Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Huu utaratibu wa kuhama nyakati za usiku ni nani aliuanzisha. Kwanini utaratibu wa kuhama usiku unapendwa sana na Watanzania wengi hasa wa huku uswahilini? Nini siri ya utaratibu huu? Karibuni kwa mjadala...
IMG_20190703_204351.jpeg
 
Mkuu hapo kuna mambo mengi, isipokua hakuna sababu moja ya msingi inayowafanya watu wapende kuhama usiku.

Mfano kuna wengine hawataki kujulikana kua wanahama, wengine ni imani za kishirikina zinawasumbua, wengine hawataki vyombo vyao vya ndani majirani wavione, wengine wanakuaga na madeni kwahio wanaamua kuhama usiku ili majirani wasije kuwapa taarifa wanaomdai na mengineyo mengi.
 
Hahahaha
 
Huu ni utaratibu ambao uliwekwa na mababu zetu kipnd cha karne ya 16 ,huu utaratibu ulienea sana kanda ya ziwa na viunga vyake,mwishon mwa karne ya 20,mwingereza akaanzisha utaratibu Wa kuhamisha vitu wakati Wa asubuhi na mchana kwa baadhi ya vitu,lakn karne ya 21 baadhi ya binadamu hawakuwa wepesi wakuhama asubuhi wao huhama ucku.baadhi ya taasisi huamisha mambo yao asubuhi na mchana,,
Jamii inayonizunguka huhama mchana kweupe..nadhan kwenu ndo utaratibu huu upo
 
Issue kubwa ni uchafu na baadhi ya vitu kachakaa. Wewe unakuta mtu ana kisofa kochi chake kimechakaa mpaka basi sasa kukitoa mchana anaona nouma.

Kingine,Vyombo vilivyopitwa na wakati, maplastiki kibao, chupa za maji nyingi utafikiri muuza gongo. Vigodoro vilivyochoka full mafua.

Yaani kwa kifupi ni kuficha uchafu na umaskini.
 
Back
Top Bottom