Salamu Wakuu,
Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers
Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao
Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw
Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?
Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X
"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.
"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.
"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.
"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
Kiuhalisia watu wa bank ni wezi sana, usipokuwa makini kupigwa ni nje nje.
Nakumbuka kuna kipindi fulani nilikuwaga Mafinga hapo hapo kama ambavyo mwenye Iki kisa alipokuwa.
Nakumbuka nilienda NMB kuweka hela, ilikuwa mida ya mchana hivi. Nilivyokamilisha zoezi, nikarudi zangu maskani. Inaonekana kuna shida ilitokea, jamaa (teller) akanipigia sana simu ila hakunipata. Mida ya usiku nilivyorudi hewani, nikapata ujumbe kwamba namba fulani ilijaribu kukupigia. Nilivyoipiga Ile namba, akapokea yule teller, akaniambia kesho yake niende tena pale bank. Kesho yake mapema wanafungua Niko pale. Yule teller akanivuta pembeni na kuniambia
"Jana zile hela ulizoleta tulizihesabu vibaya, hivyo nilikuzidishia laki 3. Nilijaribu sana kukupigia simu nikakukosa hivyo nikaikata Ile lakini 3 iliyozidi"
Baada ya kuniambia kauli hiyo, akatoa slip akanipa. Kuiangalia naona imejazwa upya kwamba kiasi fulani ( pungufu ya lakini 3) kimewekwa kwenye account yangu, alaf muwekaji wa hiyo hela ni Mimi (paliwekwa majina yangu) kisha akaweka na sahihi yangu (yule teller).
Ikabidi nimkalishe chini vizuri na kumwambia kuwa Ile hela sijaokota Wala sijapewa zawadi kusema kwamba nitoke nazo home bila kujua ni kiasi gani. Zile hela zilipofikia Ile amount niliona sio vyema kuzitunza home hivyo nikaamua kuziweka bank, na ndio maana nilifungua account mpya ya saving na kuziweka, hivyo amount niliyoandika ndio sahihi.
Teller akanibishia, mwisho wa siku tukaenda kwa meneja wake. Inaonekana scenario meneja alikuwa anaijua so tulivyofika akamwambia "Boss huyu ndio yule mteja ambae nilimzidishia lakini tatu kimakosa"
Nikamkazia tena yeye na meneja wake kwamba waangalie tena walipozidisha hela, ila kwangu hela nilizoweka zilikuwa sahihi. Teller anazidi kukomaa kwamba Mimi ndio nilikuwa mteja wa mwisho kuhudumiwa na yeye, hivyo wakati wa kufunga hesabu jioni ndio akaona hiyo pungufu ya 300k, na alivyochek kwenye CCTV camera, akaona kosa limetokea kwangu.
Hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kusikia CCTV camera zinaweza kuonesha clear details za kwenye screen ya computer. Anyway, tukiwa tunaendelea kubishana, yule teller akaitwa na bi mkubwa mmoja ambae nae ni mfanyakazi wa pale bank, hivyo akaniachia na meneja wake. Baada ya kama dakika 10 akarudi. Kumbe Jana Mimi nilivyoondoka, kuna mteja mwingine alikuja na kuwithdraw 150k, ila yule teller kimakosa akaandika kwenye mfumo kuwa mteja ameweka 150k, maana yake amempa cash akaondoka alaf akamuongezea na 150k kwenye account, hapo ndio loss ya 300k ilipotokea. So yule bi mkubwa aliyemuita ndio aligundua hiyo mistake.
Baada ya kujua kosa lilipo, jamaa anaanza kujichekesha na kuomba msamaha. Namuuliza siuliniona kwenye CCTV camera kwamba hela hazikuwa zile nilizoandika? Anacheka tu. Menejea akaomba twende tukaongelee nje.
Siku ile ndio niligundua jamaa wanaweza kutuibia bila sisi kujua, maana walifoji hadi sahihi yangu, na pia sikupata notification yoyote kwamba kuna hela imeingia au kutolewa kwenye account yangu. Kibaya zaidi walishafabricate ushahidi wa uongo kuback up theory yao.