MBEZI: Rais Magufuli azindua kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani

Nimefatilia sehemu hotuba, Bus terminal eti anafuraha sana, awali hawakuwepo wa kuomba( Wabunge upinzani) leo anaombwa kwa unyenyekevu mbuge Mtemvu. Kwamba Dar yote ni raha tupu.

Ushauri wangu kauli hizi za kibaguzi hazijengi taifa, ni bora awatumie ccm wabadili katiba, endapo ni kweli serikali ya wapinzani( mjumuisho) ilikwamisha maendeleo. Pia kauli miaka 60, kwanini hawakujenga stand kama hii? Ndege? Reli? Hizi kauli hazina afya kwa taifa.
 
Mzungu kakuzidi ndo maana ukaweza kua hapa jf otherwise ungekua unaandika kwenye makaratasi ambayo nayo yaliletwa na mzungu
Akili mbovu kabisa kila kitu eti mfano Marekani nk.... huwezi ata jisifia kutoa mifano hai ya waafrika wenzanko tabia hii hua inanikwaza sana kila kitu mzungu, mzungu .........................
 
Hivi kuna watu manatenga muda kumsikiliza Yamungu ?
 
Mbona hiki kituo cha mabus kinaonekana bado hakijakamilika..haraka zote za nn
 
Hio stand imepewa jina gani la swahiba Ili tuanze kujizoeza
 
Mbona hiki kituo cha mabus kinaonekana bado hakijakamilika..haraka zote za nn
Usishangae SGR Dar Moro ikafunguliwa mapema kwq demo kutest behewa kuacha legacy, phase 2 kitu SA hakina masihara.
 
ila mheshimiwa hajui kamari inayochezwa hapo kupata eneo la biashara ni mtihani mkubwa hapo ni shimo la RUSHWA hakika walio nacho wataongezewa hizo zabuni watashinda wakina bakrhessa, then kunakuwa na vipandikizi akina sisi eneo ni kubwa ni fursa kwa wajasiriamali but kama huwezi kumtoa adui MDUDU RUSHWA. hata korido ya kuuzia vocha hupati naomba viongozi waliangalie kwa mbali....japo nia kuu ni kuongeza mapato.
 
Hii tuifungulie uzi wake mkuu. Nilimskia pia akiongelea hii nikabaki mdomo wazi.

Katka yote nimevutiwa na mbunge wa kibamba alivyopewa nafasi akaitumia vizuri kuyaelezea matatizo ya wananchi wake kwa njia inayompendeza mtukufu Jiwe.
Ila kanyenyekea Sana.
 
Kauli hii ya mkuu wa nchi yetu ameitoa leo wakati anafanya ufunguzi rasmi wa stendi mpya ya mabasi ya mbezi mwisho ambayo kwa sasa inaitwa stendi ya Magufuli.

Huku akishangiliwa kwa furaha na akina mama na vijana ambao kwao sasa inaonekana kuwa ni fursa . Rais Magufuli ametoa agizo kwa waziri wa Tamisemi kuwa machinga na mamalishe waruhusiwe kufanya biashara kwenye stendi hiyo ili nao wanufaike.

Kwa sababu rais Magufuli amepewa jina la stendi hiyo na yeye hapendi kuona wanyonge wananyanyaswa ameagiza Waziri Jaffo kuhakikisha raia wanyonge wananufaika na mradi mkakati huu.

Stendi hii itakuwa inahudumia mabasi 3000 kwa siku hivyo abiria watakuwa wanahitaji chakula na kununua bidhaa muhimu. Kwa hiyo ni fursa kwa raia wanyonge hasa mamalishe na wamachinga.

My take; Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge na wanaoonewa, tumpongeze kwa hili.
 
KWA KAULI YA JPM,

Nawaskitikia sana
Waliochukua fremu za biashara ndani ya stend kwa gharama kubwa IMEKULA KWAO.

Machinga watauza bidhaa ile Ile kwenye kibaraza cha frem uliolipia mwenyewe,

Wateja hawataona umuhimu wa kuingia ndani ya frem lako,
Na watauziwa biadhaa ile ile kwa Bei ya chini zaidi,

na huna Cha kuwafanya kwasababu mweshimiwa tayari keshasema[emoji1]

MUHUDUMU[emoji1635], MITANO TENA TAFADHALI[emoji1]
 
Akili mbovu kabisa kila kitu eti mfano Marekani nk. Huwezi ata jisifia kutoa mifano hai ya waafrika wenzanko tabia hii hua inanikwaza sana kila kitu mzungu, mzungu.
Tatizo lako unatumia muda msingi sana kwenye korido za CCM Lumumba, ukienda mitaa ya Kinondoni utajua kuwa South Africa iko Afrika siyo Marekani wala Ulaya.
 
Mzee huyu!!! Kwani kituo kilianza wakati wa mbunge gani? Watu mna shangilia ujinga tuu.
 
Wabongo tujitahidi kuwa wasafi basi
Wakuangaliwa sana sana ni wamachinga na mama lishe...

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…