Nilipata mtoto kiutata 2010, kwanza mwanamke nilikua nshaachana Naye ila pili alikuja kunijulisha ana mimba akiwa ana miezi 8. Binafsi nikaona nimepigwa Japo kimahesabu anaweza kua wangu pia maana Mara ya mwisho nakutana Naye ilikua 26/06/2009 na mtoto akazaliwa 22/03/2010 nikasema mtoto Hana kosa nitamlea akifikisha miaka mitano tukapime DNA. Alipofikisha miaka mitano nikajiuliza mtoto atajisikiaje atakapokua mkubwa asikie baba alimpeleka kumpima DNA? na Kama mtoto sio wangu nitampeleka wap, na mama yake alishaolewa na Toka nimchukue Ana mwaka na nusu hajawahi Hata kuja kumsalimia kimsingi hawajuani.Wanaume wengi wanalea watoto sio wao! Ndo maana mimi kuna mmoja nilizaa nae mtoto wa kwanza ni pacha kabisa na mimi ila huyu wa Pili kafanya kubambikia alafu namwabia kabisa huyu wa pili sio mtoto wangu kabisa basi angekua hata amechukua vina saba vya mtoto wa kwanza napo hakuna..haya turudi ujombani na ushangazini hakuna aliyefanana nae.
Nikafatilia kwa kina kabisa Kiroho hilo swala wanasema mtoto wako hapo ni huyo mmoja tu wa kwanza huyo mwingine ana baba yake anachotaka kufanya mwanamke ni kutaka kuchuma pesa kwa kisingizio cha wa kwanza. HELL NO.
Sasa mama mtu anajitahidi kulazimisha na mimi nilishamkataa long time. Tuna mwaka wa 4 sipo nae.
Nitalea Damu yangu Tu.
NB; Wanawake hawajui tu. HAKUNA KITU KIBAYA NA NI DHAMBI KAMA KUMBAMBIKIA MTU MTOTO! Wanaume tunapenda ukweli mfate mwambie niliteleza kwa huyu mtoto hapo ndo jamaa ataamua aendelee au aache kwa kuchunguza parameters Je huyu dada ana mahusiano ya siri na huyo baba mtoto ambapo kwa asilima 99% lazima awe nayo basi unapiga chini unalea mtoto wako Before it is Too Late.
Wanawake wengine wajinga sana unaweza lea mtoto/watoto pasipo kujua na kugharamikia gharama zote alafu mwisho wa siku mkitofautiana ndo anaonesha makucha na kukwambia kwanza watoto hawa sio wako! HOW DOES THAT FEEL?
Kimsingi nikaona Mimi nitamlea Kama mwanangu sitaki kujua ni damu yangu ama sio, nitamchukulia kama mwanangu, Kwan nikilea mtoto sio damu yangu Kuna shida gan? Kimsingi sikutaka mtoto aishi Kwa shida sababu yangu. Awe wangu ama Asiwe wangu Mimi sijali. Kwa Sasa yupo kidato Cha pili namlea vizuri Tena kuliko watoto niliowazaa kwenye ndoa Ili asijihis vibaya