Kabla ya hii no reform no elections Kulikuwa Na movements ngapi nyuma na vp ziliweza kufanya kazi?
Zote zilifanya kazi vyema kabisa maana zimeifanya CCM izame deep zaidi kwenye kuiba uchaguzi wote na sio kura tena...
Sasa Ili kukomesha kabisa hilo, movement ya NO REFORMS, NO ELECTION ndiyo ya mwisho na Tanganyika na Zanzibar zinakwenda kukombolewa kutoka kwa mkoloni mweusi aitwaye CCM...
Aisee n kweli sio watu wote tumeumbwa ili tuwe viongozi ila Mm ningekuwa kiongozi wa chadema bc kila siku ningekuwa rumande mana nngeenda hatua kwa hatua na ccm yn jino kwa jino, ccm wametangaza wagombea wao kabla ya muda bc Mm hakuna kulalamika n mwendo wa kuchagua wagombea na Mm, ccm wanapiga kampeni kimya kimya na Mm naenda nao sambamba napiga kampeni kimya kimya n.k
Wewe tatizo lako ni ujinga ndio unakusimbua...
Utangaze kugombea kwenye uchaguzi upi? Huu unaojua kabisa kuwa unakwenda kuchinjwa hata kabla hujalisogelea sanduku la kura au kuenguliwa kwa kuwa eti hujui kusoma na kuandika? Yaani eti wewe
Mbaga Jr eti hujui kusoma, kuandika na kujaza fomu za kuomba kuteuliwa, really...?!
Mbaga Jr Acha ujinga...
Mbaga Jr Toka usingizini....
Mbaga Jr Pigania kwanza mifumo ya
usawa,
haki na
uwazi ktk chaguzi zetu ili uwe na uhakika kuwa ukiwa mgombea unaenda kushindana kwenye sanduku la kura...!
Wewe
Mbaga Jr ni kipi hasa usichokielewa? Kwanini unaziweka akili na ufahamu wako rehani wewe...!!???
Tatizo lenu chadema nyie mnaendesha mambo yenu kwa kubembeleza system wakati wenye system wanaenda rafu afu mwisho wa siku mnataka huruma ya wananchi, hamuhamasishi wanachama wenu kujiandikisha afu mtakuja kuwaambia waandamane kupinga matokeo ya uchaguzi 😂
Kimsingi nakuona kabisa, you are sailing in the same boat na CHADEMA....
Movement ya No Reforms, No Election haibembelezi mtu wala hicho unachokiita "system" bali inashurutisha kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kikatiba Ili kuleta chaguzi Huru, za Wazi na za Haki kwa vyama na watu wote wanaoshiriki...
Kwa Sasa mambo hayako hivyo, kwa sababu, kwa mfano:
1. Unaingiaje kwenye uchaguzi ambao wewe mwenyewe unasema "wanachezewa rafu" na mpinzani wao kwa sababu sheria, kanuni na taratibu zote za mchezo (uchaguzi) zinampendelea yeye...?
2. Ili kurekebisha hili, unadhani utafanya nini ili kupata uwanja ulio sawa wa mchezo? Bila shaka ni kipigania mabadiliko ya kisheria, kikatiba, kikanuni na taratibu za uchaguzi kwanza...
3. Kama utajibu maswali hayo👆👆vizuri na kwa ufasaha, basi itakuwa umeelewa maana ya movement ya NO REFORMS, NO ELECTION...
##Tunataka chaguzi za kweli, za haki, za wazi zinasimamiwa na sheria na kanuni zisizompendelea awaye yeyote...
##Mabadiliko haya hayawezi kuletwa na watu kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura ambalo hata huwezi kuliona zaidi ya yule anayejishindisha uchaguzi mwenyewe...
##Aidha Moja ya taasisi inayotakiwa kufanyiwa mabadiliko ni hii inayojifanya kuandikisha wapiga kura wakati kinachofanyika ni uchafu na usanii mtupu...!