Mamlaka ya bandari (TPA) imekanusha eti mkataba sio wa miaka 100 bali ni wa miezi 12. Machawa wanasambaza hilo "kanusho" wakidhani wanaisaidia serikali kumbe wanazidi kuharibu.
Kifungu cha 25(1) kinasema utekelezaji wa mkataba utaanza mara baada ya kusainiwa (promptly after signature of the State parties). Je, mkataba umesainiwa lini? Umesainiwa 25 October 2022. Hadi sasa imeshapita miezi 8 tangu usainiwe.
Kama kweli mkataba ni miezi 12 kama wanavyotaka kutuaminisha, it means imebaki miezi minne tu mkataba uishe. Sasa unawezaje kupeleka azimio bungeni kwa jambo ambalo limebakiza miezi minne!