Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Per Diem

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
2,189
Reaction score
3,724
Nilikua namsikilizambowe anasema mkataba hauna ukomo.

Anasema yupo tayari kuamsha nchi nzima Kama bunge litapitisha

Leo nimeona ameongea kwa hisia sana.

---
"Watu wengine wanasema mkataba ni wa miaka 100, kwa mujibu wa mkataba huu unaweza kuwa miaka 200, huu mkataba hauna mpaka. Waliosema miaka 100 wamekadiria, huu mkataba hauna ukomo." Mhe. Freeman Mbowe

 
Ndio maana nilikuwa namsubiri kwa hamu sana huyu mtu azungumze, kwasababu nilijua tu, linapokuja suala la maslahi ya taifa hajui kumun'gunya maneno.

Nashangaa kuna vipofu walikuwa wanaulizia kwenye ule mkataba miaka 100 iko wapi, wao wakadai hawaioni, wakashindwa kutazama vipengele vingine kwenye ule mkataba, kisha wajumlishe na zao kichwani ili wapate jibu.

Kwa akili ya kawaida tu, kama mkataba hauna kipengele cha duration, at the same time panakuwepo na kipengele cha confidentiality, hapo anayejielewa hatakiwi kuuliza namba 100 iko wapi? common sense kwa baadhi yetu is not common!.

Rais na watendaji wake wanatakiwa kuhukumiwa vifungo virefu gerezani kwa hii dhambi waliyolitendea taifa letu, dhambi itakayoviumiza mpaka vizazi vijavyo, hawana huruma kwetu hawa viumbe, walaaniwe!.
 
Maisha ya Mtanzania ambaye hajui issues za mikataba anaweza kuona au asione hiki alichokisema Aikaeli.

Mtanzania huyu anayesoma kupitia mitandao anaweza kuelewa kidogo ila akapotoshwa na wanaoitwa walamba asali, hao ndiyo wabaya kwa sababu wanajifanya vipofu na viziwi huku hawana tatizo.

Mwisho ndiyo hawa hawa ikitokea dhahama wanakaa kimya kama kipindi kile cha corona.
 
Back
Top Bottom