Japokuwa bado sijajua bayana hiyo kampeni ya Samia Must Go itafanyikaje, lakini Nina uhakika kabisa kwamba hata kama Rais Samia ataamua kuachia ngazi leo hii bado vitendo viovu vya utekaji Watu, utesaji na Mauaji vitaendelea kuwepo. Kwa jinsi ninavyofahamu, kiini Cha kuwepo kwa matatizo haya siyo Samia, Bali chanzo halisi Cha kuwepo kwa matatizo haya ni kutokana na kuwepo kwa Katiba ya nchi ambayo ni mbaya sana, pamoja na Sheria zingine ambazo pia ni mbaya au Sheria kandamizi,
Hivyo basi, kitu sahihi kabisa kinachopaswa kuondoka hapa nchini Tanzania ni Katiba iliyopo pamoja na Sheria kandamizi zilizopo. Katiba iliyopo ikiondoka, na Sheria kandamizi zilizopo zikiondoka, automatically hata mamlaka ya kuteka Watu waliyonayo hao Watekaji pia yataondoka, hatimaye sasa Tanzania itakuwa ni mahali salama na pazuri pa kuishi, Wananchi wote wa nchi hii ya Tanzania tutakuwa tumejikomboa kutoka Jehamu tulipo hivi sasa na kwenda peponi katika nchi ya ahadi ya asali na maziwa.