Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Hata ukihamia usiku watu wakiamua kukupiga wanakupiga tu
 
Zaidi Ni Kuficha Aibu. Uchakavu Wa vifaa kama magodoro na vyombo visionekane. Pia vibaka na wezi wasiweze kuona mali wasipate kutamani
 
Ungenipa kazi ya ulinzi mrembo
 
We mtu nna godoro moja zaidi ya miaka kumi limeshachanika cover lake
Halafu lina madoadoa mengi katikati sehemu ya kiuno na juu sehemu ya kukoromea
 
Naona umeorodhesha vitu vya geto la demu wako na lako
 
Usalama muhimu. Usiku mtu anakuwa hajui mali ulizonazo tofauti na mchana.
 
Unahama mchana unafanya matangazo kila mtu ajue ameingia mtu mpya au fulan kahamia sehmu,usiku au jion maswal so mengi kila mtu yuko bize na shughul zake
 
1.Inategemea location ulipo, kwa eneo kama Dsm waendesha canter,vicarry mchana huwa hawakubali kutokana na usumbufu barabarani.

2.Kukwepa madeni

3.Hali ya vyombo vya mhusika
 
Wanakwepa msongamano wa magari barabarani. na mwenye kirikuu anataka aende arudi faster kuendelea na kazi. wenye kirikuu ukiwafuata watakwambia kazi hii tufanye usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…