Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Eti katika hali ya uchumi wa namna hii miaka 50 ya uhuru kuna mtanzania anakejeli juhudi za kuiondoa CCM, Juhudi za Ukombozi kwa mara ya pili, HUYU MTANZANIA ni njaa ya tumbo au kichwani??? ili mkapa alisema uvivu wa kufikiri ambao actually ndo upumbav au sio hivyo??
 

cdm inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia...

Acha kushinikiza.magamba ndivyo walivyo kutuma?

Just a bunch of useless mind.
 
Mmiliki wa chama hawezi kukosa sifa za kuwa mwenyekiti wa chama. fullstop.

mods, funga huu uzi, now.
 
kweli aisee Yatupasa tujadili matendo ya watu na mienendo isiyofaa ya watu na watawala na Lazima utoe mifano ya watu hao ili wengine wapate kuelewa unachokisema.

Yani fasihi lazma iwe na wahusika
Sidhani kama ni suala la "kuachiana madaraka"... Cha muhimu ni demokrasia. Mbowe is not the best ever na naamini siku akijitokeza mwingine mwenye nia, na wanachama wakaona anafaa zaidi ya Mbowe, then demokrasia itachukua mkondo wake. Sio kazi ya Mbowe kuanza kutafuta wa kumuachia uenyekiti, bali ni jukumu la kila mwanachama anayehisi anaiweza hiyo nafasi kujitokeza na wanachadema wakiridhika kuwa ndiye mwenye uwezo kuliko wengine waliojitojeza, then wanamchagua...
 
mwekiti mwingine chadema utarajie baada ya miaka kumi ijayo wala siyo leo,mipango iko wazi kuwa mbowe ataendelea kuwepo sana halafu ukimuondoa mbowe wenye chama utawaambia nini.

Na lengo la kumuondoa ni nini?
 

Mawazo yako sehemu ni mazuri but yametawaliwa na muono mfupi. kwanza huwezi kusema Kamanda Mbowe hawezi kuifanya CDM kumiliki Media mbona nikitu kidogo ukilinganisha na makubwa aliyoyafanya. CDM unayoisema sasa Kamanda Mbowe ndie alieongoza kufika hapa ilipofika. Na Kubwa kuliko yote amemudu kuiweka hai CDM mpk sasa. Hivi huzioni Hujuma kubwa ccm na serikali yake zimeelekezwa CDM? Uliza NCCR na CUF wako wapi Mara baada ya Uchaguzi vimekufa kifo cha Mende. CDM wanamiliki UMMA, CDM wana miliki MALI, CDM hawasubiri uchaguzi kuwafikia wapiga kura Muda wote CDM wako kazini. CDM ina wabunge wengi ina madiwani wengi CDM inaongoza halimashauri sasa. CDM ina matawi kila kata. unataka nini zaidi. Mbowe Katengeneza kauli MTU YEYOTE ATAKAE SEMA UKWELI UMMA UNASEMA HUYO NI CHADEMA. CHADEMA CHAMA CHENYE KUSEMA UKWELI CDM ndie mkombozi anaesubiriwa kuwa peleka Watanzania kwenye nchi Ya ASALI NA MAZIWA.
 
Na wewe umepoteza sifa za kuongoza familia yako! did i say that?!
 

Itakuwa ni akili ya ajabu na imani ya aina yake, kufikiri na hata kuamini kuwa CCM wote wanafurahia uongozi makini wa CHADEMA unaotaka kuwang'oa madarakani na kukata mirija ya unyonyaji na mifereji ya ufisadi na ubadhirifu.

Na kwamba eti wana CCM watatoa ushauri wa namna gani CHADEMA iendeshwe vizuri zaidi ili iwaondoe madarakani kwa urahisi.

Kwamba wana CCM waliofikia hatua ya kutaka kuua wenzao kwenye mikutano ya hadhara, kuteka na kutesa wapinzani wao, wanafurahia mwenendo chanya wa CHADEMA unaoambatana na mafanikio makubwa, hasa katika ushawishi kwa wananchi, hazina ya vipaji vya uongozi, vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume, ndani na nje ya bunge pamoja na fursa zingine zote za majukwaa mbalimbali.

Kwamba CCM yenye ombwe kubwa la uongozi, unaosababisha kuwa na taifa lililoshindwa, watumwa wake wa mawazo, wanaweza kufurahia utumishi bora kwa watu unaotolewa na CHADEMA na kuendelea kukipandisha chati chama hicho na kukubalika kuwa chama mbadala kuanzia mwaka 2014 na 2015!

Media factor, ingelikuwa ni only and the only one remaining factor kama unavyotaka kuonesha, basi CCM wangelikuwa na uhakika wa kukubalika na kuendelea kutawala 'milele'.

Hoja zako zingine nyingi hapa tulishakujibu sana hapa, lakini kwa sababu nilizosema hapo juu, si ajabu umekuwa na utaendelea kuzirudia. Na mara nyingine tumekuuliza hapa, huwa una nia gani ya kutaka CHADEMA ianike wazi mipango mikakati yake! Ili watu wako waione au siyo?

Usiku mwema William. Jitahidi kutafuta hoja mpya. Utajibiwa kwa hoja pia.
 
Kunawakati watu lazma wakubali kila mtu ana kiwango chake cha mwisho cha kuweza kuongoza. Alipofikia mbowe ndo hapo hawezi kwenda zaidi tutafute mtu wa kuongeza kasi ikibidi aendelee kuwa mshauri tu
 
kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA uchaguzi ni 2014 mara ya mwisho ulifanyika 2009 kwanini mnataka MBOYE ang'atuke leo! na kwa utaratibu gani!,CCM imetawala inchi hii kwa miaka 50 hebu tuoneshe demokrasia kwa vitendo kwa kuwa pisha wengine waongoze inchi hii
 

mbowe pia aoneshe kuwaamini wenzake na asigombee tena ili tukuze democrasia
 
Kunawakati watu lazma wakubali kila mtu ana kiwango chake cha mwisho cha kuweza kuongoza. Alipofikia mbowe ndo hapo hawezi kwenda zaidi tutafute mtu wa kuongeza kasi ikibidi aendelee kuwa mshauri tu

Wewe unazo hizo sifa?
 
HOJA YAKO NI MUENDELEZO WA HOJA ZILEZILE ZA SIASA ZA MAJI TAKA.

Unataka kuaminisha wasomaji wako kuwa: WEWE UMEFIKIRI NA KUONA TATIZO LA CHADEMA KWA SASA NI MBOWE?????????????????????? Kwamba chademaikimwondoa mbowe baaaaasi! kila kitu kitakwenda sawa.
Kwa nini isiwe kuwa tatizo ni slaa,lama,shibuda au baregu????????????

akili zako hazina Akili!!!!!!!! this is my conclusion anyway!
 
Ulianza vizuri sana lakini mwisho wa hoja yako umejidhihirisha kuwa una fikra potofu juu ya Mh Mbowe. Pengine nia yako ni njema lakini umekosea kudhani kuwa mabadiliko ya uongozi yanatokea ili mradi tu ionekane kuwa watu wanapokezana madaraka. Uongozi ni vyema ubadilike kwa misingi ya kidemokrasia tu sio vinginevyo. Tukianza kusema kiongozi huyu aachie madaraka ili tu kuondoa maneno, kesho pia yatatokea maneno mengine kwa atakayekuwepo. Tutakuwa tuanongozwa na upepo wa propaganda badala ya busara. Mimi tuanchie mambo haya yaamuliwe na chaguzi za chama, sio upepo wa wakati.
 
Lazima ukweli utasimama tu,hivi wewe "Mbwenuu"katika majimbo ya mkoa wako kuna wabunge wangapi wa CDM acha kulewa rubisi halafu unatapika hovyo.Hakuna adui nayeweza kumshauri mgomvi wake ni silaha zipi zitumike dhidi yake.
hao wanaoutaka uenyekiti wangetumia njia sahihi kuna taabu gani?CDM ndio watakao amua nani ni nani ndani ya chama na siyo magamba watakaoamua hatima ya CDM.P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…