Inaendelea..
Rayns mawardat MIRA01 Statics
Zilipita wiki mbili za Mwanzo kwa ugumu sana ingawa nilizoea kiasi hizo shida.
Kuna siku nipo Chuo nawapigisha msasa madogo wa diploma wale navyokumbuka, kuna mmoja alikuwa very interested na maswala ya Network infrastructure etc.. so akawa ananiuliza maswali mengi nikawa namjibu.
Baada ya kipindi kuisha akanifata pembeni, akaniuliza kama naweza kuwa na muda niwe nampigisha msasa hata home hivi au sehemu yotote ile katika muda wangu wa ziada.
Nikamwambia hiyo ngumu, then nikamuuliza interest yake ni nini hasa ktk hizo ishu? Hakusita kuniambia kwamba anahamu sana ya kufanya kazi ktk hizi kampuni za kimitandao like Tigo, Airtel etc. Nikampongeza then kanidokezea huko ana watu mbalimbali anafahamiana nao so yeye akipata Gamba tu kuingia ni rahisi ila anahitaji awe well competent na ndoto zake ni kusoma Telecommunications Engineering na vitu kama hivyo. Mie nikaona ananipigia kelele muda huo nishachoka, nikamwambia anipe mawasiliano yake siku nikiwa free ntamtafuta.
Wakati nipo njiani, akili ikanijia... kwanini nisitafute nini chanzo cha haya yote? Nini kipo nyuma ya pazia? Kama mimi nawindwa why na mimi nisiwinde ukweli niujue?.
Siku hiyo ilikuwa Ijumaa navyokumbuka, niliwahi kutoka nikaenda ktk ofisi yangu ile ya Zamani kuna documents za kusaini na kurudisha vitambulisho vya kazi baada ya kukamilisha michakato yote ya kuacha kazi. Baada ya hapo Akili ikanituma niende anapofanyia kazi yule Dada (Ofisini kwake).
Sitaweka wazi ni wapi exactly ila nilifika mpaka pale, kulikuwa na madereva boda kwa nje na kivuli flani hivi, nikawa kama mtu aliyesimama muda mrefu kidgo kuna jamaa akanifata kuniuliza kama kuna mtu namsubiri au vipi? Kwa mavazi yake nilitambua ni Boda yule.
Basi, nikampanga kwamba kuna Mzigo nimekuja kuuchukua ila kuna Mzigo upo hapa na mwingine kauacha nyumbani, so inabidi niende nyumbani kwake hivyo namsubiri hapa akitoka niongozane nae. Yule boda akasema poa hamna shida akapanda juu ya piki pik yake akawa ametulia anakula story tu..
Mie nikavutiwa na story zao nikawa napiga domo pale, basi ghafla tukawa kama watu waliozoeana sana yani kama mmoja wao tu. Ghafla nikaiona ile gari ya yule Manzi imefika pale ikaingia sehem ya kupaki (Kumbuka sahivi anafatwa na kupelekwa kazini na Mumewe).
Kwa kuwa gari iliingia na kupaki katika direction ambayo ilinipa mgongo sikuweza kuona nani yumo ndani. So fasta nikamvuta Boda yule niliekuwa naongea nae.
Nikaanza kumpanga stori nyingi za uongo uongo then nikamuuliza kama boda ina wese? Akasema yapo ila sio mengi. Nikamwambia nenda kaweke kama ya elf 10 maana nimetumiwa ujumbe hapa kuna sehemu natakiw niende chap so wakati nasubiri mzigo hapa.. we nenda kajaze mafuta ili ukija niwe nishachukua mzigo alafu tukianza safari ni moja kwa moja. (Nilifanya hivyo maana najua bodaboda hawawekagi mafuta ya kutosha, na sitaki mishen yangu ifeli kwa uzembe wa kijinga jinga) so far misheni yangu ni kujua makazi rasmi ya yule Manzi na Mumewe ni wapi. So tunawindana.
Basi, mwamba akarudi fasta nikamuuliza umeweka kweli wese kidebe akatoa risiti nikaichek nikaona ya saa 3 asubuhi alafu muda huo ni saa 12 jioni nikampanga akacheka sana.. nikaachana na hizo ishu nikamwambia Mzigo bado sijaletewa ingawa ni boksi kubwa je anakamba au mipira ya ziada? Akasema hana, basi akaomba pale kwa wenzie akapata. (Hiyo yote ni kumset tu awe na imani kuhusu neno mzigo).
Basi, tukakaa kama dk 10 nikamuita tena pembeni nikamwambia umeiona ile gari ? Unaijua? Akasema yaah ya Dada xxx. Nikamwambia sasa huyo ndio ana mzigo mwingine tutaongozana hadi kwake, nikamtega kumuuliza kwake ni wapi? Akaniambia kuna siku alimpeleka Msasani, na kuna siku alimpeleka Kinyerezi. Sasa hajui wapi ni kwake katika hizo sehemu mbili. Basi nikamwambia ah kama unapajua basi tutafatana nae akitoka twende tu.
Basi yule boda hakuwa na neno zaidi ya kufuta futa pikipiki yake na kuwa standby. Dakika kama 10 tena mbele ndio akatoka yule Manzi. Na pochi yake akaingia katika gari, na kuanza safari. Mie nikamtonya boda nikamwambia yule dada alitupungia mkono hapa kutusalimia em twende tuifate gari. Basi muda huo ni saa 1 na nusu usiku ilikuwa, changamoto ni nyingi sana ikiwemo mafoleni alafu mtu una bodaboda. Ikabidi aniulize kwanini nisingepanda ile gari mule wakati yupo tu mwenyewe kwanini niingie gharama za kumfata na wakati mzigo wenyewe sijaubeba.. na huko kuna bodaboda kibao. Mie nilichomjibu ni kwamba sichukui tu bodaboda mpaka nione huyu anajielewa, nikampanga pale na maneno ya kumsifia kwamba ana akili.. akajiona kweli ana akili sana.
Basi, mbelembele road ilifunguka gari zikawa zinatembea, kufika njia panda ya segerea gari ikaingia kulia kuelekea kinyerezi. Na mimi ndipo nilipogundua huyu anakaa kinyerezi maana nilifanya ulinganifu na maelezo ya boda, basi nikawa namuuliza tu boda zimebaki kilometer ngap kufika? Boda nae ananiambia hapo atakunja kushoto, atakunja kulia kuna mteremko kushoto kuna hichi.. yaana akawa anapita mule mule.. basi nikamwambia tukikaribia kufika kwake tusimame sehem yenye maduka mengi, kuna kitu ninunue kabisa.
Basi kweli ilikuwa imebaki kama kilometer 1 hivi au meter 800 boda akasimama nikashuka kuzuga zuga pale. Nia yangu nisiifate bumper to bumper ile gari, pia boda hachelewi kuovertake kwa mbele akanifikisha kabla ya wao hawajafika ikawa noma pale.
Basi baada ya kuzuga kama dk 6 hivi nikamwambia boda tuendelee na safari na ananidai kias gani? Boda akashangaa maana anategemea ningepakia mzigo alafu nirudi nae. Mie nikamjibu kwamba yule Dada kanitumia ujumbe wakati nipo dukani pale kwamba chakula tayari so nile kwanza ndio niondoke, nikaongezea kwamba namjua yule, tutapiga mastory sana pale nitakuchelewesha. Akanitajia kiasi anachodai na kunifikisha kabisa getini.
Nikashuka nikamlipa, nikachukua na namba za bodaboda yule. Yeye akageuza na kusepa.
Sasa, ule mtaa wote upo kimyaa na ni nyumba kali tupu. Yaani ni ghorofa tu zimepangana. Akaja mlinzi nje pale maana alisikia kuna mlio wa pikipiki, then ikazimwa watu wakaongeoa ongea.. pikipik ikawashwa na kuondoka. Alikuja kuhakikisha kama kuna mgeni au nini?
Kutoka nje kanikuta na mimi nishasogea pembeni kidogo, akanisalimia na mimi nikaitikia nikamsogelea, nikamuuliza jina tofauti kabisa kama anakaa mule? Akasema hapana huyo hakai hapo, nikamzugisha kwamba nimeelekezwa kwamba jirani wa huyo mtu ninaemuulizia jina lake ni fulani (Nikataja jina la yule dada) yule mlinzi akasema ni kweli hapa ndio kwa huyo jirani. Ila huyo mwenyeji wako unayemuulizia si hapo nijaribu mbele huko au kwa jina lingine. Basi nikamshukuru yeye akarudi ndani, mie nikaset Coordinates katika Google map ili nisipoteze location, ikasave then nikashare ktk system moja inaitwa Track me ISW version. Nitakuja kuielezea hapo baadae.
Then baada ya kufanya hivyo nikatoka pale na kurudi mainload, nilivyofika sikuwa mgeni maana nina idea na maeneo ya huko. Na sio mbali na nilipokuwa nakaa maana mie nilikuwa nakaa Tabata katikati huko.
Hii siku nilirudi mapema kidogo, nikakaa chini na kuweka records zangu vizuri. Baada ya kumaliza zoez la kwanza. La kujua huyu Dada anakaa wapi. Zoez la pili ni kujua Mumewe ni nani? So kesho yake nikaendelea na mission inayofata..
Itaendelea.. nikitulia...[emoji50][emoji100]