Mbona kama tatizo la wateja katika benki kupata noti pungufu wanapotoa hela linaota mizizi?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Salamu Wakuu,

Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers

Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao

Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw

Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?

Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X

1714121017383.png

"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.

"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.

"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.

"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
 
Attachments

  • 1714121032687.png
    1714121032687.png
    266.7 KB · Views: 6
Ndugu wasomaji. Kisa hiki ni cha kubuni tu, hakihusiani na tukio lolote la ukweli ndiyo maana halijatajwa jina la bank.

N.B: Count your money before you leave the counter.
Mkuu hata karibuni lakini ni kweli ma tellers wengi kwenye benki siyo waamifu. Mimi mlimani city 2018 walishanipunja kama elfu 60 hivi nikapotezea. Nilirudi zangu likizo hela yangu ya kubeba box iliniuma siyo kivile.
 
Siwatetei, bank ni wezi, ila huyu amezingua kwa kutoitaja hiyo bank.
Mimi bank waliwahi pita na hela yangu ya kwenye account, ila waliirudisha. Walidhani nisingetambua
 
Salamu Wakuu,

Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers

Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao

Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw

Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?

Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X

"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.

"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.

"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.

"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
Hii iliwahi kunitokea ila ni musa mrefu sana.niliona elf 20 zimepungua kwenye milioni.nikashangaa ila nikapotezea
 
Kuna siku nilienda kupataa huduma benki.
Sasa mbele yangu alikuwepo mama mmoja alitoa milioni 5.
Akawa anataka kuhesabilia palepale, tellor akasema zimetimia, haamini nini wakati ameshuhudia akihesabu kwenye mashine!
Mama akang'ang'ania lazima azihesabu kwa sababu ameshawahi kupigwa katika withdrawal iliyotangulia. Wateja nao wakaanza kuongea ongea kwamba anawachelewesha.

Ndio wahudumu wakamwambia aingie kichumba fulani akahesabilie.
 
Back
Top Bottom