Mbona wasukuma na wahaya wana akili sana za darasani 🤔

Mbona wasukuma na wahaya wana akili sana za darasani 🤔

LISHE LISHE LISHE

Ni kweli hilo jambo halina ubishi, sababu kuu ni samaki.

Samaki wana madini yakuweza fanya ubongo wa mtoto kutunza kumbukumbu.

Ukitaka mtoto mwenye Akili lishe yake kuu itokane na samaki..

OMEGA 3 ndio siri ya watu wa mwanza
 
LISHE LISHE LISHE

Ni kweli hilo jambo halina ubishi, sababu kuu ni samaki.

Samaki wana madini yakuweza fanya ubongo wa mtoto kutunza kumbukumbu.

Ukitaka mtoto mwenye Akili lishe yake kuu itokane na samaki..

OMEGA 3 ndio siri ya watu wa mwanza
sijui wanaongelewa wasukuma wa wapi, ndio hawahawa watani zangu au wengine? issue ya wasomi wengi inatokana na wapi walipata mwamko wa elimu mapema, ndio maana utaona makabila kama wahaya, wachaga, wanyakyusa, wapare, wangoni, wahehe, wabena, elimu ilifika mapema kwasababu wamisionari walifika kule mapema. 'songea kwa mfano, misioni kama Peramiho ni za zamani sana, shule kama Kigonsera, songea boys, na zingine zilikuwa za mission, walianza kusoma zamani. usukumani ukristo umeenda hivi karibuni na wasomi hata kama wanaonekana wengi ni kwasababu ya idadi yao kubwa nchini ila mwamko wa elimu sio wa zamani. kwa habari ya akili, omega3 ipo kwenye ndizi, parachichi, kiini cha yai na mafuta ya samaki, lakini vipo vyakula vingine kama nyama huwa vina madini ya chuma kusaidia kuboresha ubongo, na hii haiendani na kabila kwasababu huwezi kusema msukuma ana akili kwasababu anakula samaki, ukamsahau mkerewe, mkala au mjita ambao wanaishi na samaki kabisa. au wazaramo ambao chakula chao ni samaki na ugali. nimesoma na wasukuma wengi, nimefanya nao kazi, sijawahi kuona aliyenizidi akili, na mimi sio msukuma.
 
Hesabu yako ni nzuri ila inaweza leta matokeo tofauti na uhalisia pia kutokana na miundombinu. Kila kilomita 10 za mraba wilayani rombo na mreba kuna shule wakati ni zaidi ya kilometa 30 za mraba shinyanga ndo unapata shule moja ya msingi. Labda tutumie kiwango cha ufahuru maana kufahuru kunalindwa na kiwango flani cha max ambacho kila mtoto atakuwa amekivuka. Mfano kwa kila watoto kadhaa walioshinda kwenda form 5 wa kabila flani je niwangapi waliweza kuwa wasomi wa ngazi flani.
Nashukuru kwa hesabu hii bado hesabu itakuja vizuri tu mkoa wa kilimanjaro ni mdogo sana na shule ziko nyingi tu kwa hiyo utakuwa wa kwanza.Mimi natoka mkoa huo wilaya tofauti.Tarafa ninayotoka kuna shule za sekondari zaidi ya 10 achilia mbali shule za msingi.
 
Back
Top Bottom