Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Unyama sana...Sema Mwamba utakuwa ulijichanganya kwa wife wa usalama
 
Hahaha.. basi hapo atatoa ushahidi kwamba kuna wanaume wakarimu.. hawana Tamaa za kimapenzi anaweza kukusaidia bila kuomba papuchi..

Kumbee hajafiti kwenye mfumo na mwamba umeona yanini mie..

🤣
Mimi kwa ujumla sina ugwadu. Ningekuwa nina ukame ningejilipua tuu
 
...kipande cha leo nimekipenda kuliko vipande vyote... Nimependa jinsi ulivoplay kama spy... Nasubiria uni-tag ukiweka muendelezooo... Alaf na hyo "track me ISW" Kama sijakosea kuandika fanya utufunulie mkuu Gentlemen_ ...inshort niseme tu nimeburudika na kujifunza pia, natamani kujifunza zaidi...

asante sana uncle Gentlemen_
 
Thanks...

Nitajitahidi niiweke vizuri zaidi maana huko mbele ndio kuna vitu vingi vingi kias..
 
Thanks...

Nitajitahidi niiweke vizuri zaidi maana huko mbele ndio kuna vitu vingi vingi kias..
usisahau kuni tag uncle Gentlemen_ kila unapotoa muendelezo, nipo na wewe bega kwa bega kila story yako na likee uncle...
 
Nakubali mike.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo alijuaje namba yako uliyoisave kwenye simu yake
 
Inaendelea....

Rayns mawardat MIRA01 Statics Tiffay

Kuna mdau ameuliza kuhusu Track Me ISW version ni nini?
Well, hii ni moja ya systems ambazo ni forbidden kwa matumizi ya Raia na pia si kila mwenye hii system anaweza itumia (Ina Secret codes/commands) zake ambazo watu wachache wanazijua so far ipo inapatikana katk black market but nyingi ni copy. hii inafanya kazi ya kudukua location ya mhusika ambaye amesetiwa/pandikiziwa huu mfumo. huu mfumo umegawanyika katika functionality nyingi ila kwa mimi niliutumia katika matumizi ya location validation.

Location Validation ni nini?: ni kwamba wakati nasimulia kuna sehemu nilielezea jinsi nimeset coordianates ktk Google map yangu, then natumia device mac adress ya host wangu kuattach payload ya google map, hili zoezi likibind vizuri. naiwekea command ya kunipa sign au blink spot katika dashboard yangu kwamba mhusika yupo katika eneo nililolisetia coordinates. mfano: una mke wako unataka kujua yupo nyumbani au hayupo? ukiingia ktk dashboard unaona kwamba yupo au hayupo. na kama hayupo kuna settings zingine unatakiwa uset kutambua yupo wapi exactly. hiyo inaitwa real time tracking mechanism.. hata akizima Location/GPS bado atapatikana.

Kwanini nilitumia hii?: nilitaka kujua ni muda gani anakuwepo kwakwe, anakaa saa ngapi (time intervals) na mambo mengine ambayo sitayaweka wazi.

Tuendelee..

Kesho yake baada ya kujua hawa watu wanaishi wapi, ilibaki kutambua identity ya mume wa yule dada ni nani? anafanya kazi gani na mambo kama hayo.. najuaje?

Asubuhi na mapema kama kawaida niliamka na kwenda Chuo, baada ya kumaliza mambo ya msingi nilikaa sehemu tulivu na kuanza upekuzi, nakumbuka alinitumia picha whatsapp ile picha ilikuja na neno forwarded. na aina ya picha ilivyopigwa ni kama alikuwa na mtu, ni picha ambayo alipiga akiwa kwake chumbani akiwa na night dress ameshika glass ya wine. so akili ikanicheza kwa kuwa yeye ndio kapigwa picha basi huyo aliyempiga kamtumia, na yeye (Huyo Dada) akanitumia mimi. sasa picha itanisaidia nini mimi?

Ni hivi: katika ulimwengu wa Forensic ile picha kuna sehemu inapitishwa, na kutoa taarifa za msingi na muhimu, naaaaam.... kama hulijui hilo basi kuna mambo mengi yatakufungua macho.. tuendelee kula story.

Basi niliexport ile picha kwenye Pc yangu na kuanza kuichunguza, nilibaini exactly location iliyopigwa, muda, siku na saa pia na kifaa kilichotumika kupiga hiyo picha. nilijitahidi kuchimba zaidi nikapata na Device unique identifier number. hili zoezi linaitwa Information gathering kwa wale Wataalamu wa matumizi ya OSINT nafkiri tunaelewana vizuri.
Basi, nikarun zile number sehemu (sitataja ni wapi) nikapata taarifa za msingi. taarifa ya msingi zaidi ni account ID ambayo ilikuwa ni Email ya Mume wake. hapa kwangu kazi ilikuwa ishaisha. nilifunga mashine na kupak vikorokoro vyangu na kwenda kulala.

Wiki ya nne sasa inaenda, sipati vitisho tena si SMS wala si kupigiwa simu. nikaona jamaa washanisahau.. kumbe jamaa wamejipanga vibaya mno. nakumbuka kuna siku nipo bafuni naoga, nikawa nasikia miguu ya mtu anapita pita nje (kibarazani) nilichofanya ni kuzima taa ya bafuni, nikaacha bomba la maji wazi.. nikarudi mlangoni nikasogeza kochi (kikochi) taratiibu.. nikachukua panga nikalishika vizuri. muda huo nina taulo tu na mapovu mgongoni, niliskia kuna mtu kama anatengua kitasa, na mwingine anamulika mulika kwa tochi upande wa chumbani, nilichokifanya ni kutulia tu kimya nikisubiri atakayeingia natoka na kichwa. walihangaika kufungua (walitaka waingie kimya kimya) naona wakaghairi na kuondoka, sikumbuki walikuwa wangapi.

Kesho yake nikaona sio tabu, nikatafuta chumba sehemu nyingine na kuhama siku ya pili yake, akili ikawa haitulii kabisa sina amani na wala sijui hatima yangu ni nini?.. nilipata hasira na nguvu nyingi kumjua huyu jamaa ni nani na ananitafutia nini?.

Naomba niongelee kitu kidogo hapa: Je unajua kwamba kama mtu anayo Email yako anauwezo wa kupata taarifa zako za msingi? ikiwemo hata namba yako ya simu? umejisajili wapi katika mifumo? na hata kuiwinda email yako (credentials) na kuidukua? atakayebisha aje.

Basi, kwa kuwa nilikuwa na Email yake niliifatilia vizuri na kubaini identity yake. kwanza alikuwa kajiunga LINKEDIN, kufungua profile yake nikabaini ni mtu mzito serikalini (Sio Usalama kama wengi mlivyodhani) ila alikuwa na wadhfa sehemu.., baada kujua hilo sikuhangaika sana, nilifanya utafiti (Information Gathering) kwenye website ya taasisi aliyokuwa anafanyia kazi, na kubaini email yake ya ofisi ni ipi.. pia nikazibaini emails zingine za staff wa pale hii njia ni common kwa wale wataalamu wa Nmap au recorn softwares (Network pentesters) mtakuwa mnanielewa vizuri ni namna gani system inakuwa uchi, nilifanya yote haya kwasababu sina resources nyingi (hela na muda) pia sikutaka physical involvement katika utafiti wangu, tofauti na yeye aliyekuwa anatuma mapolisi na watu mbalimbali kunifatilia, mie nilitumia akili zaidi.

Haya, naomba pia niwaweke sawa katika matumizi ya Emails: je mnajua kwamba unaweza clone email ya taasisi yoyote au ya mtu yeyote yule? (Email Clonning/Impersonating), je wajua kwamba unaweza kutumia temporary emails kufanya uwizi, kusambaza kirusi etc bila kuacha tracing points?.......??
Mambo ni mengi nimechoka kuandika ila next nitawaelezea ni namna gani niliweza dukua mawasiliano yake ya ofisini na binafsi na kumfanya akawa Mtumwa wangu...

Nikipata muda.
 
Nitarudi
 
Wew ni mtaalm wa IT nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…