Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Unajua jinsi kunguni au mende wanavyopenda sifa mkuu!? Yaani nyumbani wakija wageni tu ndio mipanya inakatiza sebuleni kama iko kwenye maulid. Sembuse kuhama mchana! Watacheza segere njia nzima.
 
Mtaani huwa tuna madeni mengi hivyo huwa tunakimbia madeni mangi anakudai, mama muuza vitumbua anakudai, bombani bill ya maji unadaiwa, mzee mwenye nyumba mwezi mmoja ukulipa mchango WA umeme so usiku panausika
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Wanaogopa mende na mipanya..iliyojificha kwenye sofa na kabati isonekane..sio siri huu utaratibu mbovu na upo nchi zetu za kimaskini hizi..

sijui kama hii nchi tutapiga hatua kama mtu kama wewe unakua mbeya kiasi hicho, je umefanya utafiti kabla haujauleta ushilawadu wako huo? mimi hua naona wengi tu hasa mwisho wa wiki wakihama mchana, kuna sababu nyingi pengine muda wa kutoka kazini hasa katikati ya wiki au hata kuepuka foleni ya magari hasa katika miji mikubwa, nashauri watanzania tuache umbeya na tuangalie fursa na kufanya kazi kwa bidii.
 
magodoro yashakuwa kama mtumbwi aibu majirani wakiyaona
 
Mimi sijawahi kuhama na mizigo yote isipokuwa huwa ninauza baadhi na kubeba vitu vya muhimu na lazima.So sijwahi kuwa na muda maalum wa kuhama.Lakini nadhani watu wengi wanaopendelea kuhama usiku huwa wana sababu zao.Huenda madeni,hofu ya kujadiliwa,kutokujiamini kutokana na samani wanazomiliki,masharti ya waganga,miiko ya kikabila,kukwepa usumbufu wa barabarani zikiwemo foleni na wengine huona huo ni muda mzuri kwa sababu familia inakuwa imeshamaliza pilika za mchana hivyo kila mwanafamilia hujumuika.Pia wengine waliishi kwa kujinadi sana huku wakiwa na siri zao ndani so huwawia vigumu kujianika hadharani hasa wakati wa kuhama.Hayo ni yangu mimi...
 
sijui kama hii nchi tutapiga hatua kama mtu kama wewe unakua mbeya kiasi hicho, je umefanya utafiti kabla haujauleta ushilawadu wako huo? mimi hua naona wengi tu hasa mwisho wa wiki wakihama mchana, kuna sababu nyingi pengine muda wa kutoka kazini hasa katikati ya wiki au hata kuepuka foleni ya magari hasa katika miji mikubwa, nashauri watanzania tuache umbeya na tuangalie fursa na kufanya kazi kwa bidii.
Umbea kuongea hali halisi.? Tambua kila mtu ana mawazo yake kulingana na mazingira anayoyafahami..wewe kama unafahamu hivyo hongera zako.

Sent from my SHV-E250L using JamiiForums mobile app
 
Nadhani ni issue ya security kwa wengi ili watu wasione au wasijue samani na mali mbalimbali mhamiaji mpya anazo. mimi ndio sababu iliyonifanya nihame usiku toka saa moja hadi saa saba usiku dah! nachukia kuhama
 
Toka nimekuwa huwa naona watu wanahama usiku najiuliza kwann sipati jibu na kingine kinachonishangaza sijawah kuona mtu akihama mchana

We magodoro chawa Na Mende zinakimbizana humo mubashara uhame mchana unataka kujiaibisha halafu godoro zenyewe ukilala ni kama umelala kwenye chaga jinsi zilivokonda hivo inakuwa vema ukichapa lapa night maana wambea wanakuwa wameshaegesha
 
Back
Top Bottom