Mbinu gani ulitumia kuishi na kabila la wanguu? Moto wao sio mchezo!

Mbinu gani ulitumia kuishi na kabila la wanguu? Moto wao sio mchezo!

madam karibu kilindi ,gairo,kiteto uone wanavyo ogopwa
Wangulu (au Wanguu) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi mipakani mwa mikoa minne ya Tanga, Dodoma, Manyara na Morogoro, hasa upande wa Kusini-Magharibi mwa mkoa wa Tanga ambako sasa ni wilaya ya Kilindi na upande wa Kaskazini-Mashariki mwa mkoa wa Morogoro ambako sasa ni wilaya ya Mvomero na milima ya Nguu. Upande wa Magharibi ni mkoa wa Manyara ambayo sasa ni wilaya ya Kiteto.

Masimulizi ya kale ya Mbega na Kimweri yanasema kuwa kabila la Wanguu ndilo kabila mama la makabila ya Wazigua, Wabondei, Wasambaa, Waluvu na Wakilindi, ambapo makabila hayo yanaendeleza mila na desturi za asili moja na katika umoja huo hujulikana pia kwa jina moja la Waseuta. Kwa asili Wanguu ni wafugaji na wakulima.

Mwaka 2009 walikuwa 219,000 hivi.[1]
 
we ni kabila gani mpaka ushangae watanzania wenzako? Inawezekana we si mtanzania au umeingia mjini hivi karibuni kutoka huko kwenu ukajua Tanzania nzima ni kabila lako tu. We ni mshamba umeingia mjini kujichanganya na watanzania siku za karibuni ndio maana unawashangaa raia wenzio. Wenzako wanaifahamu nchi yao hawawezi kumshanga hata mhadzabe
😂😂😂 una kitu sio bure, Jipe muda hio hali itapitaa
 
Ndio nawasikia leo,
Kuna kabila lipo mbeya, tofauti na wanyakyusa sijui ndio Waswaa mtanirekebisha kama sio nalo nimelisikia juzi, wansema kazi yao kubwa ni kulima, wanalima kama misukule, ni native sana.

Wanyantuzu nao nimewajua hivi karibuni, naambiwa ni jamii ya wasukuma..
Kuna wambugu nao..
Halafu kila wale unaambiwa ni wachawi.

Yaani hii nchi kuleta umoja na kuongea lugha moja ni jambo gumu sana, unakutana na kabila wanaongea kama wanatapika.
Hapo Manyara babati-hydom-hanang niliona watu wanaongea nikadhani anatema ulimi.
Waswaa....==Wasafwa
 
uchawi pia hawapendi mgeni afanye maendeleo iwe kuvuta umeme, maji ama kujenga utapugwa vimbora mpaka basi
Chukua mke wa mnguu adhabu yake unarogwa uhamie mbali kwa kutumia bunduki.Jina lako linaandikwa kwenye karatasi halafu karatasi inawekwa kwenye bomba la bunduki halafu mpiga bunduki ananuia uhamie mbali na huko unakokwenda usifanikiwe maisha na inakuwa hivyo kwa imani yao.
 
Back
Top Bottom