Mbona kama tatizo la wateja katika benki kupata noti pungufu wanapotoa hela linaota mizizi?

Mbona kama tatizo la wateja katika benki kupata noti pungufu wanapotoa hela linaota mizizi?

Unamwambia zihesabu. Atafungua na kuhesabu hana mamlaka ya kukataa. Pale pameandikwa mteja hesabu hela zako kabla hujaondoka kaunta ni haki yako. Na akikwambia sogea wateja wemgine wahudumiwe muoneshe hilo tangazo kuwa uhakika kabla ya kuondoka kaunta.
Okay! Hapa nimekupata.
 
Ile kudondosha noti ni taaluma kama taaluma kama nyingine, mwenye hela huwezi kuona inapodondoka ila utashuhudia mashine imehesabu kiasi kamili ambacho wewe umeona, lakini ukicheki kiasi ulichopewa unakuta pungufu.
Ni sawa na kuchezea karata tu ukizoea kuishi nazo.
 
Niliwahi kwenda kutoa pesa kwenye mashine.
Nina tabia ya kuhesabu kila nikitoa.
Nilitoa sh.400,000/=, nilipohesabu nilikuta sh.250,000/=.
Niliingia ndani nikawafafamisha. Baada ya siku mbili walinirudishia zilizopungua.
Jitahidi kila unapopewa bunda lililofungwa ujiridhishe.
Akitumia mashine jiridhishe kwa kuangalia.

Mmh..kwamba hadi ATM ZINAIBA????
 
Huko bulk cash room kuna kaunta pia.
Nishatoa pesa huko.
Hakuwi kama sebuleni.
Usimfikirie mtu usiyemjua unavyofikiri binafsi yako.
Sasa point yako nini? Kwamba bulk cash room hawajesabu hela wanakupa tu? Tusipoteze muda. Bottom line mteja ana haki na anatakiwa kuhesabu hela zake kabla ya kuondoka. Ziwe 50,000 au 50,000,000.
Ukiamua kuchukua hela bila kuhesabu usilalamike ukiibiwa umetaka mwenyewe.
 
We

Wenye pesa huwa hawahesabu noti ndugu.
Wakisha andika cheki pesa inaletwa nyumbani.
Wanaohesabu pesa ni sisi wenye vipesa kichele.
Benki kuna mabanda ya pesa yamesha hesabiwa na kufungwa na rubber bend.
 
Salamu Wakuu,

Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers

Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao

Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw

Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?

Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X

"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.

"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.

"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.

"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
Wengi wanaokumbana na hali hii sio wazoefu wa mipesa mingi, hivyo kwao kuhesabu hata (mil 1 tu) baada ya kuidraw kbl ya kueguza kisogo anaona tabu
 
We

Wenye pesa huwa hawahesabu noti ndugu.
Wakisha andika cheki pesa inaletwa nyumbani.
Wanaohesabu pesa ni sisi wenye vipesa kichele.
Benki kuna mabanda ya pesa yamesha hesabiwa na kufungwa na rubber bend.
Still sijui point yako ni nini. Uzi huu watu wanalalamika kuibiwa hela zao benki. Ndio hao matajiri wasiohesabu pesa? Okay nilijua ni masikini wenzangu ambao tunatakiwa kuhesabu pesa.
 
Hata kwenye kufanya deposit, unaweza toka umehesabu pesa zako zote zimekamilika safi, ukifika pale wanakutia wenge kwanza, andika elfu 10, zipo ngapi 5 ngapi 2 ngapi na 1 ngapi. Huku wanapima wenge lako. Ukimaliza ukampa ahesabu atakwambia labda kwenye million, elfu tano haipo. Hapo inabidi uongeze
Chai hii
 
Nilikuwa nimeihesabu 7,000,000/- mara mbilimbili. Nikaenda ku-deposit pale CRDB Tunduma kule chini Customs. Wakanipiga laki.

Nikaja tena kupigwa 15,000/- CRDB Tegeta. Nilitoa 5,000,000/-wakanipa notes za 5,000/- nimeenda kuziweka NMB zikapelea. Na zilikuwa zimefungwa ile mikanda ya plastic.

Huu mtindo upo sana.
 
Back
Top Bottom