Mbinu za utajiri ni ubahili, bila kuwa bahili sahau utajiri. Faida yake naiona

Mbinu za utajiri ni ubahili, bila kuwa bahili sahau utajiri. Faida yake naiona

Kuna totauti kati ya kuto kula vizuri(Quality) na kuto kula kushiba (Quantity)...vidonda vya tumbo vinasababishwa na kutokula kwa wakati au kuto kushiba.

Unaweza ukatumia 2500 kwasiku usipate vidonda vya tumbo na mtu akala 10,000 kwaaiku akapata suala ni Quatity sio Quality ya msosi.

Ninauwezo wa kula 2500 maisha yangu yote na sipati vidonda vya tumbo
Vipi mawazo ya kimaisha kwa kujibanabana hakusababishi hivyo vidonda vya tumbo?
 
Hili wazo la ubahili ni zuri ila uhalisia wake unategemea background ya mtu na mtu. Wengine ndio wategemezi wa wadogo zao na sio marafiki,hivyo mnyororo wa utegemezi haukatiki kirahisi.
Unaweza kuwapunguza marafiki lakini sio ndugu. Kama ndugu aliwahi kukusaidia buku ya daftari basi tayari ni kitanzi kingine.
Afrika ngumu sana hii.
Inaonekana wewe ni mtu mwenye moyo wa shukrani na unajitahidi sana kulipa fadhili, hata hivyo lazima uangalie kesho yako itakavyokuwa. Usitarajie kila mtu yupo kama wewe na kwamba watakumbuka msaada wako
 
Acha uongo. Nina matajiri wana vimada 10. Na watoto 20. Kila kimada ana mtoto. Utajiri ninuwezo wa kupata kipato zaidi ya matumizi yako tu. Kama unadhani kutokula vizuri, kuishi vizuri, kisafiri vizuri ndio kutakujirisha vizuri, Sawa. Utajikuta unaviacha wakula ambao hawakuvichuma.
Mtoa mada ajamlenga Tajiri kamlenga aliye kwenye Huatling stage.
 
Mawazo ya kimaisha ni nini kila aliye timamu kiakili ana mawazo ya kimaisha unamaanisha nini ukisema mawazo ya kimaisha.
Nilimaanisha wingi/mrundikano wa mawazo/msongo wa mawazo ila si mawazo kama mawazo kikawaida.
 
kuna sehem kasema hali vizuri halali vizuri?wabongo bana..anakimbia machawa kama wewe hapo huchelewi ishia kula maisha kufa kwaja halafu unaagiza nusu kuku boss anakula chipsi kavu
hela yake matumizi mkuu
 
Nilimaanisha wingi/mrundikano wa mawazo/msongo wa mawazo ila si mawazo kama mawazo kikawaida.
Sijaelewa yaani uwo msongo wa mawazo umekujaje yaani una uhusiano gani na mimi kufanya Saving...Depression inatokana na kupatwa na tatizo au changamoto nashangaa yaani imekujaje.
 
Sijaelewa yaani uwo msongo wa mawazo umekujaje yaani una uhusiano gani na mimi kufanya Saving...Depression inatokana na kupatwa na tatizo au changamoto nashangaa yaani imekujaje.
Yani mtu una hela, usiitumie kadri uwezavyo sababu una malengo kwa mwaka au miaka kadhaa ijayo kisha usiwe na msongo wa mawazo, kabisa???

Onana na wataalamu watakusaidia mkuu jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha vidonda vya tumbo.
 
Hii ndio akili, usije hata siku moja ukawathamini machawa.
Kuwa bahili jenga kwa kadri utavyopata, Kama hutaona faida Sasa baada ya miaka 10 au 20 utaona faida yake.
Usikubali wakuite mwana, hili neno mwana linachelewesha Sana maendeleo yako binafsi.
Utasikia "mwana Mtu poa Sana", "mwana Mtu Safi", Mara "mwana sio mchoyo"
Siku ukianguka na wenzio wakutreat hivyo hivyo usilalamike watu hawakupendi.
 
Yani mtu una hela, usiitumie kadri uwezavyo sababu una malengo kwa mwaka au miaka kadhaa ijayo kisha usiwe na msongo wa mawazo, kabisa???

Onana na wataalamu watakusaidia mkuu jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha vidonda vya tumbo.
Duu nimechoka kuandika maisha mema
 
Mi ni bahili nadhani hata nakuzidi x 100, but sitaki kujitesa, na gari zuri expensive one, nina nyumba kali, kwangu kutamu balaa, na kila weekend nakula bata na saving kama kawa...... na hii kwangu ndo definition ya maisha


Kujitesa ni mwiko eti ili nije kuwa tajiri , never[emoji848]
Madam naomba kuwa mlinzi wako binafsi .hamna hamna basi gate keeper km ikikupendeza
 
Ndio Hawa wanaosema Fred vunjabei anauza madawa, kisa tu maisha aliyonayo.
Juzi wakati anasaidi dili la jezi la bilioni 2 Kuna watu walikasirika Sana, povu likawatoka. Ooh anatoa wapi pesa, Mara 40 yake itafika tu.
Hawa ndio wabongo
Kuna jamaa ukitaja jina Fred VunjaBei utasikia "Nilisoma nae galanosi "
 
Ukweli mchungu.

Watu wengi wanatamani Sana kuwa matajiri lakini hawajui mbinu gani zinatumika.

Sisemi matajiri wote walikuwa mabahiri, la hasha Ila kikwetukwetu hii mbinu ya ubahili ndio njia nzuri ya kuelekea kuwa tajiri.
Ubahili nachukulia Kama kitendo Cha kutotumia pesa kwenye matumizi yasiyo ya lazima.

Hii njia nimeitumia miaka 10 Sasa na faida yake nimeiona. Kuwa mbahili sana, alafu utanishukuru baadae.

Pesa nilikuwa napata nzuri tu kwenye mishe zangu za gen supplies na kwenye construction Ila nilikuwa naishi maisha ya kawaida Sana, chumba na sebule kwa elfu 60 kimara huko ndani ndani. Ila kwa mwezi nilikuwa nakusanya faida mil 4, huu ni wastani.

Kuna mwezi napata kazi nyingi faida hadi m 8, 10 na Kuna mwezi napata mil 2 na Kuna mwezi hakuna kazi kabisa hivyo nafidia huo mwezi kwa mwezi niliopata zaidi

Ubahili unalipaje?
Baada tu ya kununua plots kadhaa jijini hapa, kila mwezi nikaanza ku-save mil 1.8 kwa ajili ya kujenga na mil 1.8 nyingine kwa ajili ya biashara ya hardware. Hivyo mwezi mzima nauendesha kwa laki 4 tu, inatoa 60 ya kupanga.

Hapo kulikuwa hakuna Cha kwenda kula bata wala kuhonga Wala kulakula ovyo(wengi mnaita eti kula vizuri). Na hakuna cha kununua gari Wala nini, nilikuwa na pikipiki boxer kwa ajili ya kuwahi mishe. Ila hata Sasa natumia ka-IST tu, hayo ma-prado baadae Sana huko.
Ndani ya miaka minne tu nikajikuta karibu ya mil 80(of course nilitumia mil 78) kwenye kujenga na zaidi ya mil 80 kwenye kuanzisha hardware.

Hivi Sasa hardware ndio inaendesha kila kitu changu na inalipa sana tena Sana. Hivyo nipate tender nisipate mambo ni byeeee.

Story itakuwa ndefu Sana, Ila ACHENI UJUAJI UBAHILI UNALIPA SANA.
ACHENI KULA BATA BILA KUWA NA MIPANGO

Next project ni hii dream house(namba mbili), location itakuwa Tegeta - wazo.
Hii natembea nayo kila mahali hadi kitandani ninayo, soon inazikwa kwa ground.

Architect ni mtaalam vantano, yupo sana kule IG, haikuwa yangu Ila niliipenda sana. Soon, soon.....

View attachment 1771255
unajibana halafu unakufa unawaachia washenzi watumie mali zako
 
vitu vya msingi ni gani mkuu,, uyo jamaa kasema tujibanr kwenye kula sijui uwe na kipatao cha milioni mbili kwa mwezi ukae chumba cha elfu60 uko mpiji magohe ,,,

Binafsi siwezi kuwa milion alfu nianze kula maugali Aaaagr Bora ninyongwe[emoji1781]

me nikipokeaga mshahara wangu wa laki3 kwa muhindi lazima kwanza niende pale marrybrown napiga kuku chips 12,500/= alfu kila siku lazima nipigr juice ya tende pale buguruni,

hela ikiisha mwezi nao unakuwa umeisha marufuku mshahara wangu kukutana mfukoni
Marufuku mshahara wangu kukutana mfukoni[emoji1787][emoji1787]
 
Mabeki 3 hapana asee wanashika mimba kirahisi kama simbilisi. unamlala sku1 na mimba inaingia hapo hapo. na hakunaga beki 3 tasa.[emoji23][emoji23]
Hivi watu mnawaza nn mnapoandika[emoji1787][emoji1787]
Wanashika mimba km simbilisi[emoji1787][emoji1787]
 
Ukitaka kuruka ruka peke yako, ila ukitaka kuruka MBALI zaidi ruka na WENZAKO,
nakazia tu neno lako ulomjibu jamaa kuwa Wabongo hautujui
 
Huo ndio ukwel , mbinu ya utajili ni ubahili
 
Nilichojifunza mimi katika maisha,ubahiri nao unakuachia makovu mengi tu,ambayo ukiishakuwa tajiri yanakuwa hayafutiki,mfano watoto wanakuwa wamepata elimu duni,wamekua bila mlo kamili,n.k
 
Back
Top Bottom