Uchaguzi 2020 Mbowe aitahadharisha Tume ya Uchaguzi kuhusu tuhuma za kupanga njama ya kumuengua Lissu kwenye mbio za Urais

"KUTOKUKAMATWA KUNAVYOMLIZA DOMOKAYA"

Well, Zaidi ya Mara 6 Tundu amejitabiria kukamatwa, amejitabiria akiwa Nje ya mipaka ya Tanzania ..amejitabiria akiwa ndani ya Mipaka ya Tanzania...na ktk Tabiri zote hajakamatwa, hajaguswa...je kiu yake ni kuwa "Huru" au kukamatwa?..definately ni "kukamatwa"

Kifupi Kutokukamatwa kwake walau hata mara moja tangu atue Bongo inauharibu vizuri ule Mpango Mkakati kati yake na Ndg Robert Amsterdam toka Amerika....Mpango uliojadiliwa ktk kikao cha Watu 7 jijini Brussels Siku 9 kabla hajatua Bongo ...Wao wakiamini kuwa Domokaya akitua Bongo tu atapokelewa Airport na UBA ya Magereza, Jambo ambalo halikuwa!

Ni dhahiri kupotezewa na vyombo vya dola kunafelisha Mchongo!...kwa namna wanavyopotezewa ktk Movement zao zilizo kisheria na zilizo kinyume cha sheria, na pamoja na juhudi zote za kuhakikisha "Tundu linakanyaga waya" kwa kila namna aidha kwa kutukana au kuvunja utaratibu ili kuchochea Kukamatwa na kuchukuliwa hatua ".Wameendelea kupotezewa! na inauma!..

Those Satanic Missions zilizopangwa zifanyike akiwa kadakwa zinafeli!..Mauaji ya wenyewe kwa wenyewe ktk kutawanywa kwa mikusanyiko yanafeli...imebaki kujichomea ofisi kama Ndafu au Meat chops za KFC na kisha kuripoti BBC,DW, KTN na VOA

Copy & paste
 
"Neno lake na litimie kwa kuwa hayo ni mapenzi ya Bwana.
 
Serikali haiendeshwi kwa mashinikizo ya watu bali na taasisi halali zenye watu ambao huweka pamoja mawazo yao yenye manufaa kwa taifa na wananchi wake na kutoa uamuzi wa kuendesha serikali.
 
#NoLissu,NoElection!#SasaBasi

Naunga mkono hoja kuwa kumwuengua Lissu kwa mizengwe, ili asiwe mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Taifa hili litakuwa limeweka rehani amani yake!
 
Bunge la 11 walifanya uzembe kukamilisha mchakato wa taifa la kifalme.Tayari wapo wanaoishi kifalme bila ridhaa ya katiba.
 
Kitu gani amefanya?
 
Naishi leo lakini naifikiria kesho, naiomba Tume ya Uchaguzi Tanzania itoe mchango wake katika kulinda amani ya taifa letu, hasa kipindi hiki tukielekea uchaguzi mkuu, pasiwepo na jambo lolote litakalosababisha kuzua taharuki isiyo ya lazima.
NEC inafanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo...vitisho kwa Tume havitasaidia...
 
Bila shaka utakuwa msitari wa mbele karibu kabisa na huo mstari mwembamba
 
mungu amekataa siku 4 7 kabla akatwi mtu hapa, na hakuna wa kumlazimisha mungu , wagombea wote wa vyama vyote niwatakie kampeni njema ,bila kusahau tume nanyi mungu awatie nguvu katika kutekeleaza majukum yenu katika kipindi hiki cha kutafuta viongozi wa taifa letu
 
Lissu aachwe wasimuengue,watapata kisingizio hawa wanyanyembe Chadema.
hata kama kunasheria kavunja wamuweke kiporo mpaka baada ya uchaguzi.
 
Haki si kupitishwa tu kuwa mgombea, bali hata kuenguliwa ni haki pia ili mradi sababu za kuenguliwa ziwe ni valid. Huwezi kufanya ujinga halafu eti ukasema No Lissu no election, kama kuna sehemu kakosea atapata haki yake ya kuenguliwa. Mwanakulitafuta mwanakulipata, kafuta haki ya kuenguliwa ataipata haki yake.
 
Alishasema atawapeleka barabarani. Nasikia magari yanawasubiri kwa hamu kubwa huko barabarani. Lissu anajua akiwekewa pingamizj hawezi toboa labda wa mwache tu. Rejea sababu za kufukuzwa ubunge ndiyo utajua kuwa hana sifa ya kugombea urais mpaka miaka mitano ipite.
 
Wasi wasi wangu mimi si tume ya uchaguzi, bali wadhamini wa Lissu na mahakama. Huko nyuma nilisikia wadhamini waliomba kujitoa na mahakama ikakataa ombi lao kwa sababu mshtakiwa hakuwepo mahakamani.
Inawezekana hiyo kesho wadhamini kwa maamuzi yao ama kwa kufika bei wakaomba kujitoa kwa kuwa mshtakiwa yupo, na mahakama inaweza kukubali kisheria ama kimaagizo. Hivyo kuanzishwa tena mchakato wa dhamana ambao kinamna yoyote ile unaweza kupelekea Lissu kuwa kizuizini huku muda wa kwenda tume ya uchaguzi ukikosekana na tume kutumia kivuli cha mahakama kutengua nafasi yake.
 
Haiwezekani. Kwani mwamuzi ni nani? Binge wala mawaziri. Ina maana kuwa mwamuzi wa haya ni mgombea mwenzake? Haileti maana!
 
Nawaomba NEC wachague zimwi nafuu kati ya KUMKATA Lissu na KUMTEUA agombee. Kwa maoni yangu ni nafuu kumteua agombee kuliko kumkata kwani sijaona sababu hasa ya kufanya akatwe ili asigombee lakini kama ataachwa agombee itawezekana chama tawala kushinda uchaguzi kwa kutumia vyombo vya dola ikiwemo NEC. NEC watumie hekima ili kutowatia watanzania katika majaribu. Watanzania wa leo si wale wa jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…