Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

[emoji16][emoji16][emoji16] noma sana...ila ndio wazuri bwana sio wasumbufu...unaweza kutoka kazini ukapita zako baa kupiga maji bila hofu maana unajua hata usipokuwepo watu watakula tu
eti unashukuru ili ukitoka kazini upitie wapi?

asee ule huko huko hili nilichopika tutakula na wanangu tu.
 
Mimi ni moja ya wale wajuba wasiopenda kula mitaani iwe hotel,cafe,bar,pub,nk sehemu yeyote wanayotoa huduma ya chakula sio mpenzi wa kula sehemu hizo na hii n kwasababu sipendi pikiwa chakula nisichojua kimeandaliwaje,kimepikwa ktk hali gani,nk nk (sababu ni nyingi).

Mimi ni moja ya watu ambao huchelewa sana kurudi nyumbani kutokana na kazi zangu lakini hii hainifanyi niache kupika kwasababu moja ya vitu nivipendavyo chini ya jua basi kupika ni mojawapo ya vitu hivyo.

Unajua kuna watu humu tunawasiliana sana huwa nikirudi home naweza mwambia ngoja nipike kidogo basi wanaishia kucheka na kuniona muongo sazingine wananikubalia ila hawaniamini kbsa kama napika.

Leo nataja mboga zangu pendwa ninazo penda zipika ninapokua nimerudi home,hizi ni baadhi tu ya zile za chap chap ambazo ndani ya dk.10-20 nishaivisha mzigo upo mezani tyr kuelekea tumboni.

1. Mboga ya nyanya

Hii mboga naiita hivi kutokana nyanya ndio kitu pekee kilichotawala hii mboga.

Mahitaji yangu ni:
  • Nyanya
  • Hoho
  • Kitunguu maji
  • Kitunguu swaum (hiki hakikosekan kwenye friji huwa kipo standby maana hamna mboga napka ikose hii kitu hakuna)
  • Tangawizi (niliyoparua) hiii pia ipo standby kwa friji haikosekani maana naitumia ktk kila kitu ninachopka chini ya jua
  • Karot (nakwangua kdg na nyingine nakata kata)
  • Viungo vya pilau (vilivyosagwa)
  • Pilipili mbichi
Huo mchanganyiko naanza kuupika kama mboga zingine naanza kitunguu maji ilaa sisubri mpk ktunguu kiwe brown nakoroga in 1min natia tangawizi,nakoroga naleta karoti zangu zile zakukata kata + hoho (naweka pamoja) nafunikia kama dk kadhaa nakuja naweka nyanya + karoti zile zakukwangua naweka pamoja nakoroga then nafunika baada ya muda kidogo nakuja namalizia kile kitunguu swaum changu na viungo vya pilau masala+ ile plipli yangu kisha nakoroga mboga naifunikia, in 5min nikifunua nikipga mwko kona mbili tatu linatoka sotojo moja tamu sana. Chumvi mimi huwa nawekaga kule mwanzo kabisa wakati wakukaanga vitunguu.

Hii mboga nakulaga nayo ugali mkubwa hata mtto mdogo anaweza asivuke. (ni tamu sana na ni simple sana)

2. Mboga ya Mayai

Hii mboga ya mayai nadhani n mboga ninayoila sana chini ya jua kuliko mboga zingine nadhani n kwasababu ya utamu wake na addiction yangu na mayai kwakweli hata kama n kitambi nahisi hii mboga ndio chanzo cha kitambi.

Mahitaji

Ni yale yale na vile vile kama hapo juu kwenye mboga ya nyaya ila ninapopika mboga ya mayai huwa siweki masala za pilau so ktk mahtaji ondoa pilau masala ila vingine vyote viache kama vilivyo.

Jinsi yakuipika hiii kuna style zangu mbili ambazo napenda

style 1

Nikishaandaa mboga yangu kama nilivyoandaa mboga ya nyanya pale juuu ikiwa jikoni navunjia mayai yangu idadi ninayojiskia kisha nakoroga mpk yale mayai yaive mchuzi wa nyanya nao ukauke.Mboga tyr.

style 2

Napika mboga yangu kama mboga ya nyanya kule juu ila ikifka muda wa kuweka mayai,nakaanga pembeni mayai yangu yenyewe kama yenyewe yakiwa tyr nayaweka kwenye sahani nayakata vipende vidogo vidogo kisha vile vipande vyote namwagia kwenye ile mboga yangu,inakua kama nakula nyama mzeee kumbe n vipisi vya mayai,daah tamu sana na ugali.

3. Dagaa

Bana mimi ni moja ya wale raia ukiwalisha dagaa kila siku ndani ya wiki/mwezi/mwaka mzma hawachoki wala kukinai kila siku hii mboga n kama mpya kwangu kutokana na mapenzi yangu kwa dagaa nmejikuta jikon dagaa hawakauki ila sasa dagaa wengi walio tyr n wale wa mwanza wale wanaokua tyr wamekaangwa.

Mahitaji

  • Nyanya 1
  • kitunguu maji
  • karoti (zakukata kata + za kukwangua)
  • hoho
  • kitunguu swaum
  • tangawizi
  • pilipili
Wakati wakupka kama kawaida naanza na kitunguu changu maji,sisubr kiwe brown naweka karot + hoho nakoroga then nakuja naweka dagaa zangu + ile karot ya kukwangua kwa pamoja na pili pili yangu nakoroga mpk viungo vyangu karot na hoho nione vinakarbia iva kisha mwsho namalizia na ile nyanya yangu 1,nyanya hii nmeiweka mwsho mana haihelewi kuiva nikipga mwko mizunguko miwili mitatu mzgo unatoka unameremeta kbsa. Mboga tyr kuliwa na chakula cha siku hyo.

4. Kachumbari

Mahitaji
  • Nyanya mbichi 1
  • Kitunguu maji
  • Karoti
  • Hoho 1
  • Tango
  • Parachichi 1
  • Limao
  • Pilipili

maandalizi n simple kama yeyote anavyoweza andaa basi ikikamilika namix safi kabsa kitu tyr kuliwa na chakula cha siku husika.

5. Mtindi

Hiii kwangu husimama kama mboga na mara zingine husimama kama chakula kbsa maana kuna siku nakunywa nalala yani friji ikose kila kitu ila sio pakti ya mtindi.

Hizi ni zile za chap chap ambazo at any time naweza ziandaa mtu akala chakula akahisi kala 5 star hotel kwasababu sio masihara msosi ninaopenda kuula huwa najua upika kwa ustadi ule unaokidhi vigezo vyote kuliwa na raia mwenye njaa yake mjini.
nmekwelewa sana mkuu. japo haya mayai ya kisasa yana madawa sana asee mm siyapendi. nkimaliza kusoma hii thread nategemea nitaanza kupenda kupika mana spend kupika asee.!!
 
[emoji16][emoji16][emoji16] noma sana...ila ndio wazuri bwana sio wasumbufu...unaweza kutoka kazini ukapita zako baa kupiga maji bila hofu maana unajua hata usipokuwepo watu watakula tu
Haha...
Nikajua ukipitia kwenye maombi ya jioni, Khantwe bwaaana.!
 
Nikila dagaa wa kukaanga nasikia kichefucuefu mboga yangu Bora ya muda wote ni maini roast na ugali.


Maini nayo siyo ya kula mara kwa mara kwa mtu mwenye kujali afya yake.

Ini la mnyama ndipo chujio na sumu za mnyama huishia.
Ndiyo maana kwa nchi zilizoendelea nyama za ndani huuzwa bei ya kutupwa isipokuwa huku bongo ambapo uelewa wa jamii kuhusu maswala ya lishe salama upo chini sana na watu hawana utayari wakujifunza na kukubali kubadili tabia.
 
eti unashukuru ili ukitoka kazini upitie wapi?

asee ule huko huko hili nilichopika tutakula na wanangu tu.
Haina tabu...cha muhimu ni kuwa hautanikera na simu za kila baada ya dakika mbili kuniuliza niko wapi
 
Juzi nime advance kidogo nimetengeneza desert ya banana cake. Viuingo vyake sasa

Ila ilitoka poa
IMG_20200929_210047_765.jpg
 
Maini nayo siyo ya kula mara kwa mara kwa mtu mwenye kujali afya yake.

Ini la mnyama ndipo chujio na sumu za mnyama huishia.
Ndiyo maana kwa nchi zilizoendelea nyama za ndani huuzwa bei ya kutupwa isipokuwa huku bongo ambapo uelewa wa jamii kuhusu maswala ya lishe salama upo chini sana na watu hawana utayari wakujifunza na kukubali kubadili tabia.
Nawazaga Kama wewe. Yaani nikika maini nakuwa na wasi wasi sana
 
Pilau simple mkuu tena siku hizi haya masalla ndio yamerahisisha kila kitu,pilau ilikua gumu zamani kabla hatujajua kusaga viungo yani unaweka kimoja kimoja sijui mdalasini,iliki,binzari nyembamba yani maviungo n mengi kiasi kwamba nilikua sielewi naanza kipi namalizia kipi,ila sasa hivi All in ONE Ukijua pika wali tu basi na pilau umemaliza.

zaidi zaidi ujifunze mbwembwe za kutoa pilau tamu kuanzia machoni mpk mdomoni,hapo ndio kuna ufundi wakujua mpk aina ya mchele wa kutumia hv hv unaweza ishia toa pilau ugali... [emoji1787]
hv hz pilau masala si zina preservatives?? huon kwamba jins unavoweka viungo vingi ndo utakuwa unakula sumu nyng sana ? mfano preservatives kwny masala,kwny mtindi, nyanya enyewe inapigwa sana dawa huko shamban....how do yu ensure that ur body get natural food?
 
Nikila dagaa wa kukaanga nasikia kichefucuefu mboga yangu Bora ya muda wote ni maini roast na ugali.
hicho kichefu chefu ni mara moja au mara zote ulizojaribu kula?

ni sehemu 1 au ni sehemu tofauti tofauti,mara nyingi kichefu chefu

inaweza sababshwa na mafuta yaliyotumika pikia hao dagaa ndio sababu..
 
Nawaogopa sana wanaume ambao they can take a good care of themselves, wengi huchelewa kuoa ama wasioe kabisa..
Imagine juzi job kuna wakaka tulikuwa tunabishana nao bei ya nyanya sado..! 😂 😂
ni raha sana najua wajua na najua vile unapenda pia 😂
 
hv hz pilau masala si zina preservatives?? huon kwamba jins unavoweka viungo vingi ndo utakuwa unakula sumu nyng sana ? mfano preservatives kwny masala,kwny mtindi, nyanya enyewe inapigwa sana dawa huko shamban....how do yu ensure that ur body get natural food?
mkuu pilau masala si unatengeneza wewe mwenyewe? unanunua viungo unasaga.
 
Wanaume wengi wa kibongo hawanaga mazoea ya kujipikilisha wapo ila ni wachache kutokana na mifumo ya malezi isiyo sahihi ya kuzani mtoto wa kiume hatakiwi kuwa mazoea na jikoni kumbe siyo sahihi hata kidogo.

Wanaume wengi wa kibongo wakishapata exposure kwa kwenda kusoma au kufanya kazi nje ya nchi ndipo hujifunza na kuona wanaume wenzao wakijipikisha wenyewe kwa wepesi nao wanaona kumbe Mwanaume kupika ni jambo la kawaida na la kutokulionea aibu!
 
Back
Top Bottom