Kuna chama kinaitwa ACT, chenyewe kinafanya siasa za kutaka kusifiwa na CCM. Wenyewe huwa wanasema wanafanya siasa za masuala, lakini ukiwatazama kwa undani ni kama wanafanya siasa za kuwaridhisha CCM. Wakati CDM hawajaanza mikutano, wao walikuwa wanapitapita sehemu mbalimbali wakisema wanafanya siasa mbadala, lakini toka CDM walipoanza na wao kuona bado CDM ina wafuasi wengi, wamepoteza furaha maana wanaona CCM inataabishwa.
Hivyo vyama vingine viko kimya vinasuburi wakati wa uchaguzi kutumiwa na CCM, na wengine huwa wanakuja na utapeli kuwa vyama vya upinzani viunganishe nguvu ili kuitoa CCM. Na CDM wakigoma utasikia wanailaumu CDM eti haitaki kuunganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani ili kuitoa CCM! Kibaya zaidi CDM ikikosea ikakubali kuungana navyo wanaanza kutumiwa na CCM ili kuvuruga upinzani.