Mbona wanajikomba kwa Israel

Mbona wanajikomba kwa Israel

Mchina amekuwa akinunua tech Israel kwa muda mrefu tu, na wala si kitu cha kushangaza.

Mojawapo ya tech hizo ni semiconductors. Kuna wakati Marekani na Urusi hufuata tech Israel, kwanini iwe ajabu kwa Mchina?

Unafahamu hata Intel ni kampuni ya wapi?🤔
 
Mimi MTANZANIA sio Mbongo na Sina mapenzi na China bali nakubali utendaji kazi wao ni hivyo tu. WEWE NDIO MTUMWA WA MABWANA ZAKO ISRAEL
Kama wewe ni mtumwa usidhani wote ni watumwa acha kulinganisha visivyolinganishika, mbona ipo wazi kuwa wewe ni mtumwa wa mchina kuanzia jina unalotumia mpaka picha kwenye profile yako na hapo sijaongelea mawazo yako yenye ukungu
 
Jina mjamaa wa kisasa asili yake imetokana na neno ujamaa wa kisasa ambaye muasisi wake ni mjerumani Great father KARL MAX na picha ya profile ni ya chama cha kijamaa cha kisovieti kwa hiyo mpaka hapo hakuna hata sehemu moja mchina anahusika🤣
 
Swali langu haujalijibu kama ambavyo mimi nimejibu la kwako. Development center kubwa zaidi ya Intel duniani inapatikana Israel, unafikiri ni kwa sababu gani?
Mbona swali lako nimekujibu mkuu . Kuna njia nyingi za kujibu swali Mimi nazifahamu mbili
i, Kujibu swali kwa kutoa jibu moja kwa moja
ii, Kujibu swali kwa kuuliza swali
Swali lako nililijibu kwa kuuliza swali [ Kwa hiyo kwa sababu sehemu kubwa ya kiwanda/kampuni ya Intel ipo Israel basi Israel ndio mmiliki wa teknolojia?].

- kwa hiyo kwa sababu sehemu kubwa ya kiwanda cha I-Phone kipo china basi china ndio mmiliki wa teknolojia ya I-Phone?

- Kwa hiyo kwa sababu kiwanda cha Volkswagen kipo Rwanda Basi Rwanda naye ni mmiliki wa teknolojia ya Volkswagen?

N.B: by the way branch/Viwanda vya Intel duniani vipo nchi za U.S.A, China , Israel, Vietnam, Ireland, Vietnam n.k
 
Kwanini wawe AU wakati wapo Middle East huko siwajiunge na waarabu huko,,kwanza hatuwataki wasijetulea balaa Africa hawachelewi kujigawia maeneo na kusema yao!
Israel ni mwanachama wa jumuiya ya kiislamu OIC,
Israel ina idadi kubwa ya Waislam kuliko wakristo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jina mjamaa wa kisasa asili yake imetokana na neno ujamaa wa kisasa ambaye muasisi wake ni mjerumani Great father KARL MAX na picha ya profile ni ya chama cha kijamaa cha kisovieti kwa hiyo mpaka hapo hakuna hata sehemu moja mchina anahusika🤣
Pia usisahau muasisi Lenin kutoka russia. Na Uchina ilifwata sera za kijamaa kutoka russia kama ambavyo Tanzania ya nyerere ilifwata. pia embu angalia asili ya Karl Mark ni ya wapi.
 
Mbona swali lako nimekujibu mkuu . Kuna njia nyingi za kujibu swali Mimi nazifahamu mbili
i, Kujibu swali kwa kutoa jibu moja kwa moja
ii, Kujibu swali kwa kuuliza swali
Swali lako nililijibu kwa kuuliza swali [ Kwa hiyo kwa sababu sehemu kubwa ya kiwanda/kampuni ya Intel ipo Israel basi Israel ndio mmiliki wa teknolojia?].

- kwa hiyo kwa sababu sehemu kubwa ya kiwanda cha I-Phone kipo china basi china ndio mmiliki wa teknolojia ya I-Phone?

- Kwa hiyo kwa sababu kiwanda cha Volkswagen kipo Rwanda Basi Rwanda naye ni mmiliki wa teknolojia ya Volkswagen?

N.B: by the way branch/Viwanda vya Volkswagen duniani vipo nchi za U.S.A, China , Israel, Vietnam, Ireland, Vietnam n.k
Kiwanda cha iPhone na development ama R&D center ya iPhone ni vitu viwili tofauti.

Kiwanda kinazalisha end products kutokana na technology ambayo inatoka mahali pengine. R&D center inafanya kazi ya utafiti ama uchunguzi na uvumbuzi wa bidhaa na teknolojia mpya.

Kama umeshawahi kutumia ama kuziona bidhaa za Apple kama iPhone, mara nyingi utakutana na maneno "Designed by Apple in California". China inafanya assembling tu.
 
Pole ndugu,hata Mimi mwanzoni nilihua Israel ni Taifa teule,lakini baada ya kuunua ukweli, Ile ni nchi ya kigaidi,hakuna cha uteule wala Mungu pale.
Itakuwa vema kama na sisi ukitupa huo ukweli ulioujua.
 
Ni jamii na Taifa ambalo ukifuatilia Historia yao unashawishika kusema lazima KUTAKUWA NA NGUVU NYUMA YAO ISIYO YA KIBINADAMU. Hata kabla ya uswahiba na Marekani au Ulaya hii jamii ilishaonyesha ni ya kipekee sana.
Tukija kwenye Maandiko yanayosema atakayekubariki nitambariki na atakayekulaani nitamlaani , mfano ujerumani likiwa Taifa lenye nguvu duniani chini ya Hitler walipowaua wayahudi zaidi ya Million 6- JE NINI KILITOKEA(ujerumani ilianguka vibaya).

Baada ya Waisrael kunyanyaswa sana huko Ulaya hadi Marekani aliwakaribisha na kuwapa sehemu ya kuishi na wengi wakakimbilia huko(USA), kwanini leo tusiamini kuwa ndio maana Marekani imebarikiwa kuwa Tajiri na nguvu kuliko yote duniani.

Kwanini tusiamini Kuanguka kwa Idi Amin wa Uganda ni sababu alivyowateka Waisrael hadi walipookolewa ktk Operation ya Makomando wa Israel.

Baada ya Nyerere kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kuwaondoa waisrael waliokuwa wametusaidia kuanzisha jkt kwanini tusiamini kwamba ndiyo sababu ya kudumaa kwa uchumi wetu tofauti na wenzetu wa Kenya ambao uhusiano wao uliimarika siku hadi siku na hata Israel kuwa ni Taifa mojawapo lililowekeza Kenya.

Hii mifano ni tone tu ktk mifano hai iliyopo kuhusu hawa jamaa tangu karne na karne kabla hata ya ujio wa Yesu. Hakuna aliyeweka uadui na Israel akasimama.

Hivyo wazungu kumkumbatia sio wajinga, hata nchi nyingi za Kiarabu zilishaamua kujiepusha kuwa na migogoro na Israel.
 
Pia usisahau muasisi Lenin kutoka russia. Na Uchina ilifwata sera za kijamaa kutoka russia kama ambavyo Tanzania ya nyerere ilifwata. pia embu angalia asili ya Karl Mark ni ya wapi.
Wewe si ulisema profile na jina langu ni kutoka China au umekosa hoja ?🤔 Hayo yote ya china kujifunza falsafa za Kijamaa za kirusi yote hayo nayajua na pia kuhusu Nyerere pia nafahamu sijui lengo lako ni nini hasa maana ni Kama unanifundisha vitu ninavyovifahamu au unadhani mimi kujiita mjamaa wa kisasa nimejiita kimakosa?🤔
 
Back
Top Bottom