MBEZI: Rais Magufuli azindua kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani

MBEZI: Rais Magufuli azindua kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani

Kuzinduliwa na kufunguliwa ni kitu kimoja ?tuanzie apo
Kuzindua na kufungua vyote ni sawa yaani kurasimisha matumizi.
Kufungua ni neno la zamani zaidi na lilitumika sana baada ya uhuru.

Kuzindua ni neno jipya kutokana na kukua kwa lugha ya kiswahili.
 
Kuzinduliwa na kufunguliwa ni kitu kimoja ?tuanzie apo
Leo kinazinduliwa na kesho ndy kinafunguliaa rasmi kwa kuanza shughuli za usafirishaji. So unaweza ukazindua lakin kisifunguliwe au ukazindua na kufungulia hapohapo
 
Ni vigumu sana kupambana na hii kitu, tumtangulize Muumba na kutumia virutubishi kuongeza kinga.Hakika upo na tutaishi nao kwa kinga za mwili.
 
CCM WALIKUWA WANAFURAHIA KULIKAMATA JIJI LA DAR ES SALAAM LAKINI NAONA SASA WANALIVUNJA JIJI
 
itapendeza kuboresha vituo vya mikoa mingine vikaribie hadhi ya kituo cha Dar es Salaam na Dodoma.

Uboreshaji uwe endelevu
hapana sio vituo vyote nchini, kinachofuata kwa maboresho ni chatoo!.
 
1614163004802.png

Huyo binti mwenye pensi na Tshirt ya kijani anaoneshwa kwa kurudiwarudiwa sana na kituo kinachorusha matangazo yaelekea camera man anavutiwa naye
 
Tuwekeeni updates na sisi tulio huku mbwinde tujue kunachojiri...
 
Hiki kituo sio kwamba kiliwahi kuzinduliwa kipindi cha campaign? Au kwa sababu nimekua offline labda sijasikia vizuri?
Vikiisha vya kuzindua huwa wanarudia. Kwani wewe hujui kule Mwanza na Singida vilizinduliwa viwanda ambavyo tayari vinafanya kazi kwa zaidi ya miaka 5 iliyopita?

Hujui barabara ya Dodoma to Iringa, Msata to Bagamoyo, ambazo Ni miongoni mwa barabara 7 zilizofunguliwa na JK mwaka 2012, zilifunguliwa tena mwaka 2018?

Subiria kufunuliwa tena kwa flyover ya TAZARA.
 
Akili mbovu kabisa kila kitu eti mfano Marekani nk.... huwezi ata jisifia kutoa mifano hai ya waafrika wenzanko tabia hii hua inanikwaza sana kila kitu mzungu, mzungu .........................
South Africa ni Wazungu kumbe?
 
CCM WALIKUWA WANAFURAHIA KULIKAMATA JIJI LA DAR ES SALAAM LAKINI NAONA SASA WANALIVUNJA JIJI

Machinga, bodaboda, mama lishe lazima wawepo ndani ya stendi lakini madalali hawaruhusiwi...wamachinga 1 (simba) na jiji 0 (waarabu)
 
Baada ya kufungua daraja la juu la Kijazi sasa Rais Magufuli amewasili Kituo kikuu kipya cha mabasi ya mikoani tayari kabisa kwa kukifungua rasmi.

Watu ni wengi sana.

Up dates;

====

WAZIRI JAFO AAGIZA MKURUGENZI WA JIJI KUANDAA BANGO LA STENDI YA MAGUFULI

Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuandaa bango litakaloitambulisha Stendi ya Magufuli

Jafo amesema hayo katika uzinduzi wa Stendi mpya ya mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani iliyoko Mbezi Luis

Pia, amemuomba radhi Rais Magufuli kwa kutumia jina lake kwenye stendi hiyo kabla ya kumuomba ridhaa

BAADHI YA ALIYOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI:

Maendeleo hayana chama, lakini lazima kuwepo na chama kinachotoa maelekezo. Wananchi wa Kibamba hamkukosea, tembeeni kifua mbele

Sifurahii sana majina yangu kutumika kwenye vitu namna hii. Kwa sababu mnaweza kuita Magufuli Stand, halafu Wamachinga na Mamalishe wakawa wananyanyaswa hapa

Nitaumia sana kama Wananchi hawa wanyonge watakuwa wanafukuzwa, halafu pameandikwa Magufuli. Maana yake itakuwa ni Magufuli anayewafukuza, kwa hiyo sitakubali

Katika stendi hii kuna vitu vingi vizuri ambavyo sijui kama watu wa kawaida wataingia. Kuna Hoteli ambayo sijui kama Machinga ataruhusiwa kuingia

Nakubali hii stendi kuitwa jina langu. Kwahiyo nataka stendi itakapoanza hawa Wamachinga wasifukuzwe kwa sababu ni kwao

Jengeni utaratibu kwa hawa wafanyabiashara ndogo ndogo ili mabasi yakiingia wanunue chakula kwa Mama Ntilie. Watakaokuwa na hela watanunua kwenye mahoteli lakini mihogo na matikiti maji yanunuliwe

Miaka 60 tangu tupate Uhuru hakujajengwa stendi nzuri kama hii. Miaka 60 baada ya Uhuru hakujajengwa 'flyovers' kama ile ya Ubungo. Ni lazima Watanzania mtembee kifua mbele

Najua hii ni 'challenge' kwa Viongozi, kwamba hapa tutafanyaje. Ni kazi ya Viongozi kutatua changamoto. Kwahiyo mjipange mpige bongo vichwa vyenu kujua hawa wengine ambao wameshalipa elfu 20 watafanyaje biashara zao hapa

Ile barabara ya njia nane tuliomba Wafadhili wakaturingia, nikamuita Mfugale nikamuuliza hatuwezi kujenga hii? Akasema tunaweza. Nikamwambia tengeneza njia nane ili hasira yangu iwapate kabisa

=====

RAIS MAGUFULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA, LAKINI LAZIMA KIWEPO CHAMA KINACHOTOA MAELEKEZO

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema unapokuwa Kiongozi, ni lazima upate watu wanaowakilisha watu kwakuwa bila 'connection' kazi haziendi

Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua stendi ya Mabasi ya Mbezi Luis ambayo imepewa jina la Magufuli Bus Terminal

Amesema, "Dar es Salaam karibu yote ilikuwa watoto wa jirani, sasa mmenizalia watoto asilia. Maendeleo hayana Chama lakini lazima kiwepo chama kinachotoa maelekezo"

View attachment 1710840

View attachment 1710841
Napendekeza hicho kituo kipewe jina la "Bakoa" au Nyungu
 
Nilifungua wamefuta..
Hii tuifungulie uzi wake mkuu. Nilimskia pia akiongelea hii nikabaki mdomo wazi.

Katka yote nimevutiwa na mbunge wa kibamba alivyopewa nafasi akaitumia vizuri kuyaelezea matatizo ya wananchi wake kwa njia inayompendeza mtukufu Jiwe.
 
Back
Top Bottom