Hii mambo ya huyu kijana ni hatari sana, yaani huyu ni wa kumuwahi kabla jua halijazama, moto huwa unaanza kama hivi baadae wajinga wakiunga tela moto hauzimiki kama Kenya hakukaliki hivi sasa wanamtaka Ruto asepe na watu wanauwawa ,
Huyu kijana ni mgonjwa wa akili anastahili faili jipya Mirembe na apewe shamba kubwa, afungwe plau alimishwe kama ng'ombe!! Hatakiwi kuonekana hadharani tena ili asipate wafuasi. Amani ni kitu adhimu Sana. Ikipotea huwa hairudi tena.
Katika namna bora ya kupinga viongozi ni kama hii ya kuwa na id feki jf, unakaa nyuma ya keyboard na kuporomosha makombora, kujinadi kwa masifa namna ile unamkashifu kiongozi wa nchi tena ni Maza ni hatari mno na si kitu kizuri, itakuwa kijana kachoka kula pilau kuku na sasa anataka akale jela ugali unaofanana na uji na maharage ya mwaka 1990 yenye harufu ya magunia!!
Ila pia ni vizuri sana ku study ujumbe wake na kuufanyia kazi, kisaikolojia inaonesha kijana ana grievances nyingi kwa Mh Rais mpaka amepata ujasiri wa kujilipua kwa kuchoma picha ya Rais hadharani na kumualika nyumbani kwake!! Huyu anawakilisha kundi kubwa la vijana ambao wana majanga yao hawana pa kuyasemea!!