Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Hiyo ni new world order mkuu hao wote wako kujenga ajenda moja ya kuharibu uhuru wa Nchi ya Tanzania. Ccm wamekubali kutumika kama maadui na mkombozi atatoka nje ya ccm.

Kiongozi wa ccm Akisoma hapa atadharau na kucheka kumbuka musa alimshinda farao akiwa mmoja tuu. Nyie ccm tayari Mungu amewashinda hamna dira tena.
 
Ni lini nyinyi ccm mmekuwa na uwezo wa kuchunguza akili za kizazi na kizazi kwamba hata kije kizazi cha tatu bado hakitakuwa na uwezo wa kusimamia na kuendesha Bandari zetu?

Huo mkataba unaokosa ukomo maana yake ni nini?

Huu utakuwa ni mkataba wa kwanza wenye kushangaza na kuduwaza, na huwenda ukaingia kwenye record za kidunia

Haiingii akilini,

Na badala ya kuja na majibu ya Wananchi, badala yake mnasema mnakomesha mafisadi yaliyokuwa yakipitisha bule mizigo hapo bandarini kwa kutumia majina ya viongozi!!

Huu sisi tunaita, ni uzembe wa viongozi
Hawa maandazi wanadai Uchumi wetu unekua sana hivyo wanaongeza tena Kodi ya 1000 kwenye simenti.

Hili suala la Bandari, litabadili mambo mengi sana.

Tusubiri.
 
Deep green, epa, meremeta, escrow, richmond...
Seasons za ccm ni kali ndo mana bongo movie sizitamani.

Naendelea kuvuta cigar kusubiri dp world..,
 
HILI SUALA YA HUU MKATABA NDUGU ZANGU INABIDI TUPIGE MAGOTI NA KUMUITA MUNGU KWA SAUTI KUU AINGILIE KATI MAANA HALI SI SHWARI NA WALA TUSIICHUKULIE POA KITU KISICHOKUWA NA KIKOMO MLIONA WAPI?

TUZIDISHE MAOMBI.
 
Fuatilia kujua hicho kipimo kimetolewa katika mazingira gani, maana zilizopo ni kwamba tende na asali toka arabuni zimelambishwa sana huko maeneo.
 
Kwa mfano baadaye ikionekana mkataba hauna shida na wewe umekwisha pre empty kwamba Wana CCM wote ni tatizo! Itakuwaje?

Yaani kosa lilelile la kuwaona wale ni wajinga linakuwa ni kinyume chake.

Hoja hii inajadiliwa Kwa hisia Kali na ikiambatanishwa na dharau wengine wakijiaminisha kwamba wao ni superman hawana chembe ya dosari kwenye ufahamu wao! Hata kama Wana hoja nzuri lakini wameivalisha matusi na udhalilishaji ambao wao wakitendewa ni kosa kubwa.

Kwakuwa tayari kunamvutano pande hizi mbili kila mmoja anajiona yupo sahihi dhidi ya hasimu wake inatakiwa Jambo hili lisimamishwe na tutafute mshauri mmbobevu ambaye afanye utafiti utakao tupatia majibu sahihi kwasababu wakati wa maandalizi ya kufikia makubaliano hayo hatujawahi kushirikishwa kuhusu utafiti uliofanyika na kupelekea uamuzi huo.

Jambo la pili ni kutafuta watafiti sahihi ikibidi tutafute nje ya Nchi kwasababu katika sakata hili limetupa picha halisi ya wasomi Wetu na hii ni ushahidi tosha kwamba uandaaji wa wanasheria katika nchi hii ni ule ule wa kuhakikisha unakuwa mlengo wa kushoto na unakuwa rigid.

Mwisho Jambo kama hili tunatakiwa kupata ufafanuzi Kutoka Kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na washauri Wakuu wa mambo ya mikataba walioteuliwa ambao naamini kama mkataba wameuona unafaa Kwa kadri ya utaalamu wao watuambie.

Hakuna mambo rahisi katika kupanga mipango Kwa kushirikisha Wananchi zaidi ya milioni 50 hili limeshuhudiwa katika mpango wa kujenga Uwanja wa Mkapa ,TV za digital,Chanjo ya Corona NK.
Jambo jema ni kujadili bila kutumia Sura ya uadui na itikadi katika Jambo lenye manufaa Kwa taifa tutachelewa Sana kufika.
 
Wala tusidanganyane IQ zilishapimwa huko USA na SA sisi tuko chini ya average tukubali tu ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom