Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Ila usisahau kumuaga mjumbe wa nyumba kumi haiwezekani kuhama ucku ucku kama fisadi anaemkimbia Magufuriiiiiii
 
Unakuta mtu unahama na mkokoteni mara masufuria yanaanguka kule huku jiko la mchina linamwaga mafutataa linaharibu vitu vingine kqdhalika vijiko vinaanguka kah!!

Ukicheki hapo ni baba na familia mko na mkokoteni mnaongozana nao pamoja na vitoto vingine vinalia chwiii chwiii ....!!!!!

Dah wacha nicheke mieee
 
Jua Kali LA mchana linaweza sababisha kunguni toka nje halafu foleni utazani gari ipo parking hapa ndo unaamua kuondoka usiku Kama popo.
 
Kiukweli zoezi la kuhama ni gumu sana,ikiwa unahama kutoka utumwani(kupanga) ukielekea kanani( nyumba yako zoezi huwa zuri sana wakati wa mchana kwakua Ni mazingira mapya yanayohitaji umakin usije lala na nyoka lakin kama unatoka utumwani(kupanga) na unaelekea nchi nyingine ya utumwani ( kupanga) usiku ni muda muhafaka sana kwasababu ya kujistiri lakin kuepuka macho ya watu maana upangajini Ni utumwa hasaaaa
 
Ishu ni unavyovihamisha vinafananaje.... wenye maflat TV ya kiplasma na ma LCD wanahama mchana... wenye machest friza yao na wanahama mchana..... we mtu anahama utafikiri anahamisha dampo au jalala unategemea ahame mchana...??!!

hahahahaha..... you made my day
 
Mh!!!hiyo ni watu tu wajijengea mazingira yao ya kuhama usiku haina maana yeyote ,ni fikra potofu tu kwa watu

Sio kujijengea tu.Nahisi kukwepa mchoro,hususani magodoro mengine ysmechakaa yana rangi ya udongo hayafai hadharani kwenye mwanga n.k.
 
Ishu ni unavyovihamisha vinafananaje.... wenye maflat TV ya kiplasma na ma LCD wanahama mchana... wenye machest friza yao na wanahama mchana..... we mtu anahama utafikiri anahamisha dampo au jalala unategemea ahame mchana...??!!

Mkuu umeua..umepiga mle mle kwenye madonda
 
Hamjambo waungwana!

Hili jambo la kuhama usiku badala ya mchana iko siri gani katika hiyo? Tofauti na kuhama mkoa 1 kwenda mwingine.

Ila nimejaribu kuchunguza iwe mtu anadaiwa au hadaiwi kodi mida ya kuhama alipo kwenda kwingine sio rahisi mtu kuhama mchana. Kama kuna anaelewa hiyo anijuze make shemeji yenu kaniambia kuhama kawaida ni usiku tu.

Na wenzetu nao huko majuu wanahama kama sisi usiku?

Karibuni mnijuze.

Alafu watu wanaohama awaachagi kitu hadi chuma la antena wanabeba.
 
MeinKempf;
Hiyo ndiyo sababu kuubwa zaidi ukiongezea na makandokando ya magodoro machafu, mito ilokwisha na meza zilovujika bila kurepewa
Kwa kuongezea kupunguza mazingira ya wizi maana watu wakikuona na vitu vya thamani inaweza kuwa kivutio cha kuweza kuvamiwa
 
Alafu watu wanaohama awaachagi kitu hadi chuma la antena wanabeba.
Mpaka mkaa waliouzima kwa maji baada ya kumaliza kupika na wenyewe kujifanya kiherehere cha kubaki... KUHAMA MCHANA KUNATAKA UWE NA VYA KUHAMISHA, SIYO VYA KUTUPA DAMPO
 
Kwa kuongezea kupunguza mazingira ya wizi maana watu wakikuona na vitu vya thamani inaweza kuwa kivutio cha kuweza kuvamiwa

Vitu vya thamani havijulikani siku ya kuhama tu mkubwa.... Aina ya maisha unayoishi, mavazi, chakula n.k vinaweza vikasema dhamani ya vitu ulivyonavyo...
 
Back
Top Bottom