Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Wazee wa kupambania Kombe..
Huwa mnatumia Njia gani kuomba/kuchukua namba za simu katika Mazingira MAGUMU na HATARISHI?

Umafia:

Part 1>
Nilikuwa nipo katika Daladala watu wengi vibaya mno, nikatupia jicho pembeni nikaona KIFAA kimetulia kinachezea simu. Nikajiuliza hapa namba nabebaje? Kuangalia nje bado vituo viwili nishuke.

Kuchek katika wallet business card binafsi zimeisha zimebaki za Ofisini (Michoresho) nikaona hii hapana kuitoa.

Nikajipapasa huku na kule bahati nzuri nilibahatisha kipande cha TICKET ya Bus la mkoani, na katika ile ticket kuna namba yangu ya SIMU, sikujiuliza mara mbili wakati nashuka nikamshtua yule mrembo kwa kumgusa begani then ile ticket nikaipitisha kwa chini kama vile alikuwa kaiangusha then nikamkazia machoni huku nikimuonyesha ishara ya NIPIGIE. Mie nikashuka zangu huyo Home nikatulia.

Zikapita kama siku 5 kimya, nikaona hapa Mkeka umechanika.. siku ya 6 jioni nipo viti virefu nashangaa namba ngeni kupokea ni yule Manzi.. akajitambulisha pale.. then the rest is history..😋

Kuna wengine wanatumia mpaka Hela kuandika namba (Karatasi hakuna).. mtu anachukua noti ya elf 10 anachora namba yake anamkabidhi mrembo..
Mbinu zako zakipuuzi uwo ni ukwepaji wa kutongoza🙌
 
Wazee wa kupambania Kombe..
Huwa mnatumia Njia gani kuomba/kuchukua namba za simu katika Mazingira MAGUMU na HATARISHI?

Umafia:

Part 1>
Nilikuwa nipo katika Daladala watu wengi vibaya mno, nikatupia jicho pembeni nikaona KIFAA kimetulia kinachezea simu. Nikajiuliza hapa namba nabebaje? Kuangalia nje bado vituo viwili nishuke.

Kuchek katika wallet business card binafsi zimeisha zimebaki za Ofisini (Michoresho) nikaona hii hapana kuitoa.

Nikajipapasa huku na kule bahati nzuri nilibahatisha kipande cha TICKET ya Bus la mkoani, na katika ile ticket kuna namba yangu ya SIMU, sikujiuliza mara mbili wakati nashuka nikamshtua yule mrembo kwa kumgusa begani then ile ticket nikaipitisha kwa chini kama vile alikuwa kaiangusha then nikamkazia machoni huku nikimuonyesha ishara ya NIPIGIE. Mie nikashuka zangu huyo Home nikatulia.

Zikapita kama siku 5 kimya, nikaona hapa Mkeka umechanika.. siku ya 6 jioni nipo viti virefu nashangaa namba ngeni kupokea ni yule Manzi.. akajitambulisha pale.. then the rest is history..[emoji39]

Kuna wengine wanatumia mpaka Hela kuandika namba (Karatasi hakuna).. mtu anachukua noti ya elf 10 anachora namba yake anamkabidhi mrembo..
malaya hawa wakupatana nao unapata nao shida?
hao wauza kum.a wewe ndo umetumia njia ndeefu.
 
Story ile ya PART 2:
Naona kuna wadau wameomba niendelezee nini kilikuja nitokea baadae.
MIRA01 mawardat Statics

Tuliwasiliana na yule Manzi mara kwa mara, nikaja kugundua ni Mke wa mtu na yupo katika Ndoa changa yenye visa vingi. Ambavyo baadhi aliniweka wazi na vingine hakuniambia nilikuja kujua tu baada ya kufanya tafiti zangu.

Kuna siku tulipanga tuonane maeneo ya Mjini Kkoo, yeye alitokea kazini maana alikuwa anafanya katika moja ya hii mitandao ya Simu, basi bhana mida ya jioni tulivu nakumbuka ilikuwa Ijumaa tulikutana Kkoo katika petrol station iliyopo karibu na mtaa wa kongo.

Alinipick tukakubaliana pale sio sehem nzuri ya kuongea hivyo tuingie atleast City Mall. Nikashangaa tumefika Mnazi mmoja akatafuta parking akaipaki ile gari akashuka na mie nikashuka akaniambia "Tuchukue Bajaji or tutembee?" sikumwelewa alikuwa anamaanisha nini ila nikamwambia tuchukue bajaji, nikasimamisha pale tukapanda na kusogea mpaka City Mall.

Kuingia mpaka ndani, kuna restaurant moja ipo floor ya 3 kwa wale wahindi tukakaa pale zikaanza story za hapa na pale.

Nilimuuliza swali dogo tu "Kwanini umeacha gari Mnazi mmoja wakati huku pia kuna parking"? alicheka tu hakunijibu kitu. Mie sikumuuliza tena tukawa tunaongea tu ishu zingine ghafla simu yake ikaita na muda huo tumeagiza Chakula tunasubiri.

Alisogea pembeni akaongea kama Dakika 2 na kurudi akiwa kabadirika sura kias. Nikamuuliza nini shida? Akaniambia amepigiwa simu ya dharula anahitajika kurudi ofisini haraka sana.

Mie sikuwa na usemi, akakusanya pochi yake, akatoweka pale.

Sasa mie nipo tu sielewi zikaja plate mbili za msosi, nikaomba moja ifungwe as take home package. Nyingine nikaipiga pale pale, nikalipa Bill kwa kadi ikawa inasumbua.
Sasa nikajaribu kuchek simu yangu nione kama meseji imerudi au vipi, kumbe simu nayo niliacha katika ile gari ya yule Manzi. (Kiswaswadu) sasa nipo na simu kubwa kumchek simu hapokei, napiga ya kwangu iliita mara moja ikawa haiiti tena.

Basi nikaclear kwa cash ile Bill, nikajipindua kutafuta Daladala Mnazi mmoja nirudi Tabata.

Siku ilipita bila kuwasiliana nae tena, kesho yake nikawa napiga simu yangu inaita tu haipokelewi. Ya yule Dada nayo inaita haipokelewi. Nikapata wasiwasi inakuaje hii?

Basi nikaendelea na shughuli zangu za kila siku.. Jioni ya siku ya 4 tangia tuachane nae kule town, akanitumia text (XXX We need to talk). Sikujibu text nilimpigia hakupokea akawa anasema tuchat yupo ktk kikao.

Mie akili ikanicheza huyu sio kawaida yake.. ikaja text ya kuomba appointment kinondoni maeneo ya Biafra, usiku saa 2. Nikamuuliza swali kuhusu simu yangu akasema ninayo ila imecrack kioo hivyo hawezi kupokea namba ambayo hajui nani anapiga asije nigombanisha au kuniharibia mambo yangu. Ila tuchat tu nisipige simu.

Basi sawa, kuna Mwanangu mmoja nilimpanga situation ilivyo, akaniambia hiyo haipo sawa kuna viashiria sio vya kawaida. (Jamaa anaamini sana ushirikina) akawa ananijaza huwenda huyo manzi ni Jini. Mie nikaona ananizingua tu tukaagana pale huyo nikadaka Daladala mpaka Kinondoni nikatafuta kona moja nikatulia. (Nilifika mapema zaidi mida ya saa 12).

Nikapiga ile simu ya yule Manzi hapokei. Ikaja text ambayo kwa ule mwandiko nikaona kabisa hii mbona sauti ya kiume kabisa. Maana alinicommand nisiwe kama mtoto mdogo ananiambia kitu sisikiii na mambo kama hayo. Mie nikamrudishia text kwamba yeye ndio mtoto kwanini hataki kupokea simu? Kuna nini kinaendelea? Hakunijibu mpaka saa 1 na nusu akaniambia umefika? Nikamjibu bado nakaribia after 20 minutes ntakuwa hapo.

Nia yangu nione tukio zima anakujaje? And this time sikutaka kabisa kuwa front front.

Baada ya dk kadhaa almost kama 10, niliona ile gari imesimama karibu na zile costa zinazopaki pale, wakashuka watu wawili mmoja alisimama upande ule mwingine akasogea upande wa pili.

Alafu ile gari ikapaki pembeni kidogo.

Akashuka yule Manzi akasimama mbele ya gari yake.

Mie muda huo nausoma tu mchezo. Safari hii ndio akanipigia simu nipo wapi ? Nikamuuliza text ya mwisho umeisoma kweli mbn unaniuliza swali hilo hilo na uligoma tuongee kwa simu? Akawa anababaika.

Nikamwambia nakaribia nisubiri.

Sasa kichwani nikapata ukakasi ni nini exactly kinaendelea pale, nilichofanya nilisogea upande wa pili nikawa nawatazama horizontally, nikazima simu.

Ilipita kama nusu saa hivi akashuka mtu mwingine wa tatu ambaye yeye alishukia upande wa Dereva (Ndie aliyekuwa anaendesha ile gari) nikaona wanajibishana pale wale wengine wakasogea wakaamua wapande kwenye gari waondoke.

Na mimi nikabadiri njia nikazunguka huko mbali nikaamsha.

Nafika home kuwasha simu, nakutana na Text kibao za upo wapi etc. Sikujibu.

Nikawa sina Amani ni nini kinaendelea ukizingatia hata Mzigo sijala.

Ile simu yangu walitafuta txt wakapata ya jamaa yangu mmoja wa kazini, wakaona huyu atawafaa kunikutanisha nao. Maana walimpigia kwa namba nyingine then wakamuomba awaelekeze napoishi ili wanione mimi ndugu yao sijui na vitu kama hivyo. Jamaa nae hakuwaza mara mbili akawaelekeza kweli.


Itaendelea..
hii kesi kama mkuu 1 wa idarani,nikiandika hapa machawa watajua chap.

wake zao ndo wanatusumbuaga baadala wadili na wake zao......
 
Wazee wa kupambania Kombe..
Huwa mnatumia Njia gani kuomba/kuchukua namba za simu katika Mazingira MAGUMU na HATARISHI?

Umafia:

Part 1>
Nilikuwa nipo katika Daladala watu wengi vibaya mno, nikatupia jicho pembeni nikaona KIFAA kimetulia kinachezea simu. Nikajiuliza hapa namba nabebaje? Kuangalia nje bado vituo viwili nishuke.

Kuchek katika wallet business card binafsi zimeisha zimebaki za Ofisini (Michoresho) nikaona hii hapana kuitoa.

Nikajipapasa huku na kule bahati nzuri nilibahatisha kipande cha TICKET ya Bus la mkoani, na katika ile ticket kuna namba yangu ya SIMU, sikujiuliza mara mbili wakati nashuka nikamshtua yule mrembo kwa kumgusa begani then ile ticket nikaipitisha kwa chini kama vile alikuwa kaiangusha then nikamkazia machoni huku nikimuonyesha ishara ya NIPIGIE. Mie nikashuka zangu huyo Home nikatulia.

Zikapita kama siku 5 kimya, nikaona hapa Mkeka umechanika.. siku ya 6 jioni nipo viti virefu nashangaa namba ngeni kupokea ni yule Manzi.. akajitambulisha pale.. then the rest is history..😋

Kuna wengine wanatumia mpaka Hela kuandika namba (Karatasi hakuna).. mtu anachukua noti ya elf 10 anachora namba yake anamkabidhi mrembo..
Ujinga mtupu!! Duh nimechangia bila kuangalia hii post ipo forum ipi
 
Hahahaha... ungeweka shuka la Mmsai (10,000) uone kama hajakuchek
babu 10k?labda demu akupende mwenyewe tu sio kwaajili ya tembo!
kuna madem/wanawake wako vizuri kila idara.kuandika no kwa hela anaweza ona umechukulia poa.

kuna kila njia ya kudeal na kila mwanamke.

kuandika no kwenye tembo(10k) hawa uswazi take away/average.
 
Inaendelea..
Rayns mawardat MIRA01 Statics

Zilipita wiki mbili za Mwanzo kwa ugumu sana ingawa nilizoea kiasi hizo shida.

Kuna siku nipo Chuo nawapigisha msasa madogo wa diploma wale navyokumbuka, kuna mmoja alikuwa very interested na maswala ya Network infrastructure etc.. so akawa ananiuliza maswali mengi nikawa namjibu.

Baada ya kipindi kuisha akanifata pembeni, akaniuliza kama naweza kuwa na muda niwe nampigisha msasa hata home hivi au sehemu yotote ile katika muda wangu wa ziada.

Nikamwambia hiyo ngumu, then nikamuuliza interest yake ni nini hasa ktk hizo ishu? Hakusita kuniambia kwamba anahamu sana ya kufanya kazi ktk hizi kampuni za kimitandao like Tigo, Airtel etc. Nikampongeza then kanidokezea huko ana watu mbalimbali anafahamiana nao so yeye akipata Gamba tu kuingia ni rahisi ila anahitaji awe well competent na ndoto zake ni kusoma Telecommunications Engineering na vitu kama hivyo. Mie nikaona ananipigia kelele muda huo nishachoka, nikamwambia anipe mawasiliano yake siku nikiwa free ntamtafuta.

Wakati nipo njiani, akili ikanijia... kwanini nisitafute nini chanzo cha haya yote? Nini kipo nyuma ya pazia? Kama mimi nawindwa why na mimi nisiwinde ukweli niujue?.

Siku hiyo ilikuwa Ijumaa navyokumbuka, niliwahi kutoka nikaenda ktk ofisi yangu ile ya Zamani kuna documents za kusaini na kurudisha vitambulisho vya kazi baada ya kukamilisha michakato yote ya kuacha kazi. Baada ya hapo Akili ikanituma niende anapofanyia kazi yule Dada (Ofisini kwake).

Sitaweka wazi ni wapi exactly ila nilifika mpaka pale, kulikuwa na madereva boda kwa nje na kivuli flani hivi, nikawa kama mtu aliyesimama muda mrefu kidgo kuna jamaa akanifata kuniuliza kama kuna mtu namsubiri au vipi? Kwa mavazi yake nilitambua ni Boda yule.

Basi, nikampanga kwamba kuna Mzigo nimekuja kuuchukua ila kuna Mzigo upo hapa na mwingine kauacha nyumbani, so inabidi niende nyumbani kwake hivyo namsubiri hapa akitoka niongozane nae. Yule boda akasema poa hamna shida akapanda juu ya piki pik yake akawa ametulia anakula story tu..

Mie nikavutiwa na story zao nikawa napiga domo pale, basi ghafla tukawa kama watu waliozoeana sana yani kama mmoja wao tu. Ghafla nikaiona ile gari ya yule Manzi imefika pale ikaingia sehem ya kupaki (Kumbuka sahivi anafatwa na kupelekwa kazini na Mumewe).

Kwa kuwa gari iliingia na kupaki katika direction ambayo ilinipa mgongo sikuweza kuona nani yumo ndani. So fasta nikamvuta Boda yule niliekuwa naongea nae.

Nikaanza kumpanga stori nyingi za uongo uongo then nikamuuliza kama boda ina wese? Akasema yapo ila sio mengi. Nikamwambia nenda kaweke kama ya elf 10 maana nimetumiwa ujumbe hapa kuna sehemu natakiw niende chap so wakati nasubiri mzigo hapa.. we nenda kajaze mafuta ili ukija niwe nishachukua mzigo alafu tukianza safari ni moja kwa moja. (Nilifanya hivyo maana najua bodaboda hawawekagi mafuta ya kutosha, na sitaki mishen yangu ifeli kwa uzembe wa kijinga jinga) so far misheni yangu ni kujua makazi rasmi ya yule Manzi na Mumewe ni wapi. So tunawindana.

Basi, mwamba akarudi fasta nikamuuliza umeweka kweli wese kidebe akatoa risiti nikaichek nikaona ya saa 3 asubuhi alafu muda huo ni saa 12 jioni nikampanga akacheka sana.. nikaachana na hizo ishu nikamwambia Mzigo bado sijaletewa ingawa ni boksi kubwa je anakamba au mipira ya ziada? Akasema hana, basi akaomba pale kwa wenzie akapata. (Hiyo yote ni kumset tu awe na imani kuhusu neno mzigo).

Basi, tukakaa kama dk 10 nikamuita tena pembeni nikamwambia umeiona ile gari ? Unaijua? Akasema yaah ya Dada xxx. Nikamwambia sasa huyo ndio ana mzigo mwingine tutaongozana hadi kwake, nikamtega kumuuliza kwake ni wapi? Akaniambia kuna siku alimpeleka Msasani, na kuna siku alimpeleka Kinyerezi. Sasa hajui wapi ni kwake katika hizo sehemu mbili. Basi nikamwambia ah kama unapajua basi tutafatana nae akitoka twende tu.

Basi yule boda hakuwa na neno zaidi ya kufuta futa pikipiki yake na kuwa standby. Dakika kama 10 tena mbele ndio akatoka yule Manzi. Na pochi yake akaingia katika gari, na kuanza safari. Mie nikamtonya boda nikamwambia yule dada alitupungia mkono hapa kutusalimia em twende tuifate gari. Basi muda huo ni saa 1 na nusu usiku ilikuwa, changamoto ni nyingi sana ikiwemo mafoleni alafu mtu una bodaboda. Ikabidi aniulize kwanini nisingepanda ile gari mule wakati yupo tu mwenyewe kwanini niingie gharama za kumfata na wakati mzigo wenyewe sijaubeba.. na huko kuna bodaboda kibao. Mie nilichomjibu ni kwamba sichukui tu bodaboda mpaka nione huyu anajielewa, nikampanga pale na maneno ya kumsifia kwamba ana akili.. akajiona kweli ana akili sana.

Basi, mbelembele road ilifunguka gari zikawa zinatembea, kufika njia panda ya segerea gari ikaingia kulia kuelekea kinyerezi. Na mimi ndipo nilipogundua huyu anakaa kinyerezi maana nilifanya ulinganifu na maelezo ya boda, basi nikawa namuuliza tu boda zimebaki kilometer ngap kufika? Boda nae ananiambia hapo atakunja kushoto, atakunja kulia kuna mteremko kushoto kuna hichi.. yaana akawa anapita mule mule.. basi nikamwambia tukikaribia kufika kwake tusimame sehem yenye maduka mengi, kuna kitu ninunue kabisa.

Basi kweli ilikuwa imebaki kama kilometer 1 hivi au meter 800 boda akasimama nikashuka kuzuga zuga pale. Nia yangu nisiifate bumper to bumper ile gari, pia boda hachelewi kuovertake kwa mbele akanifikisha kabla ya wao hawajafika ikawa noma pale.

Basi baada ya kuzuga kama dk 6 hivi nikamwambia boda tuendelee na safari na ananidai kias gani? Boda akashangaa maana anategemea ningepakia mzigo alafu nirudi nae. Mie nikamjibu kwamba yule Dada kanitumia ujumbe wakati nipo dukani pale kwamba chakula tayari so nile kwanza ndio niondoke, nikaongezea kwamba namjua yule, tutapiga mastory sana pale nitakuchelewesha. Akanitajia kiasi anachodai na kunifikisha kabisa getini.

Nikashuka nikamlipa, nikachukua na namba za bodaboda yule. Yeye akageuza na kusepa.

Sasa, ule mtaa wote upo kimyaa na ni nyumba kali tupu. Yaani ni ghorofa tu zimepangana. Akaja mlinzi nje pale maana alisikia kuna mlio wa pikipiki, then ikazimwa watu wakaongeoa ongea.. pikipik ikawashwa na kuondoka. Alikuja kuhakikisha kama kuna mgeni au nini?

Kutoka nje kanikuta na mimi nishasogea pembeni kidogo, akanisalimia na mimi nikaitikia nikamsogelea, nikamuuliza jina tofauti kabisa kama anakaa mule? Akasema hapana huyo hakai hapo, nikamzugisha kwamba nimeelekezwa kwamba jirani wa huyo mtu ninaemuulizia jina lake ni fulani (Nikataja jina la yule dada) yule mlinzi akasema ni kweli hapa ndio kwa huyo jirani. Ila huyo mwenyeji wako unayemuulizia si hapo nijaribu mbele huko au kwa jina lingine. Basi nikamshukuru yeye akarudi ndani, mie nikaset Coordinates katika Google map ili nisipoteze location, ikasave then nikashare ktk system moja inaitwa Track me ISW version. Nitakuja kuielezea hapo baadae.

Then baada ya kufanya hivyo nikatoka pale na kurudi mainroad, nilivyofika sikuwa mgeni maana nina idea na maeneo ya huko. Na sio mbali na nilipokuwa nakaa maana mie nilikuwa nakaa Tabata katikati huko.
Hii siku nilirudi mapema kidogo, nikakaa chini na kuweka records zangu vizuri. Baada ya kumaliza zoez la kwanza. La kujua huyu Dada anakaa wapi. Zoez la pili ni kujua Mumewe ni nani? So kesho yake nikaendelea na mission inayofata..

Itaendelea.. nikitulia...[emoji50]‍[emoji100]
Aisee___story tamu.
 
Inaendelea....

Rayns mawardat MIRA01 Statics Tiffay

Kuna mdau ameuliza kuhusu Track Me ISW version ni nini?
Well, hii ni moja ya systems ambazo ni forbidden kwa matumizi ya Raia na pia si kila mwenye hii system anaweza itumia (Ina Secret codes/commands) zake ambazo watu wachache wanazijua so far ipo inapatikana katk black market but nyingi ni copy. hii inafanya kazi ya kudukua location ya mhusika ambaye amesetiwa/pandikiziwa huu mfumo. huu mfumo umegawanyika katika functionality nyingi ila kwa mimi niliutumia katika matumizi ya location validation.

Location Validation ni nini?: ni kwamba wakati nasimulia kuna sehemu nilielezea jinsi nimeset coordianates ktk Google map yangu, then natumia device mac adress ya host wangu kuattach payload ya google map, hili zoezi likibind vizuri. naiwekea command ya kunipa sign au blink spot katika dashboard yangu kwamba mhusika yupo katika eneo nililolisetia coordinates. mfano: una mke wako unataka kujua yupo nyumbani au hayupo? ukiingia ktk dashboard unaona kwamba yupo au hayupo. na kama hayupo kuna settings zingine unatakiwa uset kutambua yupo wapi exactly. hiyo inaitwa real time tracking mechanism.. hata akizima Location/GPS bado atapatikana.

Kwanini nilitumia hii?: nilitaka kujua ni muda gani anakuwepo kwakwe, anakaa saa ngapi (time intervals) na mambo mengine ambayo sitayaweka wazi.

Tuendelee..

Kesho yake baada ya kujua hawa watu wanaishi wapi, ilibaki kutambua identity ya mume wa yule dada ni nani? anafanya kazi gani na mambo kama hayo.. najuaje?

Asubuhi na mapema kama kawaida niliamka na kwenda Chuo, baada ya kumaliza mambo ya msingi nilikaa sehemu tulivu na kuanza upekuzi, nakumbuka alinitumia picha whatsapp ile picha ilikuja na neno forwarded. na aina ya picha ilivyopigwa ni kama alikuwa na mtu, ni picha ambayo alipiga akiwa kwake chumbani akiwa na night dress ameshika glass ya wine. so akili ikanicheza kwa kuwa yeye ndio kapigwa picha basi huyo aliyempiga kamtumia, na yeye (Huyo Dada) akanitumia mimi. sasa picha itanisaidia nini mimi?

Ni hivi: katika ulimwengu wa Forensic ile picha kuna sehemu inapitishwa, na kutoa taarifa za msingi na muhimu, naaaaam.... kama hulijui hilo basi kuna mambo mengi yatakufungua macho.. tuendelee kula story.

Basi niliexport ile picha kwenye Pc yangu na kuanza kuichunguza, nilibaini exactly location iliyopigwa, muda, siku na saa pia na kifaa kilichotumika kupiga hiyo picha. nilijitahidi kuchimba zaidi nikapata na Device unique identifier number. hili zoezi linaitwa Information gathering kwa wale Wataalamu wa matumizi ya OSINT nafkiri tunaelewana vizuri.
Basi, nikarun zile number sehemu (sitataja ni wapi) nikapata taarifa za msingi. taarifa ya msingi zaidi ni account ID ambayo ilikuwa ni Email ya Mume wake. hapa kwangu kazi ilikuwa ishaisha. nilifunga mashine na kupak vikorokoro vyangu na kwenda kulala.

Wiki ya nne sasa inaenda, sipati vitisho tena si SMS wala si kupigiwa simu. nikaona jamaa washanisahau.. kumbe jamaa wamejipanga vibaya mno. nakumbuka kuna siku nipo bafuni naoga, nikawa nasikia miguu ya mtu anapita pita nje (kibarazani) nilichofanya ni kuzima taa ya bafuni, nikaacha bomba la maji wazi.. nikarudi mlangoni nikasogeza kochi (kikochi) taratiibu.. nikachukua panga nikalishika vizuri. muda huo nina taulo tu na mapovu mgongoni, niliskia kuna mtu kama anatengua kitasa, na mwingine anamulika mulika kwa tochi upande wa chumbani, nilichokifanya ni kutulia tu kimya nikisubiri atakayeingia natoka na kichwa. walihangaika kufungua (walitaka waingie kimya kimya) naona wakaghairi na kuondoka, sikumbuki walikuwa wangapi.

Kesho yake nikaona sio tabu, nikatafuta chumba sehemu nyingine na kuhama siku ya pili yake, akili ikawa haitulii kabisa sina amani na wala sijui hatima yangu ni nini?.. nilipata hasira na nguvu nyingi kumjua huyu jamaa ni nani na ananitafutia nini?.

Naomba niongelee kitu kidogo hapa: Je unajua kwamba kama mtu anayo Email yako anauwezo wa kupata taarifa zako za msingi? ikiwemo hata namba yako ya simu? umejisajili wapi katika mifumo? na hata kuiwinda email yako (credentials) na kuidukua? atakayebisha aje.

Basi, kwa kuwa nilikuwa na Email yake niliifatilia vizuri na kubaini identity yake. kwanza alikuwa kajiunga LINKEDIN, kufungua profile yake nikabaini ni mtu mzito serikalini (Sio Usalama kama wengi mlivyodhani) ila alikuwa na wadhfa sehemu.., baada kujua hilo sikuhangaika sana, nilifanya utafiti (Information Gathering) kwenye website ya taasisi aliyokuwa anafanyia kazi, na kubaini email yake ya ofisi ni ipi.. pia nikazibaini emails zingine za staff wa pale hii njia ni common kwa wale wataalamu wa Nmap au recorn softwares (Network pentesters) mtakuwa mnanielewa vizuri ni namna gani system inakuwa uchi, nilifanya yote haya kwasababu sina resources nyingi (hela na muda) pia sikutaka physical involvement katika utafiti wangu, tofauti na yeye aliyekuwa anatuma mapolisi na watu mbalimbali kunifatilia, mie nilitumia akili zaidi.

Haya, naomba pia niwaweke sawa katika matumizi ya Emails: je mnajua kwamba unaweza clone email ya taasisi yoyote au ya mtu yeyote yule? (Email Clonning/Impersonating), je wajua kwamba unaweza kutumia temporary emails kufanya uwizi, kusambaza kirusi etc bila kuacha tracing points?.......??
Mambo ni mengi nimechoka kuandika ila next nitawaelezea ni namna gani niliweza dukua mawasiliano yake ya ofisini na binafsi na kumfanya akawa Mtumwa wangu...

Nikipata muda.
Umetisha,big up bro[emoji1317]


Tupo pamoja.
 
Back
Top Bottom