Binafsi naomba Lissu apite pamoja na uvunjifu wa kanuni aliofanya. Tatizo NEC wakifanya ivyo Lissu na wenzake watadhani wanaogopwa; wakati wenzao wameamua kutumia busara.
Kwa mtazamo huo ingekuwa serikali za mabeberu wangemkata bila ya kujali what next kwa sababu moja tu vyombo vyao vya ulinzi ulaya avipendi mikwara wala kuwekwa ransom.
We ukishika raia wao nje ya nchi utake ransom wako radhi watume askari wao kuja kwenye mission yenye gharama zaidi ya ulichoomba kuwatoa kama inawezekana na kama ikishindikana wapo tayari uwauwe tu labda wananchi wajichangishe wenyewe watoe hiyo hela. Lakini serikalini watakwambia wao awafanyi negotiations na terrorists.
Ndio CDM ata kwa wale ambao tungependa kuona Lissu anapewa nafasi ya kugombea, kutokana na kauli zao za vitisho unajikuta una split opinion upande mwingine unataka Lissu akatwe halafu tuone huo ubavu wao.