Mbona malalamiko mengi kwenye nyumba za kuficha Bati (Hidden Roof), Mafundi wanakosea nini hadi zinavuja?

Mimi mwenyewe hapa nina msala wa kubadili paa la nyumba. Mafundi wengi hawawezi upauaji huu. Fundi wangu kanitia hasara sana
pole ulitaka uende na fashion
kwahiyo mvua ikinyesha masufuria na mabesen yana kuhusu😅😅
 
Acha iendelee kunyesha tujue wap panavuja
 
ni sahihi kabisa.

watu wengi wanakurupuka tu kubadilisha nyumba za kawaida inakuwa hidden wasichokuwa hizo nyumba zina formula yake ambayo inaanzia toka unaanza msingi. wengi wanafikiri hidden inahusu kupaua tu ambayo sio kweli hidden inahusu ujenzi wa nyumba nzima kutokea msingi.

na wengi wanadai wanataka hidden ili waokoe pesa wakati kimahesabu hidden inatakiwa iwe ghali zaidi ya nyumba ya kawaida maana kuna ile mifumo ya kupitisha maji kutoka juu inakula material nyingi.

ukiona unajenga hidden na unabaki na chenchi ndugu shtuka mapema, hapo umepigwa chukua hiyo.
 
Ukimwaga zege sio contemporary house bali ni ghorofa
Nyumba ambayo utamwaga zege juu msingi wake, na nondo ni tofauti na contemporary house
Usiwe unapenda shortcut
Umemjibu vizuri kabisa .msingi wa kuweka silabu juu huweiz kuwa wa kitoto hata kidogo
 
Umemjibu vizuri kabisa .msingi wa kuweka silabu juu huweiz kuwa wa kitoto hata kidogo
Nimejenga nyumba kama mbili za namna hiyo amna kuvuja hata tone , na kwa sasa kuna technology mbali mblai za kupaua kwa kutumia bitumen membrane
 
Maandalizi ya hidden roof unaanzia chini kwa kuweka miundombinu ya kupitisha maji ya mvua ila wengi wanajenga kikawaida alafu wanakuja kubadili gear anagani hapo ndipo tatizo linapoanza.
 
Kama umepata fundi makini utajivunia mjengo wako na furaha tele.
 

Attachments

  • FB_IMG_1695367754032.jpg
    135.8 KB · Views: 36
  • FB_IMG_1695367746245.jpg
    150.5 KB · Views: 34
Upo sahihi mkuu, na mafundi tunaojua kuzijenga tupo wachache sana tz, na kingine kuna matilio yanayotumika mle, mafundi wengi hawayajui au, wanayajua ila kuyatumia ndio mtihani.
 
Wewe ni wle wale tu! Bati halichimbiwi hata kidogo
 
Kweli kabisa, tatizo linakuja pale anaehitaji kujengewa hana ujuzi wowote anakuja kushtukia anapata tatzo/matatizo badae.
Na wengne nyumba ni ya paa la nje sasa anakaribia kufunga mkanda anamwambia fundi nataka hiden roof ndo changamoto zaid hapo
 
Hapo kwenye tiles mkuu umenikumbusha nyumbani ,chooni na bafuni kwa bimkubwa .Fundi aliweka tiles kama mtoto anachezea matope.Tiles hazieleweki mistari katapakaza masimenti kila mahali .Tiles mara sehemu nyingine zimevimba kama jipu.
 
Kuna fundi namfahamu na namkubali sana na alishanifanyia kazi kadhaa ila za kawaida, sasa home kwangu nilijenga chumba kimoja self kwaajili ya wageni wangu na ni Hidden roof, najuta aisee, ni chumba kimoja tu lakini ngoma inavuja hatari. Mpaka sasa nimemaliza zaidi ya 200k kurekebisha ila bado anachemsha.

Sitaki tena huu upuuzi wa Hidden Roof kwakweli.
 
Mimi ni fundi wa kupaua na kupiga dali na showcase natengeneza nambari zangu za simu. 0621131880&0743744445
 

Attachments

  • IMG20231209185221.jpg
    2.6 MB · Views: 23
samahani mleta mada nipo nje ya mada kidogo,mimi ni fundi wa kufunga cctv camera,electric fence,gate motor pamoja na video door bell,kwa mwenye kuhitaji huduma naomba tuwasiliane kwa namba 0622667749 au 0674376787 nipo Dar es Salaam
 
Pole kwa maumivu makali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…