Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watanganyika ndio kina nani? Mali zipi zilizouzwa? Yeye binafsi na mtu mmja anawezaje kuuza Mali za Watanganyika? Mnakuwa hamna akili au?
Sasa hapa nani hana akili 😃

Kwahiyo Watanganyika na Wazanzibar huwajui?
 
Hii mambo ya huyu kijana ni hatari sana, yaani huyu ni wa kumuwahi kabla jua halijazama, moto huwa unaanza kama hivi baadae wajinga wakiunga tela moto hauzimiki kama Kenya hakukaliki hivi sasa wanamtaka Ruto asepe na watu wanauwawa ,

Huyu kijana ni mgonjwa wa akili anastahili faili jipya Mirembe na apewe shamba kubwa, afungwe plau alimishwe kama ng'ombe!! Hatakiwi kuonekana hadharani tena ili asipate wafuasi. Amani ni kitu adhimu Sana. Ikipotea huwa hairudi tena.

Katika namna bora ya kupinga viongozi ni kama hii ya kuwa na id feki jf, unakaa nyuma ya keyboard na kuporomosha makombora, kujinadi kwa masifa namna ile unamkashifu kiongozi wa nchi tena ni Maza ni hatari mno na si kitu kizuri, itakuwa kijana kachoka kula pilau kuku na sasa anataka akale jela ugali unaofanana na uji na maharage ya mwaka 1990 yenye harufu ya magunia!!

Ila pia ni vizuri sana ku study ujumbe wake na kuufanyia kazi, kisaikolojia inaonesha kijana ana grievances nyingi kwa Mh Rais mpaka amepata ujasiri wa kujilipua kwa kuchoma picha ya Rais hadharani na kumualika nyumbani kwake!! Huyu anawakilisha kundi kubwa la vijana ambao wana majanga yao hawana pa kuyasemea!!
 
Umewaza kipumbavu , kichawa. Ukikaa ukapata akili utagundua hamna kosa alilofanya. Rais si Mungu. Ni binadam wa kawaida kabisa. Amevunja sheria gani kwa kuchoma picha ambayo ni mali yake ameona ni takataka? Mi nimechoma sana hayo mapicha.
Mmmmmmh, mm naumia tu nimeitwa elfu mbili wakati nanunua umeme
 
Naomba kujua huyo unaemuita rais alichaguliwa lini na aligombea na akina nani hadi akaibuka mshindi.?
 
Yule sio Rais Bali picha yenye sura ya Rais au picha yenye sura ya Rais imekuwa nyara ya serikali siku hizi?
Ni ujinga tuu wa kutozingatia Mambo ya msingi na kutafuta milage za kipuuzi namna hiyo....viongozi wetu wana Mambo ya ajabu Sana Hilo nalo lakutolea taarifa, picha kuchomwa imedhalilisha nini au mtu gani? Kwa hiyo Dr mwenye cheo kikubwa kuliko raisi utu wake umeshuka.

Naamini Homera anajiona mpuuzi Kwa Jambo Hilo akikaa chumbani kwake akitulia 😅
 
aloo mimi nilijua ni ile official potrait kumbe kaprint mwenyewe kwa epson yake apo labda kibabe tu ila mwambo yuko sahihi
 
Kakamatwa faster

Vp waliyompiga na kumtesa SATIVA wamedakwa pia

Ova
 
Kiukweli sioni ubaya wa samia kabisa ukimfananisha na magufuli yani sijui watanzania wanataka nini? Kiukweli siasa za mama ni nzuri sana ukilinganisha na mtangulizi wake aliekuwa anauwa watu hovyo.
 
Back
Top Bottom