Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Watu wanaogopa trafic. Manake wakiona tu kafriji kamepita urefu wa kirikuu cabin wanaanza usumbufu. Mbona huku uswazi tunahama na guta mchana kweupee.
 
He he he! Swali zuri sana. Imekuwa ni utamaduni. Unajua ukihama mchana wezi watachora ramani ya vile ulivyo navyo alafu usiku wanaviibukia. Zamani hata ukiwa na redio nzuri unaiweka chumbani alafu sebuleni unaleta spika. Ukiiweka sebuleni wezi wataiona... Duh, tumetoka mbali wandugu...
 
Hamjambo waungwana!

Hili jambo la kuhama usiku badala ya mchana iko siri gani katika hiyo? Tofauti na kuhama mkoa 1 kwenda mwingine.

Ila nimejaribu kuchunguza iwe mtu anadaiwa au hadaiwi kodi mida ya kuhama alipo kwenda kwingine sio rahisi mtu kuhama mchana. Kama kuna anaelewa hiyo anijuze make shemeji yenu kaniambia kuhama kawaida ni usiku tu.

Na wenzetu nao huko majuu wanahama kama sisi usiku?

Karibuni mnijuze.


Rudia utafiti wako.
Kuna jamaa yangu kahama majuzi alitoka saa 2 asubuhi.
 
wanahama usiku kwa sababu trafiki barabarani wanawasumbua wenye magari... ooh mara mzigo umezidi sasa mtu huwezi kukodi magari mawili kuhamisha vitu ni bora ukasubiri trafiki walale ndiyo upite
 
Majuu kuna kampuni maalum za kuamisha watu vitu vinafungwa kwenye mabox vinahamishwa tu muda wowote"
 
Kuna sababu nyingi za kuhama usiku,mojawapo ni hizi:
1.Kuficha udhaifu wa mhamaji(kujistiri),ama kuepuka fedheha.
2.Sababu za kiusalama.
3.Hulka ya kutopenda kujulikana(kueji-expose
kwa watu)
 
Kuna siri nyingi zimejificha, kwa mfano utakuta baba anajifanya pedeshee kitambi cha udalali nini, mama mtu nae ndio wale wasiopitwa na shughuli kila siku dera jipya na wote ni vibonge. Kitanda wanacholalia futi2 na nusu kwa 6 watu kama hawa hata tingatinga liwe ndio linabomoa nyumba hawahami mchana ng'oo.
 
Unakuta mtu unahama na mkokoteni mara masufuria yanaanguka kule huku jiko la mchina linamwaga mafutataa linaharibu vitu vingine kqdhalika vijiko vinaanguka kah!!

Ukicheki hapo ni baba na familia mko na mkokoteni mnaongozana nao pamoja na vitoto vingine vinalia chwiii chwiii ....!!!!!
 
Nilihama KINO MKWAJUNI saa 6 mchana, nikaingia MAILI MOJA saa 2 usiku, traffic wa Kimara Mwisho round about na wale wa Maili Moja, hovyo sana. Nawashauri msihame Mchana gt wenzangu
 
Back
Top Bottom