuja!
Hii nchi ni moja, alituasa baba wa Taifa kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Wizara ya Elimu ni moja, wizara ya afya ni moja rasilimali zikibaki ilipo wizara itahudumiaje nchi nzima? Hayo mawazo yenu hayawezekani huo ni uhaini. Hakuna eneo ktk uso wa hii dunia haina rasilimali labda tu bado hatujaweza kuigundua au kuitumia. Tusimkosoe Mungu. Usije kuona penye dhahabu ndiyo pa maana ni kwa leo tu na hata hivyo itakuja kuisha. Dodoma watu wanaisema vibaya kumbe chini imejaa Uranium. Kule ziwa Eyasi Karatu mkoani Arusha kuna Nickel nyingi sana. Kila sehemu nchi hii ina utajiri wake siyo kusema sehemu fulani inanyonywa hakuna kitu km hicho. Tujivunie kuwa na nchi moja imara siyo kuzungumzia kuigawa sijui ktk nini.
 
Una hakika huyo nyerere alikuwa sio mkabila na mdini fuatilia huyo alikuwa mdini sana ndo kaharibu balance imeanza kwa magufuli ndo alikuwa na hakk sawa ila sio nyerer na wengine
 

Kama umenisoma vizuri nimesema asilimia fulani inabie eneo lenye rasilimali na siyo 100% , hata tu ukibakiza 10% ingekuwa vizuri sana na maeneo mengi ya nchi yangeweza kuendelea.

Labda nikuulize, unaona ni sawa mfano mtoto atoke Musoma au labda Tunduru asafiri mpaka Dar kufwata tu cheti cha kuzaliwa kwa mfano ? Huo ni mfano mdogo sana sijaongelea wastaafu ambao wanalazimika kusafiri kuja Dar kufwatilia tu mafao yao, unaona ni sawa ?
 
Kila kitu kinakimbilia Dar na watu wanakimbilia Dar kwa kufuata huduma bora kjnachofuata ni kuiangaisha serikali kuweka miundombinu bora.Ukiangalia kwa makini tatizo walilitengeneza wenyewe.
 
Naona sukuma gang mnataka kuigawa nchi kwa ujinga wenu
 
Kwa nini usiwepo utawala wa majimbo (states) kama USA? Kila kanda itumie rasilimali zake, iwe na utawala wake na sheria zake alafu ndo kuwe na serikali ya shirikisho? Haya mambo ya mikoa naona kuna kanda zinanyonywa especially kanda ya ziwa[emoji35]
sema tungekua tunachagua wakuu wa mikoa na wilaya, ili kila watu wachague mtu wao wa kuwaongoza!

nchi yetu kimsingi imegawanywa kwenye majimbo (mikoa) na wilaya, ni kiasi cha kuruhusu kila wilaya na kila mkoa uchague hao watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…