Mbona Rais Samia anaturudisha Dar es Salaam wakati Makao Makuu ni Dodoma?

Na Chato ulikuwa mji mkuu wa sangoma au ??
JF siku hizi pumba zinakuja nyingi sana.
Tulieni dawa iwaingie...mlizoea mtu anapeleka Airbus Chato inapaki mwezi mzima kusubiri km boda...
 
Uzi huu naona umefufua #treasury wengi... naona na mkubwa naye yupo.....!kama kawa kam dawa..!safi sana,naona sasa wana breath at least..they smell a air of hope
 
..kwa maoni yangu, GHARAMA za kuhamia Dodoma ni kubwa kuliko faida.

..fedha zilizotumika zingeweza kugharamia mahitaji mengi ya msingi, yanayogusa wananchi wengi kuliko walioguswa na zoezi la serikali kuhamia Dodoma.

Sawa, lakini tayari serikali imeshahama sasa. Haileti mantiki kurudi maana kufanya hivyo hakupunguzi gharama bali kuziongeza zaidi. Wizara zote ziko Dodoma. Na inaeleweka hivyo. Shida inakuwa wapi?

Kwani ilipotungwa sheria kuwa makao makuu ya nchi yatakuwa Dodoma kulikuwa na makosa katika hilo?

Gharama zipo na zitaendelea kuwepo lakini haina maana kuwa sasa viongozi wa juu waanze kurudi kufanya matukio ya kitaifa Dar es Salaam. Kama maamuzi ya kuijenga Dodoma yalipitishwa basi utekelezaji wake uendelee. Serikali ilianza kuhamishiwa Dodoma kuanzia Rais wa tatu, wa nne na wa tano (aliyefanya kazi kubwa zaidi). Sasa “kazi iendelee” iwe na uhalisia maeneo yote muhimu yenye maslahi kitaifa.
 
We kama unapapendaa sana dodoma si uende brasa !! mikelele ya nini - tuache.
 
Mwendazake alikuwa anaapishiwa watu Chato wakati mwingine.
Shida kubwa ni ushabiki usio kuwa na maana. Huenda kuna watu wengi hawakupenda serikali kuhamia Dodoma. Na wengine ni viongozi wakubwa. Hivyo kuona mwendazake amenyamaza milele usistaajabu yanayotokea. Lakini muda ni mwalimu mzuri.
 
Kuhamia Dodoma hayakuwa matakwa ya Watu wengi makini bali yalikuwa ni ya Watu kadhaa na Imani zao za Kipuuzi.

Kuna Mtu nilipenyezewa za chini chini kuwa hakupenda kuishi Ikulu ya Dar es Salaam kwakuwa kuna Miiko Maalum ya Kiutamaduni ( Ushirikina ) aliikiuka ambayo Watangulizi wake wote Wanne ( 4 ) waliikubali na najua hata huyu wa Sita ( 6 ) nae kaikubali.

Binafsi ni Mmoja wa Watu ambao sijaafiki na wala sijapendezwa kwa Serikali nzima kuhamia Mkoani Dodoma kutokana na Changamoto za Kimsingi zilizoko huko.

Mkoa wa Dar es Salaam una Sura halisi ya kuwa Mji Mkuu ( japo nimedokezwa kuwa ) Kimkakati na Kiusalama pia haujakaa vyema na Salama ila kungefanyika Utaratibu wa Kimedani bado ungefaa kuwa Mji Mkuu.
 
Kama ameamua kurudisha makao makuu ya nchi kuwa Dsm aseme wazi tu, SSH ana ka unafiki fulani, anafanya maamuzi ili ku please watu tu, ni kheri aseme wazi waache kujenga Dodoma kuliko huo unafiki anaotaka kujaribu kufanya.
Umeumia sana ehhhh. Na bado, mwenye unafiki alienda zake. Miradi yote upande mmoja. Kisha maenderreeo hayana chama (Ameingia ktk historia kama mnafiki no 1)
 
Bora huyo anafanyia kazi kwenye majengo/ofisi za serikali. Mbona wakati mwendazake anafanyia kazi na kupokea wageni wa kitaifa nyumbani kwake Chato hamkulalamika, na mlikuwa mnasema pote ni tanzania?
 
Ni ghafla kweli, kwakuwa Mwendazake akiwa Dar alikuwa anaota ndoto mbaya, kwenda Dom ikawa ndiyo njia bora kwake na washauri wake. Baadae Dom nako ndoto mbaya zikaendelea, ikabidi nduki to Chettle. Pia huko ndoto mbaya zikamfuata. Dooo ikabidi ashinde barabarani kwenye uzinduzi kuelekea Dar. Mwisho kukawa hakuna namna, ikabidi apae. Maana chanzo cha ndoto mbaya si eneo ulilo pumzika, bali matendo yako. Kama ni maovu haukwepi.
 
Arudi tu dar , Mji wa serikali Dodoma kiwe chuo kikuu. Sababu tuna vyuo vikuu vichache sana
 
Dar ni mji mkuu.dodoma ni makao makuu.acheni majungu jamaa alijichimbia chato mnasema chato pia ni tanzania
Hapana Dodoma ndio mji mkuu wa Tanzania na pia ni Makao makuu ya Chama cha Mapinduz, Dar ni Mji wa kibiashara na mji wa bandari wa Tanzania...
 
Safi wengi wanatoa mchango kishabiki bila sense. Wanalinganisha chato na dodoma. Chatto ilikua nyumbani kwa jpm..sasa dar ni nyumbani kwa samia au anarudisha kazi za rais ikulu ya zamani?
 
Sukuma Gang mwacheni Rais afanye kazi bila bughudha.
 
enzi za meko zimepita dsm ndo kitovu cha nchi hii,kuna rafiki yangu alihamia dodoma kikazi tangu enzi za mwendazake ila naona kila siku yupo Dar kikazi nikajua ni siasa tu kupeleka serikali kwa wagogo ila utendaji wote upo dsm mwache mama ale upepo wa bahari
 
Kwani weye wa Idodonywa,ama mkwamia awamu iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…