Mbivu na Mbichi za kuzalishwa ukiwa bado ni Mwanafunzi wa Chuo

Mbivu na Mbichi za kuzalishwa ukiwa bado ni Mwanafunzi wa Chuo

Kuna wengine wanawishi kuzalishwa.. sio kama wanazalishwa kwa bahati mbaya ila tu wanataka wenyewe..
Kipindi nikiwa 4th yr nilitamani na mm nipate mtoto kwani marafiki zangu wengi walikuwa Wana mimba nawengine wamezalishwa..
Kidogo nami nilitaka kuhamasika[emoji16]
Ila nilikosa mtu WA kunitongoza...
Ila lait kama ningelipata mtu wa kunitongoza na nikamridhia huenda na mm ningezalishwa mapemaa saiv ningekuwa na watoto
N.B wale marafiki zangu waliozalishwa kipindi wapo chuo wachache wameolewa na hao hao waliowazalisha na wengine wanalea watoto wao ki mpango
wao..
Km wanaweza ku afford malezi kwa hao watoto pasipo shida, basi hakuna tatizo.
 
Kuna ex wangu kazalishwa mwaka jana mwishoni ilibidi mwaka huu ndio amalize chuo...sahivi yupo tu kwao kazaa kwa sababu ya rafiki yake wanaitana BF forever(hahaha) kazaa naye akazaa anataka watoto wao wawe umri sawa.

Kabla ya kuzalishwa alinambia hizo habari nikamkataa ndio akaja ni hiyo surprise.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka had machoziii, aaah
 
Sio kweli
Nimefundisha kwa kujitolea kuanzia 2020 mpaka 2023 ......
2020-2021 secondary shule za sekondary 3 na 2022-2023 shule za msingi mbili.

Na nilikuwa nafundisha table(Home) teaching ya kumfata mtoto nyumbani.

Hunidanganyi kitu kuhusu mazingira ya kayumba tena nimefundisha dar na kwa taarifa yako primary kuna ela za hapa na pale kuliko secondary.

Endelea kujidanganya na kuwadanganya watu.
 
Kwa mabinti au wanawake, matokeo yanaonekana mapema, ndo maana rahisi kuona hivyo.

Ila vijana na wanaume ndo wanaharibikaga mazimaaa.
Wanaharibika niini hao wanaume? Bangi pombe umalaya wizi au ugasho
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi kuanzia kidato cha tano na Sita wanadhani Maisha ya Chuo ni ya Starehe sana bila kujua undani wake.

Baadhi ya wanafunzi huenda Chuo wakiwa na matumaini makubwa sana ya kutimiza ndoto zao.

Lakini Ndoto hizo hukwamishwa na vitu vingi hasa kwa wale wenye tamaa na pupa.

Kwa kuanza na watoto wa kike ambao huwaona dada zao wamemaliza Chuo na kurudi nyumbani na watoto hutamani na wao wafanye hivyo bila kujua madhara yake.

Mara nyingi wanapoanza Mwaka wa Kwanza huwa ni wanafunzi wapole na watiifu.

Lakini baada ya Muda kidogo makundi hujigawa na kuanza kuonyesha tabia zao halisi.

Mara mtoto wa kike anajikuta amenasa mimba kutoka kwa mtu asiyemtarajia, anaishi na mimba kwa kumficha mzazi wake hadi anajifungua.

Changamoto katika hilo huanza pale atakapokosa matunzo kutoka kwa mhusika aliyekutana nae Chuo.

Kiwango cha masomo kinashuka, maisha huanza kuwa magumu na badala ya kuzingatia masomo na kutafuta fursa za ajira unazingatia malezi malezi zaidi.

Wazazi wanashindwa kupata kile walichokitarajia kutoka kwa mtoto wao kutokana hizo changamoto anazokumbana nazo.

Mnachopaswa kukifahamu watoto wa Chuo hao watu mnaokutana nao Chuo tayari walishadanganya wanafunzi wengi waliopita hapo.

Mnapaswa kukumbuka kuwa nyie sio wa kwanza. Umakini unapaswa kuchukuliwa mapema zaidi.

Maisha ya Chuo ni kusoma na kutafuta Fursa na sio kulea watoto.

Ingawa kuna wachache waliofanikiwa baada ya kupambana sana.
Wrong heading haya maneno ndio yanayowafanya dada zetu/wadogo zetu/mama wadogo zetu wanajisikia vibaya sana wakijifungua kutokana na heading km hizi kuzalishwa,mpe heshima mzazi at least call it kujifungua mfanye anaemleta kiumbe hai nae aone thamani ya kujifungua msimfanye km hastahili kuishi dunia hii.
 
Wrong heading haya maneno ndio yanayowafanya dada zetu/wadogo zetu/mama wadogo zetu wanajisikia vibaya sana wakijifungua kutokana na heading km hizi kuzalishwa,mpe heshima mzazi at least call it kujifungua mfanye anaemleta kiumbe hai nae aone thamani ya kujifungua msimfanye km hastahili kuishi dunia hii.
Sawa
 
Back
Top Bottom