Mbinu ya awali kujua kama unalea mtoto wako au wa mwanaume mwenzio

Nilipata mtoto kiutata 2010, kwanza mwanamke nilikua nshaachana Naye ila pili alikuja kunijulisha ana mimba akiwa ana miezi 8. Binafsi nikaona nimepigwa Japo kimahesabu anaweza kua wangu pia maana Mara ya mwisho nakutana Naye ilikua 26/06/2009 na mtoto akazaliwa 22/03/2010 nikasema mtoto Hana kosa nitamlea akifikisha miaka mitano tukapime DNA. Alipofikisha miaka mitano nikajiuliza mtoto atajisikiaje atakapokua mkubwa asikie baba alimpeleka kumpima DNA? na Kama mtoto sio wangu nitampeleka wap, na mama yake alishaolewa na Toka nimchukue Ana mwaka na nusu hajawahi Hata kuja kumsalimia kimsingi hawajuani.

Kimsingi nikaona Mimi nitamlea Kama mwanangu sitaki kujua ni damu yangu ama sio, nitamchukulia kama mwanangu, Kwan nikilea mtoto sio damu yangu Kuna shida gan? Kimsingi sikutaka mtoto aishi Kwa shida sababu yangu. Awe wangu ama Asiwe wangu Mimi sijali. Kwa Sasa yupo kidato Cha pili namlea vizuri Tena kuliko watoto niliowazaa kwenye ndoa Ili asijihis vibaya
 
Nzuri! Kwa hiyo kesi yako upo sahihi kumbe alikubwagia mtoto..!?
Mimi nazungumzia ishu ya kubambikia na ingali bado mtu ana mahusiano na baba wa huyo mtoto na mama watoto upo nae ndani/mnaishi pamoja.
Wangapi wanasomesha watoto wa single mothers? Wengi tu.

Mimi nazungumzia mwanamke awe submissive kujua alitereza na kukueleza ukweli wanaume tunapenda ukweli hata kama ni mchungu lakini sio kubambikia kimya kimya na wengine wanaenda mbali kutoa hata jina la huyo baba mtoto🤣( mwingine ukisema tumpe jina fulani yeye anakataa anasema tumwite fulani🤣) mwisho wa siku mwanamke anakuja ropoka kwanza hao watoto sio wako "How does that Shit Feels?"

NB; Tumetofautiana Uwezo wa kubeba vitu na kuchanganua vitu kwa mapana moyoni. kwahiyo kwa upande wako upo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…