Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Kwa experience yangu na ya nyie wengine humu Jf na huko mtaani, tumezoea watu wengi wanaohama makazi/nyumba au vyumba vyao huhama wakati wa usiku....je kuna kipi nyuma ya pazia kwa raia kutumia usiku kuhama na si mchana?.......

Hirizi huwa zinatulia vyema katika mkoba au mfuko wakati tulivu wa Usiku ila kwa mchana huwa zinasumbua sana hadi zinaweza hata zikakuumbua na ukaumbuka ile mbaya.
 
bora tuhame nao hawa hawa waliotuzoea hao wengine watakimbia maana hawana undugu
😂😂😂 Nimekuvulia kofia yaani hawa mbu wanavyotutesaga mpaka tunakesha jf usiku wa manane bado tu unatamani tuhame nao kwa kisingizio kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha?
 
😂😂😂 Nimekuvulia kofia yaani hawa mbu wanavyotutesaga mpaka tunakesha jf usiku wa manane bado tu unatamani tuhame nao kwa kisingizio kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha?
aliyekwambia wahenga waliongopa nani ?
 
Ni imani hasa kwa watu wenye uwezo wa chini na kati kiuchumi,

Nimefanya kazi kwenye kampuni ya kuhamisha maofisi na makazi,

Kazi zilikuwa zinafanyika kuanzia asubuhi hadi jioni au kesho yake mzigo unakiwa tayari,

Hatua ya kwanza ilikuwa kupack vitu kwenye boxes na bubbles,

Then tunapakia, tumefanya kwa watu binafsi kadhaa na watu mashuhuli kama mabalozi wa nchi jirani kadhaa
 
Kuhama mchana na jua kali sio jambo rahisi. Pia usiku watu ndio wanakuwa na muda baada ya kumaliza shughuli za kutwa.
 
Back
Top Bottom