Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

uuuuwi nimecheka sana sijawahi kujiuliza hicho kitu.
 
Ni wachafu wanaogopa vyombo vyao visionekane.
 
hujawahi kaa uswazi weye ukapigwa plus.mafoleni na matrafiki kila kona
 
Inategemeana na mazingira na tabia zilizojengeka miongoni mwa jamii.

Wanaoishi mijini wengi hupendelea kuhama wakati wa usiku lakini vijijini wanahama wakati wa mchana.
 
Ukitaka kujua mali za mtu muangalie anavyohama.

Wengi wanaogopa kuhama mchana kwa sababu hawataki watu waone una miliki vyombo gani!

Wenzetu wazungu anavyotaka kuhama anahama yeye na begi lake mavyombo anauza au anagawa au anaviacha humo humo kabisa ila Waswahili wanahama mpaka na Makopo ya maua.
 
Usiku una privacy watu wasikufatilie wakajua unaenda wapi
 
Inategemea unahamia mtaa gani, wengine kuna mitaa tukiwa tunahamia tunaogopa vibaka maana mchana itakuwa muda muafaka kwa wao kuhesabu mali mpya inayoingia kitaa. Wewe unahamia wengine wanahesabia then wanakuja kufunga mahesabu baada ya siku kadhaa wakiwa na uhakika na mali iliyopo ndani.
 
Back
Top Bottom