Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

CCM wanasema wanalinda huo wanaouita muungano kwa gharama yoyote. Kwa mantiki hiyo watafilisika muda si mrefu. Nchi fukara kama Tanzania haiwezi kukaa nchi vamizi milele. Ufaransa ilivamia Algeria ikabaki karibu miaka 140, lakini mwishowe ilishindwa majeshi yake yakatimuliwa. Marekani ilivamia Afghanistan ikakaa miaka 20, mwishowe ilishindwa majeshi yao yalitimuliwa. Majeshi ya vamizi Zanzibar hayawezi kubaki muda mrefu.
 
Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekuwa hawaridhishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawahi sema muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Pia nakumbuka awamu ya 4, Rais akiwa Kikwete kuliibuka wimbi kubwa sana la wanaharakati kutoka Zanzibar wakiongozwa na jumuia ya UAMUSHO wakidai Zanzibar inatakiwa kuwa huru eti kisa viongozi wao wanachaguliwa kutoka Tanganyika.

Lakini jambo la ajabu awamu hii ya sita ni kama hakuna tena hizi harakati za kuvunja muungano wetu mtukufu sasa najiuliza je, shida ilikuwa nini kwa hizi harakati na imekuaje awamu hii zisisikike tena? Au ulikuwa ni unafiki tu wa wanasiasa na sasa hivi wameona huu muungano unawanufaisha na wao!

Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wana manufaa kuliko Watanganyika hivyo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.

Mzanzibar ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika wakati Mtanganyika hana hiyo haki Zanzibar. Je, nani hapo ananufaika? Nawaomba tena Wanzanzibar waache unafiki huu muungano wao ndiyo wanufaika.

MUUNGANO UDUMU MILELE.
Kwa hiyo unataka Mzanzibari Adai Zanzibar huru toka kwa mzanzibari?
 
Alieniambia mimi kuwa wewe ni shoga ni wewe

Kwani Mimi ni Yesu ?

wjd-billboard-born-gay.jpg
 
Waliokuwa wanapiga kelele sasa hivi wako mezani
Tatizo bara mkiwa madarakani mnawabania sana,, yaani mikopo yote mnatumia kwenu tu, misaada yote,,,
Wabara tuacheni ubinafsi,,, hata yesu amesisitiza upendo,
Ubinafsi ni uroho,,, mambo ya kung'ang'ania madaraka tuache ,, cheo hauzikwi nacho,,
Sio nyie mkikamata madaraka hamtaki kuachia halafu vyeo mnapeana tu, [emoji23][emoji23] wenzenu wakihoji, mnawambia, "tulieni, nyie hamkusoma"
Sasa mtulie mfundishwe kuwa, uongozi ni kuongoza watu na sio kuwatawala,,,
Na kwamba vyeo ni dhamana
 
Sasa unataka wadai uhuru gani wakati nchi inatawaliwa na wazanzibari, subiri siku akitawala mbara ndio wataanza harakati upya tena
Wabara tumekwama sana , kwanza mwaka 67 watu walitaifishwa nyumba zao, bila sababu kosa lao walikua, matajiri
Pili 84,watu wenye ukwasi wakapata heka heka eti walanguzi
Bado kina Bashite, sabaya wakawa wanawapora watu wenye utajiri,, eti wanafanya money laundry,,
Kiufupi wabara hatuna ustaarabu wa uongozi, kwa walio wengi
Tujisahihishe,, tuache roho mbaya na ubinafsi[emoji3][emoji3]
 
Wabara tumekwama sana , kwanza mwaka 67 watu walitaifishwa nyumba zao, bila sababu kosa lao walikua, matajiri
Pili 84,watu wenye ukwasi wakapata heka heka eti walanguzi
Bado kina Bashite, sabaya wakawa wanawapora watu wenye utajiri,, eti wanafanya money laundry,,
Kiufupi wabara hatuna ustaarabu wa uongozi, kwa walio wengi
Tujisahihishe,, tuache roho mbaya na ubinafsi[emoji3][emoji3]
hii ni laana
 
Back
Top Bottom