Mbinu gani ulitumia kuishi na kabila la wanguu? Moto wao sio mchezo!

madam karibu kilindi ,gairo,kiteto uone wanavyo ogopwa
Wangulu (au Wanguu) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi mipakani mwa mikoa minne ya Tanga, Dodoma, Manyara na Morogoro, hasa upande wa Kusini-Magharibi mwa mkoa wa Tanga ambako sasa ni wilaya ya Kilindi na upande wa Kaskazini-Mashariki mwa mkoa wa Morogoro ambako sasa ni wilaya ya Mvomero na milima ya Nguu. Upande wa Magharibi ni mkoa wa Manyara ambayo sasa ni wilaya ya Kiteto.

Masimulizi ya kale ya Mbega na Kimweri yanasema kuwa kabila la Wanguu ndilo kabila mama la makabila ya Wazigua, Wabondei, Wasambaa, Waluvu na Wakilindi, ambapo makabila hayo yanaendeleza mila na desturi za asili moja na katika umoja huo hujulikana pia kwa jina moja la Waseuta. Kwa asili Wanguu ni wafugaji na wakulima.

Mwaka 2009 walikuwa 219,000 hivi.[1]
 
😂😂😂 una kitu sio bure, Jipe muda hio hali itapitaa
 
Waswaa....==Wasafwa
 
Wangulu ni watu poa sana. Hizo shutuma za watu humu ni ule ule utaratibu Wa baadhi ya jamii kujiona superior dhidi ya wengine hadi kufikia stage ya kuchafuana.
ndio jamii ngeni iwakimbie chief! kusingiziwa gani huko
 
uchawi pia hawapendi mgeni afanye maendeleo iwe kuvuta umeme, maji ama kujenga utapugwa vimbora mpaka basi
Chukua mke wa mnguu adhabu yake unarogwa uhamie mbali kwa kutumia bunduki.Jina lako linaandikwa kwenye karatasi halafu karatasi inawekwa kwenye bomba la bunduki halafu mpiga bunduki ananuia uhamie mbali na huko unakokwenda usifanikiwe maisha na inakuwa hivyo kwa imani yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…