Mbona Rais Samia anaturudisha Dar es Salaam wakati Makao Makuu ni Dodoma?

Vitu vyote hivyo vipo Dodoma, na vingi vilivyokuwepo Ikulu ya Dar vilifungwa au kuhamishwa.

Magufuli alizindua Ikulu iliyokamilika na kusema amehamia rasmi Ikulu ya Dodoma moja kwa moja, na ikulu ya Dar itakwenda kufungwa na kuwa makumbusho ya Ikulu.
Vipi tena sasa kurudi kujichimbia Dar?
 
Kama ameamua kurudisha makao makuu ya nchi kuwa Dsm aseme wazi tu, SSH ana ka unafiki fulani, anafanya maamuzi ili ku please watu tu, ni kheri aseme wazi waache kujenga Dodoma kuliko huo unafiki anaotaka kujaribu kufanya.
Dodoma Wizara nyingi hazina makazi ya kudumu, zinaweza geuzwa kuwa Wizara ndogo
 

Ebu keleleee huko, ww unajua Mh. Rais ana ratiba ngapi Dar, ww unajua karudi Dar kukaa tu kama ww unavyokaa kwa dada yako kaolewa ww unakaa tu hapo kwa shemeji kafanye kazi acha kudumaa kiakili, kila siku Mh. Rais ana ratiba, acha kiherehere
 
Foleni Dar haitaisha, Siku ukikuta imeisha kimbia ujifiche maana kuna shida mahali
Najuwa foleni haziwezi kuisha na foleni za Dar zina mida yake tu sio kwamba foleni 12 hours hapana ni ile mida ya kuingia makazini na kutoka makazini muda mwingine wa katikati ni foleni za kawaida sana unatembea vizuri tu. Ukijuwa timing hukwami Dar. Ndio maana stand kupelekwa Mbezi ni jambo zuri tu shughuli zisambae nje ya mji.
 
Dodoma Wizara nyingi hazina makazi ya kudumu, zinaweza geuzwa kuwa Wizara ndogo
Wizara zote zimejengwa mji wa serikali na wafanyakazi wote wamehamia pale vipi unasema hawana makazi maalumu. Nilienda kufuatilia mambo yangu pale kumejengwa haswa na ukienda unamaliza mambo yako yote sababu wako eneo moja wizara zote.
 
Dodoma Wizara nyingi hazina makazi ya kudumu, zinaweza geuzwa kuwa Wizara ndogo
Poaaa, aseme wazi anairudisha serikali Dsm, anachofanya saivi ni unafiki, kuwa na kiongozi mnafiki ni hasara kwa taifa.
 

Wananchi gani walimpigia kura Magufuli? Kwenye ule uchaguzi ambao aliunajisi kwa kiwango cha kutisha? Jenga hoja zako bila kuchanganya sifa zitakazoharibu hoja zako.
 
Poaaa, aseme wazi anairudisha serikali Dsm, anachofanya saivi ni unafiki, kuwa na kiongozi mnafiki ni hasara kwa taifa.

Dhalimu alipokuwa akifanyia mambo chattle mbona hukulalamika, au hii Id hukuwa unaitumia ww wakati ule?
 
misimamo ya kuruhusu watu kupotezwa nayo iendelee ama? kuminya democrasia nako?
 
Waswahili husema "Kila zama na kitabu chake!" Huenda mwendazake alienda na kitabu chake.
 
Mwendazake alikurupuka!
 
Wizara zote zimejengwa mji wa serikali na wafanyakazi wote wamehamia pale vipi unasema hawana makazi maalumu. Nilienda kufuatilia mambo yangu pale kumejengwa haswa na ukienda unamaliza mambo yako yote sababu wako eneo moja wizara zote.
Basi sawa
 
Haraka ya nini na ikulu huko dodoma inaendelea kujengwa haijakamilika. ?
 
Reactions: ShL
Binafsi sifurahiswi na namna anavyofanya
 
Mji mkuu kwa wajuaji Ni Dar.
Angalia balozi zilipo.
Ila kwa washamba Ni huko huko mnakojua ninyi.
Mbona kila weekend waliolazimishwa kwenda Dom wako Dar?
 
BINAFSI YAKO ULIKUWA UNAONA ALIKUWA SAWA?
IKULU YA DAR INA SECURITY CODES MUHUMU AMBAZO BAADHI HAZIWEZI KUPATIKANA DODOMA,LAKINI TUNAPAHESHIMU DODOMA,
JE UNAONA KULIKUWA PLANI NZURI KATIKA KUYAAACHA MAJENGO MUHIMU SANA YAHARIBIKE NA KUWA NYUMBA ZA NJIWA?
*TUMUACHANI MWENDA ZAKE APUMZIKE KWA AMANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…