Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa Kosa lake liko wapi, mnampa mtu attention asiyo stahili , Fanyeni shughuli nyingine
 
Kijana ameshakamatwa, Ukitukana viongozi utakamatwa ndani ya 24 hrs ila watekaji na mafisadi haawajulikani
 
Angeweźa kuchoma kimya kimya, lakini amechoma huku akijigamba na kajirekoi. Huyu lazima afike mbele ya Hakimu akakabiliane na shataka lake
 
Heshima ni lazima Kwa tafsiri yeyote uijiayo wewe au Ile ya kwenye kamisi.
Kama ni hiyo hiyo, kamwe siwezi kuheshimu mtu yeyote, hata awe kiongozi wa kiasi gani, kama kiongozi huyo haheshimu anaowaongoza.
Sasa najua hapa kwa akili yako ndogo utaanza ubishi, na kudai ushahidi, kana kwamba matendo yanayoonekana siyo ushahidi tosha.

Siwezi kuwa na mjadala wa maana na mtu kama wewe aliye jitoa akili na heshima ya utu wake, na kuwa kama mwanasesele tu.
 
Nani haheshimu anaowaongoza?
 
Huyo atakuwa Mental case wakampime. Hakuna mtu mwenye akili timamu atafanya upumbavu wa aina hiyo
 
kama amekosea, wamkamate, wampeleke mahakamani, wasimteke.kutekana huko kuna siku watu wataingia mtaani msijelaumu. kama kuna TISS wamshauri Rais akataze matendo yanayoongeza chuki mioyoni mwa watu kwasababu kuna siku watachoka na kuamua lolote na liwe kama Kenya. najua mapolisi hawawezi kumshauri, ila TISS ndio kazi yenu.
 
Hiyo picha ni mali yake ana haki ya kuifanya atakavyo

Bendera za Israel na Marekani kila mara zinachomwa moto ndio sembuse chura kiziwi.

Yupo mwamba mpaka nakala za Qurani kapiga moto ni mali yake huwezi kumpangia.
Kumbe,sawasawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…